Tanzania ukiajiriwa Serikalini ni raha kuzidi kujiajiri kwa kipato sawa na mshahara wa aliyeajiriwa

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Ikiwa alieajiriwa Serikalini na aliejiajiri wote wanaingiza kipato sawa kila mwezi

1. Aliejiajiri anaondoka kwake asubuhi kurudi hadi usiku, alieajiriwa Serikalini anaondoka asubuhi anamaliza kazi zake jioni na bado huko ofisini kuna muda anapata kufanya mambo yake.

2. Aliejiajiri anaweza asizijue weekend lakini alieajiriwa Serikalini anapumzika Jumamosi na Jumapili.

3. Aliajiajiri hana sikukuu za kiserikali, alieajiriwa Serikalini haendi kazini idi (hata kama ni mkristo), mwaka mpya, Mei mosi, sabasaba, siku ya Nyeyere, siku ya uhuru, mapinduzi, nanenane, idi, pasaka, n.k

4. Aliejiajiri akiumwa inabidi ajikaze aende tu lasivyo kipato kinaweza kutikisika, alieajiriwa Serikalini akiumwa anatoa notisi.

5. Aliejiajiri hana likizo, muajiriwa ana likizo siku 30 kila mwaka.

6. Aliejiajiri anaweza kufilisika endapo duka likiungua, akiumwa kwa muda mrefu, akiibiwa, n.k. alieajiriwa Serikalini nafasi yake na mshahara wake ni uhakika

7. Aliyeajiriwa Serikalini ni rahisi kukusanya mtaji, mkopo anapata kwa masharti nafuu sana na kwa haraka sambaamba na kudunduliza mshahara

8. Alieajiajiriwa na Serikali ana muda mwingi wa kuwa na familia yake kuzidi aliejiajiri. ikifika jioni, weekend, sikukuu za serikali, likizo, n.k. ana muda wa kutosha wa kuwa na familia yake

9. Alieajiriwa Serikalini anaweza kuwa ma biashara zake za kumuongezea kipato, hizi biashara zinaweza kumtunza baada ya kustaafu na watoto wake kuzirithi, Mifano ni kina Robert Kiyosaki mwenye kitabu cha Rich Dad Poor dad, Vunja Bei, Marehemu cpa Mengi, n.k. walianza kwa kukusanya mitaji wakiwa wameajiriwa.

Mwisho niseme Kujiajiri watu wanameki bingo lakini ni wachache, wengi wanaanguka na wengine wapo pale pale miaka nenda rudi. wachache wenye wenye roho ngumu, ubunifu, juhudi, kujibana, uvumilivu na connections ndio wanatoboa.
 
Somebody had to say this!! Mimi nimefanya sana biashara, nimetoka sana jasho la hustle za hapa na pale ila asikudanganye mtu Serikalini ni Serikalini tu!!!! Kipindi cha corona biashara ziliyumba, kwenye private sectors baadhi waliondolewa. Ila Serikalini mserereko uliendelea.

Na nyie mnaosema kama watoto wao watarithi kazi, kwani ukizaa mtoto una uhakika gani atapenda kitu unachokifanya? Una uhakika gani atakuja kupenda hiyo biashara yako ya mahindi.

Rai, tafuta kazi Serikalini, establish vitega uchumi au biashara ambazo sio lazima uwepo 24/7.. unazichanga unawanunulia ardhi wakija kukua hao wanao wana cha kurithi. Na wenyewe unawajengea misingi ya kujitegemea kimaisha hata kama umewaandalia chochote kitu incase ukidondoka. Full stop.

Hii mada haihusu wale wanaume wenye watoto sita ndani ya ndoa wanne nje. Nyie mkifa familia zenu zinatamanigi ziwachape makofi ngedere
 
Na alieajiriwa anaweza kujiongeza akajiajiri pia.. aliyejiajiiri akijiongeza ataajiri watu wa kuwatoa ngeu. Genuine aliyejiajiri anaweza kukua na kuwa mkubwa zaidi... aliyeajiriwa kugrow ni ngumu mnoooo. wengi wanaojaribu kujiajiri baada ya kutoka ajirani hawajuti na hawalalamiki kujiondoa huko.
 
Aliyejiajiri anaweza endeleza mradi wake vizuri ndani ya miaka 5 akawa anaingiza zaidi ya m10 kwa mwezi, wakati huo wewe uko palepale na kamshahara kako, pia aliyejiajiri hata akifa familia yake inaweza kua na uhakika zaidi endapo akifundisha watoto wake namna ya kufanya biashara.
.
NB: KUJIAJIRI SI KILA MTU ANAWEZA
 
Back
Top Bottom