sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,014
Kwanza kabisa naomba tuyaelewe haya makundi matatu
KUNDI LA KWANZA - ALIEJIAJIRI / SELF EMPLOYED
Huyu biashara inamuhitaji ili iende, yeye ndie ngvu kazi kuu ya kuieiendesha biashara kwa bidii yake na hata akiajiri bado yeye inabidi ahusike kwa level ya juu sana ili biashara iende, Wengi wao inabidi aende dukani kila siku alfajiri mpaka usiku, kutembeza bidhaa mitaani (machinga), fundi cherehani, n.k kundi hili mara nyingi asipoenda ofisini hakuna pesa inaingia hapo, akiumwa hakuna malipo, n.k.
Kundi hili kusema kweli hakuna uhuru, mtu ukiwa kundi hili usije kujichanganya hata siku moja kujifananisha na watu wa kundi la pili, wenzetu wengi wa nchi zilizoendelea kwenye maarifa, mtu akiingia hili kundi anasota miaka hata mitano ili aingie kundi la pili, cha ajabu huku Tanzania ni kama vile watu wa hili kundi wamridhika kuwepo hili kundi ama hawanana mikakati ya kuingia kundi la pili, wengi nimewajua tangu nipo shule ya msingi bado wapo pale pale, nahisi ni kukosa maarifa kwa kudhani kwamba wapo kundi moja na kundi la pili.
KUNDI LA PILI - MMILIKI WA BIASHARA / BUSINESS OWNER
Hawa sifa yao kuu ni kwamba wameajiri watu wengine wawasaidie kuzalisha pesa, hawafanyi kazi ili wapate pesa kama kundi la kwanza na la tatu, pesa ndio inawafanyia kazi ..Yeye anaweza akanunua kiwanja akapageuza kuwa car wash, vijana wanakuja kuosha magari, ikifika jioni anakuja kuchukua mgao wake. Anaweza akawa ni Mo au Bakhresa ikifika asubuhi watu wanawahi kwenda kwenye viwanda vyao kufanya kazi ili kuwatengenezea pesa na wao kulipwa mishahara,
Hata kwa upande wa wasanii, Diamond yupo kundi la pili, kaajiri mameneja, wasanii, n.k ana magari ya kufahari kama rolls royce toleo la mwaka huu, escallade toleo la mwaka jana, v8 kama ya wabunge, n.k , wasanii wengi wapo kundi la kwanza wanatembelea toyota za mwaka 2014 zilizotumika mno.
KUNDI LA TATU- ALIEAJIRIWA (EMPLOYED)
Hili kundi lina nafuu kuzidi kundi la kwanza hasa wakiwa wanapata kipato sawa
Huwa nashangaa sana mtu wa kundi la kwanza anaeshinda dukani masaa zaidi ya 12, anapigwa na jua mchana akitembeza bidhaa, n.k na faida yenyewe haizidi hata elf 30 kwa siku, Sijui ni wapi anautoa ujasiri wa kumdharau mtu wa kundi la tatu kwa kauli kama "ajira ni utumwa" hapo ikumbukwe yeye na mwenzake wanaingiza kipato sawa lakini mwenzake anafanyia kazi zake ofisini kwenye kiyoyozi, umeme ukikatika generator inawashwa, anafana kazi mpaka saa 10 tu jioni, ana siku siku 150 kati ya 365 za kupumzika kila mwaka, akiumwa bado anapata analipwa, kuna posho za ziada, anaweza kufungua biashara na kuajiri wasimamizi, n.k
Kauli nyingine ya kijinga ya kujifariji ni kuuliza swali "nitajie tajiri yeyote mkubwa nchini alietajirika kupitia mshahara?" Hapa mtu anauliza hili swali kwa maksudi kabisa ili kujifariji huku akijidanganya kwamba yupo kundi moja na kina bakhresa waliopo kundi la pili, anasahau kabisa kwamba watu wa kundi la pili ni Business owners (wamiliki wa biashara) wanaoajiri watu wawatafutie pesa, hata wakiuchapa usingizi mpaka saa nne pesa inaingia tu.
Kuponda ajira ni utumwa kwa mtu aliejiajiri ni sawa na "sizitaki mbichi hizi", nimeshushudia ajira zikitangazwa, hao waliojiajiri wanazishambulia sio mchezo, mtu anafunga duka lake kapata safari ya kwenda dar kufanya interview,
Kuna vijana wadogo wengi tu wameajiriwa, wanakunja mshahara zaidi ya milioni 2 kila mwezi na wamepiga hatua ya ziada kufungua biashara zao za kuajiri wenzao (kuwa business owners), kujenga wakiwa bado vijana wadogo, n.k Niambie vijana wangapi wa kundi la kwanza wanakuwa wamefika hizo level?
Jiulize kwanini hata wazazi wengi ambao wapo kundi la kwanza wanapigana kufa kupoma kuwapeleka watoto kusoma na kuwaambia wasome ili wapate ajira? Kwanini wasiwaambie wasome ili wawe kama wao?

- Kazi anayoifanya haifanyi peke yake huwa wanasaidiana na wengine kwa hio mzigo haujamuelemea
- Mshahara wake atalipwa hata akiumwa ama kuwa na sababu maalum ya kutofika kazini
- anaweza kuingia kazini saa 2 na kutoka saa 10 / 11 jioni na kupata muda wa kukaa na watoto kama mzazi.
- Bima ya afya
- Mikopo kupatikana kirahisi
- Anapumzika siku za weekend zipatazo 104, sherehe za kidini na sherehe za kiserikali siku 20, kkizo ya mwezi siku 30, n.k
- Kipatoo ambacho ni mshahara atakipata kwa uhakika bila longo longo, pia kuna posho
- Anapata status kwenye jamii mfano baba flani ni mwanajeshi, injinia, muhasibu, dokta, hakimu, n.k. ukipata tatizo flani anaweza kutumia nafasi yake kukusaidia.
- Anaweza kuingia kundi la pili bila kupitia taabu za kundi la kwanza maana tayari ana mshahara na anapata mkopo bila longo longo unaoweza kuwa mtaji na ukagharamia mfanyakazi wa kumtengenezea fedha