Tusitishane: Hakuna maisha baada ya kifo!

»Swali hili limekuwa likihojiwa kila mahali tangu nyakati za mababu. Ayubu alijiuliza swali hili ".........mtu akifa je! atakuwa hai tena?...." (AYUBU 14:1-2).

»Katika swali hilo kuna maswali hayo madogo yafuatayo:-
1. Nini hutokea baada ya mtu kufa?
2. Je, Maisha ni mtindo wa Kutoka na kurudi duniani?
3. Je, Watu wote huenda sehemu moja au kila mtu huenda mahali pake?
4. Je, ni kweli kuna mbinguni na Motoni?

»Biblia inatuambia si tu kwamba kuna maisha baada ya kufa bali ni maisha ya milele ambayo " Macho hayajawahi Ona, masikio hayajawahi sikia wala akili zetu hazijawahi fikiria ambacho Mungu ameandaa kwa ajili ya wale tu wampendae" (1 WAKORINTHO 2:9).

»Yesu Kristo, Mungu katika mwili alikuja ulimwenguni kutupatia zawadi ya maisha ya milele kwa sababu hiyo akawa tayari kuteswa kwa ajili ya dhambi zetu(ISAYA 53:5). Yesu kristo aliteswa( alisulubishwa)na kuwa tayari kuutoa uhai wake kuwa fidia ya dhambi zetu.
Siku ya tatu alijidhihirisha yeye mwenyewe kuwa ni mshindi juu

ya kifo na akafufuka kutoka kaburini. Baada ya kufufuka alikaa ulimwenguni kwa siku arobaini na alikuwa amekwisha shuhudiwa na mamia Kabla ya kwenda Mbinguni. WARUMI 4:25 inasema"....alitolewa kwa ajili ya makosa yetu , na kufufuliwa ili tupate kuhesabiwa haki".

»Ufufuo wa Yesu Kristo lilikuwa ni tukio lenye uthibitisho ulio dhahiri. Ufufuo wa Yesu kristo ni jiwekuu la pembeni katika Ukristo. Kama Yesu asingefufuka , Ukristo usingekuwepo kwani angeonekana Yeye mwenyewe kuwa ni mwongo kwa kusema kuwa atafufuka na asifufuke. Kwa sababu Yesu Kristo alifufuka Kutoka katika mauti, tunaamini kuwa nasi tutafufuliwa . Ufufuo wa Yesu ni uthibitisho mkubwa kuwa kuna maisha baada ya kifo. Kristo pekee ndiye wa kwanza katika wale watakao fufuliwa na kuishi tena.

»Kifo kilikuja kupitia mtu mmoja Adamu, ambaye kwa yeye wote tunakufa. Lakini kwa wale walio katika familia ya Mungu kwa njia ya Imanikupitia Kristo (YOHANA 1:12) watapata maisha mapya(1 WAKORINTHO 15:20-22). Kama Mungu alivyoufufuamwili wa Yesu, ndivyo tutakavyofufuliwa Yesu Kristo akija kulinyakua Kanisa lake (1 WAKORINTHO 6:14).

»Biblia inasema kuwa tunakufa mara moja na baada ya kifo ni hukumu (WAEBRANIA 9:27).Walioishi maisha yanayompendeza Mungu wataenda kuishi maisha ya milele Mbinguni lakini ambao walimkataa Bwana Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao watatupwa katika moto wa milele, vivyo hivyo nao watateseka milele (MATHAYO 25:46).

»Motoni, kama ilivyo Mbinguni si rahisi kueleza jinsi kulivyo lakini ni mahali panapotisha sana. Ni mahali ambapo wasio haki huishi maisha yao milele yote kwa hukumu ya milele Kutoka kwa Mungu mwenyewe. Motoni kunaelezwa ni kama Shimo refu lisilo na ukomo( bottomless pit) (LUKA 8:31, UFUNUO WA YOHANA 9:1)mahali hapo mtu mwovu huenda mara tu baada ya kukata roho, na baada ya hukumu ya siku ya mwisho watatupwa katika ziwa la moto unaowashwa kwa sulfur mchana na Usiku, milele na milele (UFUNUO WA YOHANA 20:10). Motoni kutakuwa na kilio na kusaga meno (MATHAYO 13:42).

»Mungu hafurahishwi na kifo cha mwenye dhambi lakini hutaka watubu ili waepukane na adhabu ya milele (EZEKIELI 33:11) Lakini hawezi kutulazimisha kama tukimkataa huheshimu maamuzi yetu yapo hafurahii.

»Maisha ya hapa duniani ni mtihani na maandalizi ya maisha ya baadaye baada ya kufa. Kwa wanaomwamini Yesu maisha yao baada ya kufa ni Mbinguni. Kwa wasiomwamini Kristo maisha yao ya milele yatakuwa katika ziwa la moto.

»Namna gani tunaweza kuepukana na ziwa la moto? Kuna njia moja pekee - kupitia kumwamini Yesu Kristo. Yesu alisema "...mimi ndimi huo Ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele.." (YOHANA 11:25-26).

»Zawadi ya bure ya uzima wa milele inapatikana kwa wote kwa kumwamini Bwana Yesu YOHANA 3:36 " Amwaminiye mwana(Yesu) yuna Uzima wa milele; asiyemwamini Mwana(Yesu) hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia".

»Hakuna nafasi ya kutubu baada ya kufa. Hatima ya maisha yetu ya mileleinafanyika hapa hapa duniani kwa kumkubali au kumkataa Bwana Yesu Kristo. "Wakati uliokubalika ni sasa....siku ya wokovu ndiyo sasa" (2 WAKORINTHO 6:2).

»Kama tukiamini kifo cha Yesu Kristo kuwa ni malipo halali ya dhambi zetu , tunaishi maisha ya milele Mbinguni baada ya kufa .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maisha baada ya kifo yapo Sana.
Ndo maana mungu aliweka siku ya Kiama.
Na siku ya malipo.
Na akaweka pepo na Moto
Ndo hivi tu mkuu hakuna neno la kuongeza..?
 
Mt 11:25-26 SUV

Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako.

Kivipi kifo Cha huyo yesu kiwe malipo ya dhambi..? Alimlipa Nani..? Kwa misingi ipi ilihitajika kuwa malipo ya dhambi na ni kanuni ipi ya ulimwengu ilihitaji yeye afe ili dhambi zisamehewe..??
 
Baada ya hizi story nikifikiria padri nae hutomba wake za watu, sheikh hula nguruwe kwa kificho nawaza tu je hawa jamaa hawaelewi kuna maisha mengine baada ya kifo?
 
Mtu aliyekufa ni sawa na mtu ambaye hajazaliwa,yaani kabla mimba haijatungwa hukua kitu na ukifa vivyo hivyo huwi kitu chochote hayo mengine ya moto,mbingu,mizimu na mengineyo ni hadith za kale za kigiriki hazina ukweli wowote!
 
Baada ya hizi story nikifikiria padri nae hutomba wake za watu, sheikh hula nguruwe kwa kificho nawaza tu je hawa jamaa hawaelewi kuna maisha mengine baada ya kifo?
Wao wenyewe wapo ktk mtambuka na wanaanzaje kuacha vitu vitamu vitamu kwa kitu mtambuka..!😂

Mkuu hayo ni mambo ya utawala tu swala ukishajua kucheza na watu kiakili basi umeula.
 
Jaribu kula sumu ukachungulie huko halafu urudi
Hii watu wengi sana wamefanya hili la kufa mara moja na wakarudia Hospitali! mpaka leo ukiwambia kufa !! mnapigana, kuna mtu anapenda kuacha ugali na firigisi? inavonogaga???
 
Ha ha! Naelewa dhana ya Uungu ila sijui ni Mungu yupi ndio kaumba ulimwengu! Kwa maana Miungu wanaotwajwa na walioandikwa kuwa wao ndio chanzo cha ulimwengu kwangu naona bado hawajajitosheleza! Au wanapewa sifa zilizozidi uhalisia.. so ili unielewe hapo usiweke Umungu bali Uungu!.. Uungu kinaweza kuwa chochote aidha ni nguvu yenye intelligence this is what i think! Ndio maana unaona jibu Kama tata.
nakubaliana nawe kwamba WANAVYOFUNDISHA NA BAADHI YA WATU SIVYO HALIVYO KABISA na swali linatokea kwanini hakuna njia moja ya wazi ili aliweke vizuri?

ukipata muda pitia na hii pdf ina maswali muhimu
 
Attachments

Usitutishe:
Hakuna ndoto baada ya kulala.
 
Kwanza nyinyi mnaosema kuwa kunamaisha baada ya kifo hamjaleta ushahidi isipokuwa mnaamini tu kuwa kuna hilo Jambo!.. hakuna mfu yoyote alieweza kutoka ktk huo ufu na akaleta majibu ya uhakika juu ya maisha baada ya kifo!.. (na najua hilo haliwezekani maana kilichokufa ni kimekufa na hakuna kipya hapo!)
Mmekuwa mkihusisha zaidi hayo maisha na maswala ya kiroho na hata hiyo roho hamjawahi thibitisha uwepo wake!.
Hakuna uhusiano wa moja kwa moja wenye wenye uhalisia wenye kuonyesha kuwa kilichokufa kinaenda kuwa hai ktk ulimwengu mwengine! Hakuna uthibitisho wa hilo!. Uhai unamazingira yake kwa haya unayoyaona,kuyahisi na kuyasikia.
Unapata ugumu wa kuelewa kwa maana bado haujafahamu maana nzima ya kifo! Kilichokufa hakina uhai na kilicho hai ni kile chenye sifa za uhai.. hizi ni kama zone na uhai ni sifa fulani zikipotea hiyo hali ndio kifo nothing utafanya you go no where!.
Kiumbe kikifika tunakizika then unaambiwa kimeenda mbinguni kwenye maisha mapya!.. huu upofu wa aina yake!.

Uhai ni uhai na kifo ni kifo labda Kama baadhi yenu hamuelewi maana ya kifo.
Kijana msiwe mnaandika mambo yaliyo wazidi uwezo na mkijua kabisa mkiombwa ushahidi hamna.

Sasa hii dibaji na kulalamika kuna toka wapi ? Wewe weka ushahidi kama unasema kweli.

Hii tabia inatakiwa ikome.
 
Ati lalamiko!..😂
Mkuu wapi nimelalamika..? Unafikiri hicho ni kitu ya kwamba nitakileta hapa au nikipige picha niweke hapa au unataka ukione moja kwa moja ndo uelewe!

"Hakuna maisha baada ya kifo"
Sidhani Kama unaelewa vilivyo sentensi hiyo! Kwako ni dibaji kwa fikra finyu.. uhai unathibitika hata kifo kinathibitika lkn maisha baada ya kifo hayathibitiki kwasababu hayapo.
Kama wewe unaona yanathibitika leta ushahidi wako hapa ikiwa Kama kweli hayo maisha yapo.. halafu tupime ipi dibaji na ngonjera.
 
Vingapi vinathibitishika na hatuvioni kijana wala hatuwezi kuvipiga picha wala kuvishika.

Inabidi mkue kiakili na kifikra pia,acheni huu utoto kisa mmeshiba makande mnakuja kutuandikia utumbo humu.
 
Sasa kuwa na maisha baada ya kifo ni kutishana au ndio poa mkuu,yaani wewe ulitaka ufe milele...?
Hahaa, Jamaa anataka aishi only once. Nadhani anaogopa zile theory za baathi ya watu wa Asia kuwa anaweza kufa akaja kuzaliwa tena kama nzi. Unazaliwa, unazurula alafu unakufa 😔
 
Vingapi vinathibitishika na hatuvioni kijana wala hatuwezi kuvipiga picha wala kuvishika.

Inabidi mkue kiakili na kifikra pia,acheni huu utoto kisa mmeshiba makande mnakuja kutuandikia utumbo humu.
Ha ha! Wewe uliekuwa kiakili leta hapa ushahidi maisha baada ya kifo..
 
Hahaa, Jamaa anataka aishi only once. Nadhani anaogopa zile theory za baathi ya watu wa Asia kuwa anaweza kufa akaja kuzaliwa tena kama nzi. Unazaliwa, unazurula alafu unakufa 😔
Mkuu mi siogopi hicho kitu na nafahamu nitaishi once ila nina nafasi ya kuendeleza uhai kwa kuzaliana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom