Tusipotoshe, ukweli ni kwamba Samia Suluhu ni Rais wa Kikatiba na si Rais wa kuchaguliwa

Ni ujinga kunilazimisha eti Samia ni Rais wa kupigiwa kura!

Samia alikuwa msaidizi wa Hayati Magufuli ambaye ndiye aliyepigiwa kura za Watanzania kuwa Rais.

Lakini baada ya kifo cha Magufuli kikatiba makamu wake ndiye aliyepaswa kuwa mkuu wa Nchi. IELEWEKE,NI KWA MUJIBU WA KATIBA na si kwa MUJIBU WA WAPIGA KURA.

Kwa muktadha huo si sahihi kusema Samia ni Rais aliyepigiwa kura bali ni Rais ALIYEPO MADARAKANI KWA MUJIBU WA KATIBA na huo ndiyo ukweli.
Sawa kwa hiyo tukisema hapendwi na Wananchi tutakuwa sahihi
 
Kweli mkuu.. haiwezekani mtu anaamka asubuhi na chuki chuki zake anakuja kuandika ujinga hapa jukwaani. Dunia nzima wakiwepo mabeberu na hao wajinga waliomtuma kuandika huu uharo hapa wanajua fika kuwa Tanzania ina raisi, amiri jeshi na mkuu wa nchi mmoja tu, nae ni Samia Suluhu Hassani. Haijalishi uraisi wake kaupata kwa kura au vinginevyo, kikubwa katiba imezingatiwa na dunia inamtambua. Sasa kama haitaji kuongozwa na huyu raisi aende kwa Lisu wakatengeneze serikali yao huko belgium.
Maneno mazuri kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni jukumu letu kuelimishana ili tusifarakane, tulijenge taifa wetu kwa umoja!
Umoja ni nguvu,utengano ni udhaifu.Nimekutana na mtu kutokana Sudani,ameniambia Tanzania tuna Amani,wao hawana,tuna raslimali wao hawana,amenipa mfano wa zao la mkonge,jinsi linavyoingiza pesa,lakini wananchi wa Tanzania hatujiingizi huko kwenye mkonge.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umoja ni nguvu,utengano ni udhaifu.Nimekutana na mtu kutokana Sudani,ameniambia Tanzania tuna Amani,wao hawana,tuna raslimali wao hawana,amenipa mfano wa zao la mkonge,jinsi linavyoingiza pesa,lakini wananchi wa Tanzania hatujiingizi huko kwenye mkonge.

Sent using Jamii Forums mobile app

Nchi yetu ni tajiri sana kwa rasili mali Watu na hata rasimali Ardhi yakiwemo madini , maziwa na bahari. Sasa kwanini tukiwa na utajiri wote huo watu wetu bado ni masikini huku nchi zisikuwa na utajiri kama wetu Watu wao sio mafukara kama sisi? Siri iko kwenye kutokutumia rasilimali hizo sisi wenyewe kwa faida yetu na hili linatokana na sera mbovu!

Leo hii makampuni yanakuja kuchimba dhahabu na madini mengine mengi [ Watu wa Thailand wanachota Rubies tu huko I fakara] lakini tunapata hela kiduchu kwasababu hatudhibiti jinsi madini hayo yanavyochukuliwa na kuuzwa. Hivi karibuni wataanza kuchimba GRAPHITE huko Lindi , hebu niambie Serikali yetu ina stake kiasi gani kwenye hayo machimbo inayotuwezesha kuthibiti mapato yatakayotokana na uchimbaji huo?

Tunawaumiza wananchi wa hali ya chini kwa hela kidogo sana zinazotokana na tozo za miamala ya Simu. Fedha nyingi zingepatikana kwa kuthibiti uchukuaji wa madini yetu na hayo makampuni yanayochimba na wananchi wasingelalamika juu ya hizi tozo za miamala zinazoendelea kuwaumiza na kuathiri ukuaji wa uchumi ingawa Serikali inawahadaa wananchi kuwa imepunguza kwa 30%!
 
Ni ujinga kunilazimisha eti Samia ni Rais wa kupigiwa kura!

Samia alikuwa msaidizi wa Hayati Magufuli ambaye ndiye aliyepigiwa kura za Watanzania kuwa Rais.

Lakini baada ya kifo cha Magufuli kikatiba makamu wake ndiye aliyepaswa kuwa mkuu wa Nchi. IELEWEKE,NI KWA MUJIBU WA KATIBA na si kwa MUJIBU WA WAPIGA KURA.

Kwa muktadha huo si sahihi kusema Samia ni Rais aliyepigiwa kura bali ni Rais ALIYEPO MADARAKANI KWA MUJIBU WA KATIBA na huo ndiyo ukweli.
So what? Ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu. Period!
 
Ni ujinga kunilazimisha eti Samia ni Rais wa kupigiwa kura!

Samia alikuwa msaidizi wa Hayati Magufuli ambaye ndiye aliyepigiwa kura za Watanzania kuwa Rais.

Lakini baada ya kifo cha Magufuli kikatiba makamu wake ndiye aliyepaswa kuwa mkuu wa Nchi. IELEWEKE,NI KWA MUJIBU WA KATIBA na si kwa MUJIBU WA WAPIGA KURA.

Kwa muktadha huo si sahihi kusema Samia ni Rais aliyepigiwa kura bali ni Rais ALIYEPO MADARAKANI KWA MUJIBU WA KATIBA na huo ndiyo ukweli.
Kwa mujibu wa Katiba yetu iliyo bora Afrika, Rais wa JMT anapatikana kwa namna mbili.
i) Kwa kupigiwa kura kila baada ya miaka mitano Mf. Mwl. Nyererer, Mzee Mwnyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli

ii) Kwa kuapishwa Makamu wa Rais kuwa Rais wa JMT baada ya Rais kufariki akiwa madarakani. Mf. Mama Samia.

Anayebisha au kupinga hili nani?
 
Muendelee kukudanganya, kama kweli mnampenda mwambieni, muda wake wa bahati ukiisha aahache, wananchi wamemchoka, hana mvuto
 
Ni ujinga kunilazimisha eti Samia ni Rais wa kupigiwa kura!

Samia alikuwa msaidizi wa Hayati Magufuli ambaye ndiye aliyepigiwa kura za Watanzania kuwa Rais.

Lakini baada ya kifo cha Magufuli kikatiba makamu wake ndiye aliyepaswa kuwa mkuu wa Nchi. IELEWEKE,NI KWA MUJIBU WA KATIBA na si kwa MUJIBU WA WAPIGA KURA.

Kwa muktadha huo si sahihi kusema Samia ni Rais aliyepigiwa kura bali ni Rais ALIYEPO MADARAKANI KWA MUJIBU WA KATIBA na huo ndiyo ukweli.
Mzee umesahau kuwa katika uchaguzi wa Rais, tunachagua rais na MGOMBEA MWENZA. Maana yake MGOMBEA MWENZA naye anapigiwa kura za Rais ndo maana Rais akishinda na yeye anakuwa Rais Mtarajiwa moja kwa moja kama kuna lolote litakalotokea kwa Rais. Hivyo basi, Rais Samia ndiye Rais kwa sasa bila ubishi wowote na Rais aliyepigiwa kura wakati alipokuwa MGOMBEA MWENZA.
 
Umesahau kuwa waliomba kura wote pamoja tena juani. Kumbuka Samia ni mgombea mwenza wa JPM, ni sawa na wagombea wenza wote unaowafahamu wewe.

Akifa Mzee Biden leo hii Mama Senator Kamala ndio atakuwa rais wa USA. Unataka kusema Kamala hajautokea jasho urais kisa Biden ndiye alikuwa mgombea mkuu?

Punguzeni kuishi na hasira mioyoni. Mama Samia ndio rais wako mpaka 2025.
 
Mzee umesahau kuwa katika uchaguzi wa Rais, tunachagua rais na MGOMBEA MWENZA. Maana yake MGOMBEA MWENZA naye anapigiwa kura za Rais ndo maana Rais akishinda na yeye anakuwa Rais Mtarajiwa moja kwa moja kama kuna lolote litakalotokea kwa Rais. Hivyo basi, Rais Samia ndiye Rais kwa sasa bila ubishi wowote na Rais aliyepigiwa kura wakati alipokuwa MGOMBEA MWENZA.
Inamuwia ngumu kuukubali huo ukweli, ukizingatia mfumo dume umetawala 'kichwa' chake.
 
Rais gani sio wa kikatiba? Hata Nyerere alikuwa wa kikatiba. Au hujui katiba maana yake nini,Kura za rais zinaweza kupungua au kuongezeka kwa sababu ya mgombea mwenza(Samia) najua hilo hujui.
 
Mbon kwenye vote kuna picha ya watu 2 na unawachagua wote emu nyie watu wa bara turieni dawa iwaingie
 
Kiufupi tukubali tu kwamba ni rais wa JMT. Kwa wanaosema kuwa kwamba kura za mhombea ndo kura za mgombea mwenza tuwaze hivi, Angewekwa Samia kama Mgombea urais na Magu mgombea mwenza matokeo yangekua yale yale?

Kiukweli na kiuhalisia watu huwa wanaangalia mgombea Urais ni nani. Mgombea mwenza hatazamwi sana. Na hata wakati mwenda zake akiwepo, alikua anasikika sana Magu na Majaliwa. Samia alikua amefichwa. Huwa wanawekwa kama boshen tu.

Angalia kipindi cha Mh. Kikwete na Bilal. Binafsi sikumsikia sana Bilal kama nilivyokua namsikia Pinda na Lowassa.

Makamu pia akimaliza muda wake humuoni sana kama anavyoonekana Rais. Shein alionekana tena kwa sababu ya Urais wa Z'bar.

Naunga mkono hoja. Huu ni Urais wa katiba. Samia aliwekwa kubalance Muungano na kutafta kura za jinsia ya pili. Afu ikumbukwe alikiri BBC
 
Ni ujinga kunilazimisha eti Samia ni Rais wa kupigiwa kura!

Samia alikuwa msaidizi wa Hayati Magufuli ambaye ndiye aliyepigiwa kura za Watanzania kuwa Rais.

Lakini baada ya kifo cha Magufuli kikatiba makamu wake ndiye aliyepaswa kuwa mkuu wa Nchi. IELEWEKE,NI KWA MUJIBU WA KATIBA na si kwa MUJIBU WA WAPIGA KURA.

Kwa muktadha huo si sahihi kusema Samia ni Rais aliyepigiwa kura bali ni Rais ALIYEPO MADARAKANI KWA MUJIBU WA KATIBA na huo ndiyo ukweli.
Watu wa mfu mna matatizo sana, kwani nani amesema alichaguliwa? BTW kwani alichaguliwa na akiingia kwa kurithi so Katiba imeruhusu njia zote sasa huoni bado hata anayechaguliwa ni Rais wa kikatiba?

Whatever the case as long Katiba imetamka na kuruhusu Rais aingie kwa njia fulani basi inakuwa kikatiba tu whether achaguliwe au vyovyote. So hata huyo aliuechaguliwa Hana tofauti na huyu wa sasa acha kutoka povu jipangeni upya tu.
 
Back
Top Bottom