UWT kumsaidia kukata Rufaa Maria aliyehukumiwa miaka 22 jela kwa kukutwa na nyama ya swala

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Siku moja baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa kumuhukumu kifungo cha miaka 22 Jela, Maria Ngoda Mkazi wa Mtaa wa Zizi la ng'ombe, Manispaa na Mkoa wa Iringa baada ya kumkuta na hatia ya kukutwa na ndoo yenye vipande 12 vya nyama ya swala kinyume na sheria, Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) chini ya Mwenyekiti wake Mary Chatanda imesema imesikitishwa na uamuzi huo na itaona jinsi ya kumsaidia Mwanamke huyo kukata rufaa na kumsaidia kupata uwakilishi mzuri ili aweze kupata haki yake.

Jana Millard iliripoti kuhusu hukumu hiyo ambayo imetolewa na Hakimu Mkazi Said Mkasiwa baada ya kujiridhisha kuwa ni Kweli Maria alikutwa na ndoo iliyokuwa na nyama hiyo ya swala yenye vipande 12 ndani yake vyenye thamaj ya Tsh. laki tisa ambapo ushahidi uliotolewa umesema siku ya tukio Maria alikutwa na ndoo hiyo yenye vipande 12 vya swala aliyokuwa akiiuza karibu na nyumba yake na hivyo nyama hiyo ikafikishwa kwa Mtambuzi na kubaini ni kweli ilikuwa ni swala na baada ya tathmini gharama yake ikafika Tsh. laki tisa.

Kwa upande wake Mtuhumiwa wakati akijitetea alikiri ni kweli alikutwa na ndoo hiyo ambayo alidai alikabidhiwa na Mtu aliyemtambua kwa jina la Fute na awali hakujua ina nyama ya nini ndani yake “Mheshimiwa ni kweli siku ya tukio nilikuwa kata ya Isakalilo na Mama Ziada nikiuza nyama kwenye ndoo sikujua ni nyama ya nini kulikuwa na vipande 13, kimoja akaondoka nacho yeye”

“Baada ya muda Mwenyekiti wa Mtaa akaja na Askari wakaniweka chini ya ulinzi wakisema nauza nyama pori, Mimi nikasema hii ndoo si yangu ni ya Fute wakaniweka kwenye gari hadi kwa huyo Fute, baada yakufikishwa kwa Fute licha ya kumtaja na kumtambua, Uongozi ulinilazimisha nibebe ndoo hiyo na kufikishwa kituoni na kufunguliwa kesi ya kukutwa na nyara za Serikali sambamba na kosa la uhujumu uchumi”

Hata hivyo hukumu hii imeibua hisia mseto kwa Wadau na Wanasheria kutokana na jinsi shauri lilivyoendeshwa kwani Mtuhumiwa hakupata uwakilishi wa kumtetea kipindi chote cha kesi yake hivyo baadhi ya Mawakili wamejitolea kukata rufaa na kumsaidia Mtuhumiwa katika kesi hii.
 
Siku moja baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa kumuhukumu kifungo cha miaka 22 Jela, Maria Ngoda Mkazi wa Mtaa wa Zizi la ng'ombe...
Mwananchi Mtanzania na mzawa huwezi hata kuonja nyama ya porini, tunaambiwa ni urithi wetu kwa vizazi vijavyo. This is bullshit! Nina miaka 65 hadi sasa, niliambiwa hivyo toka nkiwa mdogo mpaka leo kuhusu vizazi vijavyo. Sijawahi kuonja hata nyama ya Ngiri.

Toka kwetu hadi National Park ya karibu siitaji jina ni kilometa 8.

Maria aachiwe huru tena bila mashsrti.
 
Siku moja baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa kumuhukumu kifungo cha miaka 22 Jela, Maria Ngoda Mkazi wa Mtaa wa Zizi la ng'ombe, Manispaa na Mkoa wa Iringa baada ya kumkuta na hatia ya kukutwa na ndoo yenye vipande 12 vya nyama ya swala kinyume na sheria, Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) chini ya Mwenyekiti wake Mary Chatanda imesema imesikitishwa na uamuzi huo na itaona jinsi ya kumsaidia Mwanamke huyo kukata rufaa na kumsaidia kupata uwakilishi mzuri ili aweze kupata haki yake.

Jana @AyoTV_ iliripoti kuhusu hukumu hiyo ambayo imetolewa na Hakimu Mkazi Said Mkasiwa baada ya kujiridhisha kuwa ni Kweli Maria alikutwa na ndoo iliyokuwa na nyama hiyo ya swala yenye vipande 12 ndani yake vyenye thamaj ya Tsh. laki tisa ambapo ushahidi uliotolewa umesema siku ya tukio Maria alikutwa na ndoo hiyo yenye vipande 12 vya swala aliyokuwa akiiuza karibu na nyumba yake na hivyo nyama hiyo ikafikishwa kwa Mtambuzi na kubaini ni kweli ilikuwa ni swala na baada ya tathmini gharama yake ikafika Tsh. laki tisa.

Kwa upande wake Mtuhumiwa wakati akijitetea alikiri ni kweli alikutwa na ndoo hiyo ambayo alidai alikabidhiwa na Mtu aliyemtambua kwa jina la Fute na awali hakujua ina nyama ya nini ndani yake “Mheshimiwa ni kweli siku ya tukio nilikuwa kata ya Isakalilo na Mama Ziada nikiuza nyama kwenye ndoo sikujua ni nyama ya nini kulikuwa na vipande 13, kimoja akaondoka nacho yeye”

“Baada ya muda Mwenyekiti wa Mtaa akaja na Askari wakaniweka chini ya ulinzi wakisema nauza nyama pori, Mimi nikasema hii ndoo si yangu ni ya Fute wakaniweka kwenye gari hadi kwa huyo Fute, baada yakufikishwa kwa Fute licha ya kumtaja na kumtambua, Uongozi ulinilazimisha nibebe ndoo hiyo na kufikishwa kituoni na kufunguliwa kesi ya kukutwa na nyara za Serikali sambamba na kosa la uhujumu uchumi”

Hata hivyo hukumu hii imeibua hisia mseto kwa Wadau na Wanasheria kutokana na jinsi shauri lilivyoendeshwa kwani Mtuhumiwa hakupata uwakilishi wa kumtetea kipindi chote cha kesi yake hivyo baadhi ya Mawakili wamejitolea kukata rufaa na kumsaidia Mtuhumiwa katika kesi hii.
#MillardAyoMAHAKAMANI
 
Akram Azizi, Bw Pirmohamed na Suleiman Chambi waliachiwa bila shida, kisa matajiri. Ila mtanzania maskini kapigwa miaka 22. Ila Tanzania sijui nani atakuja kutuondolea huu uchuro.
Fisadi aliyefanya ubadhirifu wa mamilion ya hela anafungwa mwezi mmoja na faini ya laki mbili ila aliyeshikwa na mkaa, anafungwa miaka 30.

Hii nchi ni ya ajabu sana. Huyo dada, nyama yenye thamani ya laki 9 ndiyo afungwe miaka 22? Hii siyo haki
 
Acheni unafiki ninyi Uwt. Mnataka kuchukua ujiko. Mlikuwa wapi kumsaidia huyu mama asifungwe kwa hukumu mbaya?
20231108_084155.jpg
 
Back
Top Bottom