Kifo sio lazima niamini mimi, basi sio kwa vile jinsi tulivyokizoea broh

Uhakika Bro

JF-Expert Member
Mar 29, 2022
2,396
3,068
Ule msemo wa kwamba kila nafsi itakufa ni uzushi tu. Ni uzushi ambao umekubalika sana kiasi ambacho umeshakuwa kipande-cha-ukweli. Mbadala wa kipande-hicho-cha ukweli hata kama ni kweli kabisa lakini sasa ukizungumziwa basi watu watautazama kwa macho yenye walakini kana kwamba ni habari ya uongo.

Labda tuchunguze ni nini humaanishwa tunaposema kuhusu kufa. Kufa ni kama vile uuum….. eeeeh…. namaanisha ni vigumu sana kuongelea kuvunjikavunjika kabla hatujakuongelea kuunganika. Sasa basi tunarudi kwenye pointi moja inayoitwa UHAI.

Uhai una sifa ya kuunganika yaani mkusanyiko wa vipande vinavyoonekana kutokuwa na uhai na kuwa pamoja na kuwepo kwa umoja. Seli ya maisha ni ka rundo ka vitu vinavyosaidiana pamoja kwa faida ya wote. Mtindo huu huongeza ufanisi katika harakati za maisha/kuwepo.

Maisha bora zaidi hupatikana pale seli nyingi zaidi zinapoamua kushirikiana pamoja kwa faida. Ufanisi huongezeka maradufu kadri jumuiya za namna hii zinavyozidi kuwa kubwa, lakini zisizidi tu zikawa kubwa sana. Kwa hiyo, seli inaishi kwa ufanisi kidogo mkubwa kuliko mitochondria na ribosomu mojamoja pekeake. Ogani inaishi kiufanisi zaidi kidogo ya tishu mojamoja. Kiumbe mzima anaishi kwa ufanisi mkubwa kidogo ukilinganisha na mfumo mmojammoja pekeake.

Taifa linaishi katika ufanisi mkubwa ukilinganisha na vijiji. Uhai/maisha katika bando la jumuia kubwa na tata inayojiongoza vizuri ni yenye ufanisi zaidi kuliko visehemu vidogovidogo.

Sasa kwa kuwa tumeujua uhai asi tunaweza sasa kuianza safari yetu ya kukielewa kifo. Kifo ni kinyume na uhai. Pale muunganiko wa kile kikubwa unapokufa. Na huo ndio huwa mwanzo wa maisha ya visehemu vyake vidogovidogo. Pale nchi kubwa inapokufa basi vinchi vidogovidogo (vijiji) huzaliwa.

Kiumbe anapokufa basi seli, tishu, ogani na mifumo mbalimbali yenye uwezo wa kuishi yenyewe bila kutegemea yeye huanza kuishi/huzaliwa. Kifo kamili huwa ni pale ambapo hakuna namna kipande/kisehemu kinaweza kuishi pasipo kuwa kimeungana na vyote (kitu kizima).

Kwa sie waamini, tunaoamini katika Mungu basi kifo ni pale mtu anapoacha kuunganisha maisha yake na maisha ya Mungu.

Kwa wale wanaoamini katika ulimwengu kiujumla wake basi kifo kitatokea pale ambapo mtu ataacha kuwa sehemu ya ulimwengu au atakapoacha kusaidiwa na ulimwengu.

Hivyo basi kifo hadi hivi sasa tumekifahamu kama kitendo cha mwili kuto-jiunganisha na uhalisia wa ulimwengu hivyo unasambaratika (mwili).

Na hili jambo ndilo ninalosisitiza kwamba sio lazima bhanaa. Kila mara hii miili husambaratika kwa sababu imeshindwa kuunganika na mjumuiko mzima wa mambo yote.

Nini kitatokea endapo utaunganika badala yake?

Hahahahaaah, usiwe na haraka ndugu. Hata kama mtu ataunganika bado tu mwili itatakiwa kutupiliwa mbali lakini katika hali chanya zaidi. Kitakachotokea ni mageuzi makuu (uhamishaji wa taarifa) kutoka katika mwili mmoja kwenda katika ulimwengu uliopo potepote. Taarifa zilozokusanywa na mwili pamoja na akili zitachomekwa na kuunganishwa na kumbukumbu nzima ya ulimwengu.

Ili uweze kulielewa hili hebu chukulia mambo haya mawili. Mvunjiko wa kinyukilia na muunganiko wa kinyuklia. Hata kama yote haya hutokeza nishati kubwa sana na pia mageuzi ya mabadiliko ya umbile moja kwenda lingine (la maada) bado yapo tofauti. Moja (mbomoko/mvunjiko) huharibu wakati ambapo muunganiko hujenga. Muunganiko ni kujiunganisha ili kupata maisha tata zaidi na yenye ufanisi zaidi.

Hilo lina maana ipi kwa mwanadamu?

Kwa yule mwanadamu ambaye raha za mwili wake pamoja na roho yake zimeoana. Basi lile tukio la kukamilisha muungano wao kamilifu ndio aina ya ‘kifo’ ninayozungumzia hapa. Sehemu mbili zinaacha kuwepo kipekeyake peke ake na umoja mpya unazaliwa. Maisha mapya yanazaliwa, maisha yaliyoboreshwa.

Imewahi kurekodiwa katika hadithi za kibiblia pale manabii Eliya na Henoko walipopalizwa mbinguni. Aina hii ya ‘kifo’ hupelekea kutokea moto mkubwa sana ambao hujapata kuona. Nishati hiyo ni matokeo ya muunganiko wa taarifa binafsi za mwili na taarifa za roho za ulimwengu. Watu watakaoona watashuhudia moto kama wa nyota inayomweka. Yaani katika hivi punde tu maada zote zimeshapotea. KUPALIZWA rasmi ndio huko.

Naomba tuwekane sawa hapa; hakuna mwili wowote unaoendelea kuwepo milele. Lakini ni ile software tendanishi ya mwili, ile taarifa(wazo hai) na utambuzi wa huyo mtu ndiyo inayoweza na itakayookoka. Na huyo ndiye MTU! kama ulikuwa hujui ninekujuza

Takwa la kupalizwa ni jepesi na hapohapo ni gumu kulitimiza. Katika neno moja tunasema ni UMOJA. Umoja kati ya seli na seli. Umoja kati ya mwili na roho. Na mwishowe ni umoja kati ya roho na uhalisia wa ulimwengu. Umoja huu sio wa namna ya kulazimishana wala. Hapana.

Maana pale unapohangaika kuzitawalisha tamaa za mwili kwa mapaji ya kiroho utakachoweza kukipata ni umoja ulio nusunusu. Umoja kamili utapatikana pale ambapo matakwa ya mwili, kwa kuamua na hiyari basi yanahiyari kiroho na hivyo kiulimwengu mzima (ki-Mungu).

Kifo cha asili hutimiza jambo hili; kwa kuuharibu mwili basi mtu anapata somo la kwamba huu mwili sio wa lazima kuwa nao ili kuishi. Kama mtu anaweza kuielewa na kuitawala kweli hii tangu akiwa anaishi basi kunakuwa hakuna haja ya kufa tena. Yeye atajiunganisha mojakwamoja na kulipuka katika nishati itakayosambaa katika mazingira kama joto na mwanga.

Ikiwa hakuna maada (mwili) wakati huo wa kupalizwa basi ni mwanga tu utakaosambazwa. Hii ni kama wakati ule Yesu anapaa mbinguni.

Basi tunahitimisha kwamba, kifo hata sio lazima kabisa rafiki yangu, unaweza kupalizwa. – Mashauri

June 18, 2023


Imetolewa: ©Sahilinet
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom