Tutafakari tenda ya kampuni ya Ubapa

Malyenge

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
6,658
3,646
Lengo la uzi huu si kupinga juhudi za serikali ya kupambana na teksi bubu ama bajaji zisizosajiliwa. Na wala si lengo la kukiuka sheria ya makosa ya mtandao.

Hoja yangu ni namna wanavyokamata na kutoza faini isiyoandikwa na sheria yoyote ya Tanzania. Wanatoza faini ya shilingi laki tatu kwa kosa la teksi bubu. Hawatoi risiti na wala hiyo teksi bubu hawaisajili baada ya kulipa faini.
Wanakuachia na hawakufikishi mahakamani pindi ukitoa laki mbili.Sasa nauliza hiyo manispaa ya Kinondoni waliowapa tenda hiyo ya kukusanya mapato ya pikipiki bajaji na teksi bubu wanafaidikaje ikiwa UBAPA CO. LTD wanatia mfukoni hiyo pesa na hawaipeleki Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni?

Ushahidi upo wasitake kujitutumua kudai sina ushahidi. Na hiyo tenda gani ya kufanya kazi saa nane usiku? Na hayo maswali wanayomuuliza abiria ikiwa hiyo ni teksi bubu wamepata mamlaka hayo kutoka sheria ipi ya Tanzania? Na huo usumbufu wa kusimamishwa mabarabarani kuhojiwa ikiwa gari yangu si teksi bubu serikali inaona ni sawa tu? Ile ibara ya katiba kuhusu uhuru wa kwenda mahala popote inatumikaje? Naomba tujadili.
 
Nilishajiuliza maswali mengi sana kuhusu hii kampuni na utendaji wake.
 
Kuna kampuni nyingine za kipuuzi eti wanakuja nyumbani kwako kupulizia dawa kisha lazima uwalipe kati ya elfu tatu hadi elfu tano. Hakika nitakuja kunanihiii MTU
 
Kuna kampuni nyingine za kipuuzi eti wanakuja nyumbani kwako kupulizia dawa kisha lazima uwalipe kati ya elfu tatu hadi elfu tano. Hakika nitakuja kunanihiii MTU

Kwanini unawaruhusu kupulixa hiyo dawa? Unawaacha wanakunanilii kila siku.
 
Kuna kampuni nyingine za kipuuzi eti wanakuja nyumbani kwako kupulizia dawa kisha lazima uwalipe kati ya elfu tatu hadi elfu tano. Hakika nitakuja kunanihiii MTU
Duuu... hata mimi niliwahi kukataa....wakasema nitafikishwa ofisi za kata kujibu mashtaka ya kukataa kupuliza dawa kwangu. Nikaona isiwe tabu hela yenyewe elfu tatu. Ila inaudhi sana...
 
Lengo la uzi huu si kupinga juhudi za serikali ya kupambana na teksi bubu ama bajaji zisizosajiliwa. Na wala si lengo la kukiuka sheria ya makosa ya mtandao. Hoja yangu ni namna wanavyokamata na kutoza faini isiyoandikwa na sheria yoyote ya Tanzania. Wanatoza faini ya shilingi laki tatu kwa kosa la teksi bubu. Hawatoi risiti na wala hiyo teksi bubu hawaisajili baada ya kulipa faini. Wanakuachiana hawakufikishi mahakamani pindi ukitoa laki mbili.Sasa nauliza hiyo manispaa ya Kinondoni waliowapa tenda hiyo ya kukusanya mapato ya pikipiki bajaji na teksi bubu wanafaidikaje ikiwa UBAPA CO. LTD wanatia mfukoni hiyo pesa na hawaipeleki Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni? Ushahidi upo wasitake kujitutumua kudai sina ushahidi. Na hiyo tenda gani ya kufanya kazi saa nane usiku? Na hayo maswali wanayomuuliza abiria ikiwa hiyo ni teksi bubu wamepata mamlaka hayo kutoka sheria ipi ya Tanzania? Na huo usumbufu wa kusimamishwa mabarabarani kuhojiwa ikiwa gari yangu si teksi bubu serikali inaona ni sawa tu? Ile ibara ya katiba kuhusu uhuru wa kwenda mahala popote inatumikaje? Naomba tujadili.
Yani unasimamishwa saa 8 usiku kuhojiwa na watu walovaa kiraia bila polisi pembeni unasimama ndo maana matukio ya ujambazi hayaishi watu mnajitakia mwenyewe hao UBAPA nyie ndo mnawaendekeza mm nishawagomea kuanzia ushuru wa mabango hadi parking na hawajawahi nifanya wala nipeleka popote na heshima imekuepo mtu usipaki hata dukani kwako vichochoroni hao hapo eti ushuru wa parking niliwambia kamwambie bosi wenu aje kudai iyo pesa na atoe maelezo nani kawapa iyo tenda na wapi.

Kuhusu mabango niliwambia kama wanajiona wanaume waling'oe wakaondoka
 
Kuna kampuni nyingine za kipuuzi eti wanakuja nyumbani kwako kupulizia dawa kisha lazima uwalipe kati ya elfu tatu hadi elfu tano. Hakika nitakuja kunanihiii MTU
Wslikuja nyumbani nikawatimua wao na Mwenyekiti Wa Mtaa wao eti elfu 5
 
Wanasimamisha gari wakiwa na polisi. Wakati polisi akiuliza nyaraka za gari wao UBAPA wanamshusha abiria uliyenaye kumhoji ikiwa amekodi gari yako. Akisema ni private abiria huyo huulizwa dereva anayeendesha jina lake nani au mmiliki wa gari jina lake nani. Akishindwa kujibu moja kwa moja wanaikamata gari na kuituhumu ni teksi bubu.
 
Back
Top Bottom