Hivi kuna maisha baada ya kifo?

Grace glory

JF-Expert Member
Feb 17, 2018
330
349
Habari wana JF,

Hivi kuna maisha baada ya kifo?
Au bado sijui maana ya kifo?
Yaani babu yangu liyemzaa bibi yangu bado anaishi baada ya kufa? Kwamba hawa waliokufa wanaishi ila waneshakufa?

Au naombeni maana ya kifo ili ning'amue huu mzozo.

(Kuna mtu kaniambia kuwa kuna maisha baada ya kufa)
 
Mkuu,Hakuna maisha baada ya Kifo wala kabla ya Kuzaliwa.Wewe utaendelea Kuwepo na Bibi na babu yako bado wapo ila hawapo HAI na hawana Maisha kama ambavyo unavyoyaishi hapa DUNIANI ila wapo Ila HAWAISHI
 
ndugu maisha baada ya kifo yapo. kuna umilele baada ya haya maisha ya duniani binadamu huishi milele. maana binadamu ana roho ambayo haifi kinachokufa ni mwili.
umilele wa binadamu baada ya maisha hapa duniani hutegemea sana alivyoishi hapa duniani na kuna sehemu mbili tu ambazo mwanadamu anakwenda baada ya maisha hapa duniani. ni either uzima wa milele au moto wa milele.
 
Kwanini una roho alafu haujawahi kupata uzoefu njee ya mwili wako ? Na kama ulishawahi ebu tueleze kidogo
 
Habari wana JF,

Hivi kuna maisha baada ya kifo?
Au bado sijui maana ya kifo?
Yaani babu yangu liyemzaa bibi yangu bado anaishi baada ya kufa? Kwamba hawa waliokufa wanaishi ila waneshakufa?

Au naombeni maana ya kifo ili ning'amue huu mzozo.

(Kuna mtu kaniambia kuwa kuna maisha baada ya kufa)
"........(Kuna mtu kaniambia kuwa kuna maisha baada ya kufa)".
Sasa wewe unaamini lipi? Kuna maisha au Hakuna maisha baada ya kifo??
Huyo mtu aliyekuambia kuna maisha baada ya kifo mng'ang'anie/mkomalie akuthibitishie hivyo.
Wewe pia waweza kujithibitishia kwa kufanya yafuatayo:-
1.Chukua bakora/fimbo kamchape babu yako au kumfokea juu ya kaburi lake halafu ulete mrejesho hapa ili na wale walio na akili/imani kama yako wajifunze.
2. Pitia maandishi vitabuni, rejea maelezo ya mdomo ya jadi (Traditional History) na mengineyo mengi kuhusu hoja hiyo halafu ujipime kama kweli woote hao walivyoamini au kusema kuna maisha baada ya kifo walikuwa hawana akili ni wajinga ila ww ndo mwenye akili.
3. Kataa kabisa hakuna maisha baada ya kifo ili uachane na mahangaiko ya kutafuta eti kama kuna maisha baada ya kifo au la na uwe huru usihangaike. Kama yapo-Yapo; kama hakuna Hakuna. Ww katafute pesa full stop.
 
Habari wana JF,

Hivi kuna maisha baada ya kifo?
Au bado sijui maana ya kifo?
Yaani babu yangu liyemzaa bibi yangu bado anaishi baada ya kufa? Kwamba hawa waliokufa wanaishi ila waneshakufa?

Au naombeni maana ya kifo ili ning'amue huu mzozo.

(Kuna mtu kaniambia kuwa kuna maisha baada ya kufa)
kinadharia tunajifunza hivyo kupitia vitabu vitakatifu vya dini 🐒

kwa uhakika na ili kuthibitisha hilo kwa vilt vitendo ni lazima ufe kwanza au uwe ndani ya kifo 🐒

ndipo sasa utathibitisha kama kweli maisha yapo au hayapo baada ya kifo....
 
Ukiwa hai na ukawa umesinzia/umelala fofofo na kama hauoti ndoto yoyote muda huo, je utaweza kuhisi uwepo wowote wa maisha? Kama hauwezi kuhisi uwepo wa maisha ukiwa tu usingizini, inawezekana vipi mtu hauna pumzi (umekufa) kisha uweze kuhisi uwepo wa maisha?
 
Kwanini usiishi Sasa ndugu!? Kwan usubiri mpaka ufe!?.…Maisha ndio Haya, HAKUNA MAISHA BAADA YA KIFO!
Kuna point hapo. Hebu bainisha zaidi: Hakuna maisha au Hakuna Uhai baada ya kifo?
Niaminivyo mimi:
1. Maisha ni mzunguko (life cycle) tangu mimba, mtoto, kijana mtu mzima, uzee hadi kufa.
2. Uhai ni kile kinacho kufanya wewe (Nafsi) uwepo, ujibainishe na binadamu wenzako pamoja na viumbe wengine i.e. Ujitambue, Binadamu wenzio wakutambue, na viumbe wengine watambue uwepo wako na utendaji au uwajibikaji wako. Kwa ufupi ni Roho yako. Yapo maandiko yasemayo "Roho ndiyo itiayo uzima....." Biblia Yn 6:63. Sijui Quran inasemaje juu ya hilo.
Roho ikiachana na mwili wako, Mwili wako huo utaitwa Maiti (Mfu) na wewe(Fulani kwa jina) utapata cheo (Wadhifa) na kuitwa Marehemu.
 
Hakuna empirical evidence, ishi sasa na kesho ie kama unaweza kuishi vizuri now usijibane, pia kwa imani yako kama unahisi kuna maisha yajayo jiandae.

Utajisikiaje uache kujiandaa alafu unafariki unakuta kuna maisha mengine? Ha ha ha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom