Tusitishane: Hakuna maisha baada ya kifo!

Hizi ni myths tu ambazo waarabu walikaa chini na kutafakari ni namna gani ya kuwa indoctrinate mapimbi na ndio maana huwezi kuzitetea kwa facts bila kuleta quotes za kuran hapa
Tunaomba ushahidi wa hiki ulichokiandika.
 
Swali gani ambalo uneniuliza halafu majibu yake umeyatafuta kwenye post hiyo ukayakosa?
Hilo ulilo elezea mambo ambayo hayajibu swali nililo kuuliza. Rejea swali langu kisha soma hiko unacho kiita ni jibu.
 
Kwa hiyo hiki tu ndio umeona kinahitaji ushahidi ila the rest post imejitosheleza bila ushahidi sio?
Kilicho baki nimeshakwambia ya kuwa hujajibu swali, hiki ni kipya na ninekuomba ushahidi najua huna na huwezi kuutoa ila nakuonyesha tu ya kuwa ni kwa namna gani ulivyo mjinga katika mambo haya.
 
Hilo ulilo elezea mambo ambayo hayajibu swali nililo kuuliza. Rejea swali langu kisha soma hiko unacho kiita ni jibu.
Swali lako nimejibu kwa mapana yake yanayo jitosheleza, target ya jibu sio kumridhisha muulizaji
 
Mkuu unajifunga sana kwa kutumia akili tu umesema kufa ni kama vile bado hujazaliwa yaani hujui chochote dunia lakini uko tumboni kwa nchi za wenzetu wanakuwa wshatambua kuwa ni mtoto wa kike au kiume then ukazaliwa ukaishi ndo uhai sasa ukafa tena duniani kwa nn usiwe tena mzima na kuishi maisha mengine kama continuation of trend

Yaani tulianza kuwa wafu tukiwa tumboni tukaishi tukafa duniani kwa hyo tunaweza kuwa hai katika maisha mengine full stop epuka kula viporo asubuhi unaleta mawazo mgando hapo nimekujibu kwa fikra kama wewe sio vitabu
Binafsi naamini uhai huanza tangu mimba inapotungwa. Waliopo tumboni mwa mama zao wapo hai kwani wanazo sifa zote za viumbe hai.
 
Kilicho baki nimeshakwambia ya kuwa hujajibu swali, hiki ni kipya na ninekuomba ushahidi najua huna na huwezi kuutoa ila nakuonyesha tu ya kuwa ni kwa namna gani ulivyo mjinga katika mambo haya.
Hilo nishalifanya, sitegemei kulirudia tena
 
Swali lako nimejibu kwa mapana yake yanayo jitosheleza, target ya jibu sio kumridhisha muulizaji
Usahihi wa jibu ni kujibu ulichoulizwa, sasa unapo ona umejibu ambacho hujaulizwa na ukaona kwamba umejibu wakati majibu yanajulikana huu ni ugonjwa wa akili.
 
Usahihi wa jibu ni kujibu ulichoulizwa, sasa unapo ona umejibu ambacho hujaulizwa na ukaona kwamba umejibu wakati majibu yanajulikana huu ni ugonjwa wa akili.
Unaweza kunionesha ni Kipi ambacho nimekijibu ambacho wewe hujakiuliza?
 
Sawa ila process nzima kuanzia mimba ina wiki mpaka miezi sita ndo anakuwa mtoto means anaanza kuwa mfu baada ya wiki kadhaa hao wazungu tu wanaanza kumtambua kuwa ni jinsia gani baada. Ya wiki kaadhaa huko mwanzo inakuwa bado sio kiumbe hai kabisa mpaka mungu atakapokipa roho
 
Of course yani, maisha yapo duniani tu ukifa hakuna maisha kuna aina nyingine ya uhai na njia yake ya kuendana nayo
 
Nijuavyo wapo binadamu baadhi wameyajua matamanio ya binadamu kiujumla!,namaanisha wanajua ubongo wa binadamu unataka kusikia nini..? Unafikiria nini juu ya mambo mtambuka na binadamu anahisia zipi juu ya maisha yake!.

Hilo sijasoma mahali wala mada hii sijasoma mahali bali ni fikra zangu!,na moja ya kumfaulu mwanadamu ni kupitia matamanio yake iwe kihisia au kimwili.(fikiri)
Hayo ni mambo yanayoweza hata kupindisha fikra sahihi na kuleta fikra potofu pandikizi isiyosahihi!.

Sijaona sababu haswa inayowafanya watu wakubaliane kuwa kuna maisha baada ya kifo!!!! Labda ni upofu wangu na ujinga nilionao!

Kwangu kifo na uhai ni kama hali mbili zinazokinzana na Wala sio mabadiliko ya daraja la kutoka uhai huu na kuingia uhai mwengine!. Kama uhai unasifa za kuwa na utendaji kwa maana ya kupumua,kula,kunywa, kutembea n.k Basi kifo ni kinyume chake ambapo kuwa kinyume kunamaana ya kinyume haswa! Kilichokufa hakina fikra,hakili,hakitendi n.k

Kufa ni sawa na kuwa kabla haujazaliwa!.. kabla haujazaliwa hukuwa na fikra,hukuwa chochote hukua wewe unaejihisi hivi sasa,wewe na utambuzi huo ulionao. Baada ya kuzaliwa (kuwa hai) basi umekuwa wewe na kuwa na fikra na utambuzi huo ulionao na wewe kujihisi hivyo unavyojihisi!.. kifo ni hali inayokuja kuharibu hali hiyo,itakuwa hainamaana ya kifo Kama kinachokufa Kama bado kutakuwa na sifa za uhai Kama kufikiri,kutenda n.k

Ulimwengu tuliopo unasifa ya kuharibu na kutengeneza,tupo katika sifa ya vinavyoharibika na pia tupo ktk ulimwengu wa sifa ya vinavyojiripea ktk uharibikaji huo!.. namaanisha ipo namna ya uhai wetu umejitengenezea namna ya kusurvive ktk ulimwengu huu wa kuharibika! Na namna hiyo ni "kuzaliana" hii ndio dhana pekee nayoilewa kama uendelezaji wa uhai ktk ulimwengu!. Nafasi iliyopo ya sisi kuendelea kuishi ni ktk kuzaliana. Kifo ni kama gari la taka linalokuja kukusanya taka zilizopoteza sifa ya kuwa hai!.. ukifa ndio mwisho wa kila kitu kuhusu wewe Ila kuzaa ndio muendelezo wa uhai uliokuwanao wewe.

Niwape hongera kwa wanaojua kucheza na akili ya mwanadamu ili kufanikisha malengo yao ya kuishi vizuri na kuongoza!.

Kila kitu ambacho kinakuja kwenye maisha yako kitakuathiri kutokana na vile unavyokichukulia!. Kila hisia iliyopo mwilini mwako inakazi yake lkn akili ndio inakazi ya kuongoza hisia hizo, so nishauri lako uchague uongozwe na mitikisiko ya hisia au utumie hiyo mitikisiko ya hisia Kama njia ya kubiidisha ubongo wako ufikiri zaidi!.. it's your choice.
Kama husomi vitabu vya dini,utabaki kuwa wa shetani tu mkuu
 
Ngoja na mimi niweke comment yangu.
Ili uweze kujua kama kuna maisha au la baada ya kifo kwanza utatakiwa ujue
Maisha ni nini.
Mtoa mada hebu nakuomba au mtu yoyote anipatie maana ya maisha. Yaani ni kitu gani kinachokufanya uwe hai.

Au tukienda deep zaidi tutaona kuwa cells zetu ndio unit ya uhai kwa mujibu wa biology. Sasa kitu kinachofanya cells ziwe hai ni nini!?

In short hakuna anayejua iwe Wanasayansi au watu wa imani uhai wetu upo wapi. Ukigongwa gari ghafla tu unakufa na mwili unakiwa wa baridi. Sasa ni kipi kinaufanya mwili uwe wa moto.

Kwa ewezo wetu wa kufikiria kwa sasa hakuna anayeweza kujibu hilo.

Iwe sayansi au dini. Sana sana Wanasayansi wataleta theory ambayo haitofautiani na Imani za kidini.
 
Maisha baada ya kifo ni hadithi zakufikirika tu

Mara sijui kuna adhabu ya kaburi kuudanganya umma kua malaika anakuja kaburini na mijoka kukupa adhabu eti na watu kweli wanaamini......ni ujinga tu
Hata binaadamu mwenyewe jinsi anavyopatikana ni jambo ambalo tunalikubali kwa sababu tunaliona na sisi ni sehemu yake,lakini ukiangalia jambo lenyewe zima kuanzia yale majimaji hadi kuzaliwa kwa mtoto ni jambo la ajabu kama ingekuwa ni kuhadthiwa basi tusingekubali tungeona ni jambo la kufikirika tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom