TUT (TVT&RTD) kuonyesha mahojiano ya JK 00.01hrs EAT | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TUT (TVT&RTD) kuonyesha mahojiano ya JK 00.01hrs EAT

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Halisi, Dec 20, 2007.

 1. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #1
  Dec 20, 2007
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Jamani TUT (TVT&RTD) leo usiku (kesho!!) wamesema wataonyesha mahojiano kati ya JK na waandishi jana IKULU, lakini naona kama wanaikebehi IKULU kwa kuwa wameambia wasitoe hadi tarehe 21 Desemba siku ya Ijumaa yaani siku ya kuadhimisha miaka miwili ya utawala wa JK.. Sasa kwani kama ni hivyo miaka miwili ilianza saa sita usiku? au ndio kama "Fataki" la mwaka mpya? Hii ya kusema watu wasubiri hadi siku hiyo wakati mahojiano yalifanyika jana, haina maana kabisa kwa Watanzania. Na nadhani wangefanya mfululizo kuanzia jana, leo na kesho kila TV/radio/gazeti likawa linatangaza ama kuandika litakavyo, ingekua na impact zaidi, lakini hili la kuzuia ni kali zaidi.
   
 2. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #2
  Dec 21, 2007
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Siku 100 Za Kikwete zilitangazwa kwa nderemo na vifijo na wiki moja kabla tayari mapambio yaliashaanza. Mwaka mmoja wa Kikwete nao kadhalika, huku kila wizara ikijivunia mafanikio. Na mjadala ulianza wiki ziadi ya moja. Ni wazi mafanikio yalikuwa ni ya kawaida sana tofauti ya matarajio waliyoahidi kwa wananchi. Miaka miwili ya JK, imefika kimya kimya. Kwa maoni yangu, si wakosoaji ama wapongezaji- wote tumeshindwa kutimiza wajibu vya kutosha kuichambua kwa kina hii miaka na kutoa mchango wa mapendekezo ya mwelekeo. Lakini hatujachelewa, wapo walioanza kidogo kuanzia wiki iliyopita; wengi watasema leo. Na najua baada ya hapo mjadala utafuata. Leo, saa 3 unusu kama ratiba itakwenda kama ilivyopangwa yatarushwa mahojiano ya TVT This Week in perspective kati yangu, Tendwa, Mpenda na Mwamunyage kuhusu Kura za Maoni za REDET- yatakuwa katika Lugha ya Kiingereza. Katika mahojiano hayo(kama yatakuwa hayajahaririwa) nimemsihi Rais avunje Baraza la Mawaziri(kama sehemu ya kuamsha ari, nguvu na kasi mpya kuelekea mwaka wa tatu wa uongozi wake). Lakini naona ujumbe wangu wangu umechelewa kufika, tayari Rais wetu ameweka msimamo.


  JJ
   
 3. K

  Koba JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2007
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  ...acheni kuchekesha nyie,nchi ya watu milioni 40 huku 99.999..% wanaongea kiswahili tuu,sijui mnataka kumfkia nani na nina uhakika hata sisi tukiyaona hatutaelewa maana najua ni shitty English with crappy accent...how convenient!
   
 4. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #4
  Dec 21, 2007
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Koba:

  Nakubaliana nawe kabisa. Lakini kama jina lenyewe la kipindi kilivyo ni kipindi cha kiingereza. Nadhani ni moja ya vipindi vichache vya TVT vya ndani vinavyoendeshwa kwa lugha hiyo. Labda ni kipindi maalum chenye kulenga hadhira yenye kuzungumza lugha hiyo ama watanzania wenye kufahamu kizungu. Ningefurahi zaidi kama ningealikwa katika kipindi cha "TUAMBIE".

  Lakini natumai wapo watakao elewa hicho kingereza mbovu mbovu na ujumbe utafika kwao. PK!

  JJ
   
 5. K

  Koba JF-Expert Member

  #5
  Dec 21, 2007
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  hapo mkuu i was trying to deliver the message in a funny way at your expense,glad you didnt take it personally...happy holiday from US!
   
 6. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #6
  Dec 21, 2007
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Usijali, wala sikuchulia binafsi. Ndio maana nimekwambia Pasua Kicheko(PK).

  Eid Mubarak, Merry X-Mas and Happy New Year.

  JJ
   
 7. J

  Jafar JF-Expert Member

  #7
  Dec 21, 2007
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Koba, ujumbe wako naona una dalili za chuki kuliko hoja. Are sure we are 99.99% kiswahili literacy ? What do you mean by "shitty English" ? Does a Nigerian, Chinese, Russian, Arabs speaks better English the British themselves ?

  Jenga hoja achana na chuki.

  Hicho kipindi hakikuanza leo, kipo kila week, na kinatumia English, why "crappy anccent" now ? Is it because JJ is from Chadema ?
   
 8. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #8
  Dec 21, 2007
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0

  Jafar

  Nilichokubaliana na Koba sio maneno na takwimu zake, ni dhana ya alichokisema kwamba kwanini katika taifa ambalo watu wengi wanazungumza kiswahili tuendeshe kipindi kwa kiingereza? Nadhani ufafanuzi wangu ulisaidia kumwelewesha. Hilo la maneno na takwimu alizotumia linahitaji mjadala. Endelea.

  Ila nimtetee tu- katika ujumbe wake hakunilenga mimi kama mimi(kwa kuwa naamini hajawahi kunisikia nikizungumza kiingereza, na ni vyema akanisikiliza usiku wa leo- sijui kama Jump TV wanaweza kuwa na link!); yeye alizungumza kiujumla nami nikamjibu kiujumla tu- kwa maana ya wazungumzaji wote.

  There was nothing personal!

  BTW: Natamani lafudhi ya kisukuma ingekuwa imeniingia mpaka kwenye kiswahili na kiingereza changu. Ingekuwa rahisi sana kuonyesha msisitizo. Sisi wasukuma huongea kwa mkazo na uzito(MZAHA)  JJ
   
Loading...