Malyenge
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 6,658
- 3,646
Lengo la uzi huu si kupinga juhudi za serikali ya kupambana na teksi bubu ama bajaji zisizosajiliwa. Na wala si lengo la kukiuka sheria ya makosa ya mtandao.
Hoja yangu ni namna wanavyokamata na kutoza faini isiyoandikwa na sheria yoyote ya Tanzania. Wanatoza faini ya shilingi laki tatu kwa kosa la teksi bubu. Hawatoi risiti na wala hiyo teksi bubu hawaisajili baada ya kulipa faini.
Wanakuachia na hawakufikishi mahakamani pindi ukitoa laki mbili.Sasa nauliza hiyo manispaa ya Kinondoni waliowapa tenda hiyo ya kukusanya mapato ya pikipiki bajaji na teksi bubu wanafaidikaje ikiwa UBAPA CO. LTD wanatia mfukoni hiyo pesa na hawaipeleki Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni?
Ushahidi upo wasitake kujitutumua kudai sina ushahidi. Na hiyo tenda gani ya kufanya kazi saa nane usiku? Na hayo maswali wanayomuuliza abiria ikiwa hiyo ni teksi bubu wamepata mamlaka hayo kutoka sheria ipi ya Tanzania? Na huo usumbufu wa kusimamishwa mabarabarani kuhojiwa ikiwa gari yangu si teksi bubu serikali inaona ni sawa tu? Ile ibara ya katiba kuhusu uhuru wa kwenda mahala popote inatumikaje? Naomba tujadili.