jingalao umenena vyema. Kwa yeyote ambaye anaelewa, uzalendo wa JPM hauwezi kulinganishwa na chochote. Lakini pia, maisha ni hadithi. Siku zote nasema, JPM was the best President we never had. Huyu bwana angeweza kututengenezea mifumo ambayo ingeishi hata baada ya yeye kuondoka. Hebu angalia, baada ya yeye kuondoka hali imekuwa mbaya zaidi. Kwa sababu hakuelewa, kwa maksudi, kwamba Uraisi ni taasisi na uongozi ni dhamana yenye ukomo.
Tanzania hata tungepata kiongozi Malaika, bila uongozi wenye maono kuweka misingi ya taifa, inayolinda haki na uwajibikaji, nakuhakikishia, generation hata tano kuanzia sasa, watakuwa wanalalamikia haya wananchi wanayoyalalamikia leo. Tofauti ni kwamba hatujui kama watalalamika kwa nguvu au kwa sauti.
Maendeleo siyo maghorofa na barabara za lami.
Overall, siasa za Tanzania zimekuwa retirement plans za wale wenye connections, na siyo sehemu za uwajibikaji na uzalendo. Na tatizo linaanzia hapo.
Hata hawa unaowaona humu kama chawa, si kwamba hawayaoni haya madudu na utapeli wa watawala,, ukweli nini kwamba wengi wameshakata tamaa. Mwisho wa siku kila mtu anahitaji kulipa bills 💸 na maisha yaendelee.