Tusipotoshane, ajira ina nafuu na uhakika zaidi kuliko kujiajiri

My few cents on the drama

Guys it is tough out there

People are suffering out there

People are making money out there

Kuajiriwa na kujiajiri ni relative conditions
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Hakuna unafuu ila tu uhakika kwani kuna mkataba. Kujiajiri inalipa ila ni kuomba uwe mzima ili upambane. Wewe chunga tu kwa siku unaingiza ngapi na aliyeajiriwa apige mahesabu kwa siku anaingiza ngapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi wengi wetu ni wavivu ndio maana tunataka kuajiriwa...mfano nafasi yangu angekuwa mchina, angekuwa mbali sana...naingia saa mbili, natoka saa kumi..ninapokaa kuna abiria kibao, badala ya kununua bajaji niwe napig angalau masaa matatu kwa siku...mimi nawaza gari tu hapa...akili zetu tunazijua wenyewe
 
Sio uvivu tu pia na kuonea aibu baadhi ya kazi. Mfano Kama huo wa bajaji au hata boda boda ulioutoa utakuta mtu anaanza kujiuliza, "yaani Mimi na elimu yangu/ualimu wangu / udaktari wangu nianze kupakia abiria!?

Wengi tuna ule utamaduni wa kujiuliza "watanionaje? Watanichukuliaje"? Hala hatupigi hatua
 
Hapo umenena ...ni kweli kabisa itabidi nibadili mtizamo wangu
 
Kujiajiri vs kuajiriwa; Bora kujiajiri! Sema tu kujiajiri kunahitaji maandalizi ya kutosha. Ukikurupuka, hakika utaisoma namba.
 
Changamoto za ujasiriamali katika Afrika zimesababisha ajira ionekane kuwa na usalama wa kipato zaidi ya njia nyinginezo, kwa sababu ya kuwa na uhakika wa kipato kila baada ya muda mfupi.

Kujitegemea ni mbinu mbadala na zenye tija pale mtu anapopata mpenyo. Kwa Afrika hasa Tanzania, waliopata mpenyo ni mmoja kati ya kumi. Wengi wanaishia kulipa Kodi, kula na kukimbizana na madeni, kwa sababu, mfumo wa uchumi si rafiki kwa wasio na ajira.

Taasisi za fedha zimeelekeza nguvu zao kwa wenye ajira kwa sababu ya uhakika wa marejesho ya mikopo. Wajasiriamali wanakutana na hofu ya taasisi za fedha kushindwa kurejesha mikopo, hivyo kuwekewa masharti magumu ambayo ni wachache sana wanaoweza kukidhi vigezo hivyo.

Kwa maana hiyo, pamoja na kuwa ajira si jambo la kujivunia sana, kwa kuwa huwezi kupata mtaji nje ya kukopa, Bado katika mazingira ya sasa, ajira imekuwa mhimili mkubwa na wa uhakika kuendesha maisha ya kila siku.
 
Back
Top Bottom