Sasa wewe ndugu nini unachopinga au kuunga mkono!! Je unaunga mkono kila DINI itangaze malalamiko yake kupitia Vyombo vyake vya habari? Ndugu yangu umetoa mifano yote hiyo kwamba kulikuwa hakuna "upanga"Usipotoshe ukweli kwa dai lako la uongo kuwa Uislamu ulienezwa kwa upanga! haya nakuuliza, Uislamu ulipoingia huku kwetu miaka 1000 kabla ya ukristo kuja ni upanga gani huo uliotumika mpaka babu zetu wakasilimu?
Maeneo ya Machame, Usangi, Ugweno, Moshi mjini, Bukoba, Musoma nk, kuna Waislamu pia sasa upanga uliotumika kuwasilimisha umeuhifadhi ktk MUSEUM yako?
2) Indonesia ni nchi yenye idadi kubwa sana ya Waislamu duniani kote, sasa uislamu ulipoingia huko ni upanga upi huo uliotumika?
India, Pakistani, Afganistani, Kosovo, Bosnia, mackedonia, Uzbekistan, Urusi, Chechenia, USA na nchi nyingi duniani wanakoishi waislamu ni upanga gani huo uliotumika?
Labda Ukristo ndio ulioenezwa kwa mtutu wa bunduki ndio maana Wazee wetu akina KINJEKITILE walikataa kudanganywa na Wazungu waliokuja kama Wamisionari kumbe lengo lau ni kuwabatiza na kuwatala!
Usituletee propaganda chafu zilizopitwa na wakati tafuta lingine la kuongea lakini sio *****!
Lazima ilete tabu, as unajua Tanzania generally wachache sana waliolemika be wakristo or waislam, na sio wengi wanaoweza kupambanua kua hao ni masheikh uchwara, ni hatari sana hili jambo na halitakiwi kuwa ignored hata kidogoHao ni masheikh uchwara wackupe taabu,cc waislaum tulioelimika hatuwezi kudanganywa na hao wapuuzi
Mtu mjinga utamjua kwa matendo yake. Sasa mtu anapata urais Misri, yeye anafurahia kwa maslahi gani? Basi ukimuuliza utasikia eti kwa sababu ni muislamu, sasa kama ni muislamu ni mjomba wako..?? Nafikiri tatizo linalo wa-cost hawa jamaa zetu ni ile hali ya kutotilia maanani kigezo elimu kama dodoso muhimu katika kupata mashekhe viongozi.Jana Shekhe Issa alifurahia sana Mursi kutangazwa kuwa rais wa Misri kwa kuwa ni kiongozi wa Muslim Brotherhood. Kwa udini alionao shekhe huyu anatamani leo hii nchi hii ijitangaze kuwa ya kiislamu
Miongoni mwa wa islam wenye uelewa na wewe umo.endelea kuwaelimisha wenzako.mimi ni muislam lakini sikubaliani na yalnayosemwa na Waislam wenzangu JAMANI WAISLAM WENZANGU TUBADILIKE YUACHE UVIVU NA MAJUNGU
Tatizo ss tunajifanya kuwa na Msimamo usiokiwa na Faida jamani mm mbona ni muislam lkn nimesoma mpaka university na form four Div 1 form six DIv 2 university First class Mbona Sikufellishwa na Mtu tatizo letu wakati wakristu wanajenga Mashule na Mahospital ss tumelala Msikitikini Mchana kweupe
Ndugu zangu Majungu hayasaidii tubadilike
umesahau na kigamboni kwa wapemba....Kama kuna watanzania wanaosikiliza hiyo redio basi hawazidi mia tano. Wengi wao wapo tandale, manzese, tandika, temeke, gongolamboto na mbagala.
Wadau, jana katika kubadilisha station ya radio yangu nilikutana na mjadala uliokuwa ukiendeshwa redio imani, hii ni redio ya kiislamu iliyoko mjini Morogoro. Ingawa si kawaida yangu kuisikiliza lakini nilishawishika kuwasikiliza kutokana na uzito wa mambo yaliyokuwa yakijadiliwa.
Mjadala ulihusu tamko walilotoa kuhusu maaskofu, walivilaumu vyombo vya habari magazeti particularly mwananchi na magazeti mengine kama nipashe, Tz Daima etc kwamba yamepotosha tamko lao pamoja na kuwa waliwapa tamko hilo kimaandishi. Nilijiuliza inakuwaje magazeti yote yanakosea kitu kilekile.
Kilichonisikitisha katika mjadala huo ni uchochezi na upotoshaji wanaoueneza hawa masheikh kwa sababu wanazojua wao. Kwa mfano walisema nchi inaendeshwa kwa mfumo wa kikiristu toka enzi za Nyerere, moja ya madai yao ni kwamba waislaumu walikuwa wakifelishwa makusudi shuleni ili wasisome, bila shaka haya ni madai makubwa sana.
Mambo mengine ni kwamba ili kudhibitisha kwamba nchi inaendeshwa kikristo ni kwa nini wakristo wana university na hospitali nyingi kuliko serikali, madai mengine ni kwamba kwa nini hospitali za kikristo zilizotaifishwa na serikali zilirudishwa, bila shaka katika hili ni kwamba serikali ilishindwa kuziendesha, lakini kwa sababu wanazojua wao waliishia kulaumu mfumo wa utawala wa kikristo. Katika hili wao walikiri kwamba hakurudishiwa kitu kwa kuwa hawakunyanganywa kitu!
Baada ya kumaliza majadiliano waliruhusu wasikilizaji kutuma sms na kupiga simu studio, wengi wa wachangiaji waliwashukuru masheikh kwa hatua yao lakini pia kuna waliosema watajichukulia sheria mkononi ili kuwaadhibu waandishi, na wengine walitaka itangazwe jihad dhidi yao.
Nilivyoona mimi hakuna shabaha nyingine zaidi ya kuleta chuki miongoni mwa dini jambo ambalo si kawaida yetu watz.
Ingawa najua kwamba redio hii haina wasikilizaji wengi lakini mijadala ya uchochezi namna ile haitakiwi kupita bila kukemewa. Katika mauaji ya Rwanda redio zilitumika sana kuchochea chuki baina ya watu, hatutakiwi kufika huko, nadhani ni wakati muafaka kwa intelijensia ya polisi kufanya kazi sasa ili kuzuia maafa yanayoweza kutokana na uchochezi wa redio imani
Wana JF naomba kuwakilisha
Mdau, binafsi nakupongeza kwa kuliona hilo na kuona kwamba ipo haja ya kutoa angalizo kwa kile ulichokisikia kupitia redio hiyo inayomilikiwa na taasisi ya dini ya Kiislam.
Kwangu mimi, cha msingi ninachokiona kwenye mada yako ni kuhusu uchochezi wa kidini unaofanywa na Redio hiyo na maafa yanayoweza kulikumba taifa letu kama hatua za haraka hazitachuliwa kudhibiti hali hiyo. Mimi binafsi sina tatizo na hoja yako. Kimsingi ni angalizo linalopaswa kuungwa mkono na kila mpenda amani. Hata hviyo, ninachotaka kuongeza hapa ni kwamba, hali ya mustakabali wa kidini katika Tanzania kwa sasa ni tete. Na hili halina ubishi hata kidogo, labda iwe kwa mtu mwenye hulka ya kubishia kila jambo ndiye pekee anayeweza kupingana na ukweli huu.
Hali tuliyo nayo sasa hapa nchini haishirii dalili njema hata kidogo mbele ya safari. Zinahitajika hatua za maksudi kabisa katika kukabiliana na hali hii kabla bomu halijalipuka. Ni vema watanzania tukatambua kwamba machafuko yenye sura kama hizi za kidini mahali popote yalipopata kutokea duniani, hayakuja kama mvua au kwa bahati mbaya, la hasha!. Machafuko yalianza kama masihala kwa njia kama hizi hizi za chochoko, malumbano,na uchochezi wa chini kwa chni kama tunavyoanzashudia hapa kwetu Tanzania.
Binafsi sipendi kuhukumu kwamba ni dini gani hasa ndio inayoonesha dalili za kutaka kutupeleka kwenye machafuko ya kidini ambayo ni machafuko mabaya kupita machafuko mengine yoyote katika dunia hii. Nasita kufanya hivyo kwa sababu imani yangu inanizuia kukuhukumu na kusisitiza zaidi kuchunguza boriti ndani ya jicho langu kabla ya kutoa kibanzi katika mboni ya jicho la mwenzangu. Hata hivyo, natambua dhahiri shahri kwamba mustakabli wa hali ya kidini hapa nchini imekuwa tete tangu mchakato wa uchaguzi Mkuu wa mwaka jana. Hivyo basi, ni wajibu wa kila mtanzania mwenye dini na asiye na dini kuliona hilo na kuchukua hatua kwa nafasi yake ili kuzuia dalili mbaya zinajitokeza katika taifa letu.
Na mwisho ninapendekeza kwamba, kama ilivyo hitaji la watanzania kuwa na Katiba Mpya, basi halikadhilika iwe hivyo hivyo katika jambo la kidini. Sio vibaya tukawa na mjadala wa kitaifa kuhusu hatma ya mivutano ya kidini iliyoanza kujitokeza hapa nchini. Na kwa njia hiyo pekee ndipo tutaweza kutoa fursa kwa kila upande utoe dukuduku lake na kisha kufikia muafaka wa pamoja. Lakini, tukiendelea kupuuza, kukejeliana,kutukanana na kushutumiana bila kuchukua hatua zozote haitatusaidia. Tukumbuke kwamba panapofuka moshi lazima pana moto!!
Mungu ibariki Tanzania na watu wake!!!
Nasikia kipindi awamu ya Mwinyi waligeuza open space nyingi kujenga misikiti. Mfano ni eneo la Sinza...
Kama wanahisi wanafelishwa, watafute waislam kama mia hivi ambao wanadai wamefelishwa, alafu script zao zipitiwe na tume maalumu tuone kama kunaukweli! Si kupiga kelele tu bila kuwa na ushahidi
Hi dini asili yake ni fujo duniani kote, ndo maana hata kwenye ncgi za Kiaarabu pamoja na kuwa more than 95% ni waislam bado wataandamana wakidai wanaonewa, wao huwa wana allerge na amani so tusiwashangae.
Mkuu Barubaru, naomba link ya redio hii kwenye mtandao ili na mimi nifaidi uhondo huo.Ahali yangu unatakiwa ujuwe kuwa huo ndio UANDISHI MAHIRI kwani baada ya mashaikh kama ulivyodai kumaliza kutoa mada yao walitoa nafasi kwa watu kuchangia. WEWE NDIO ILIKUWA NAFASI yako adhimu sana kuchangia kwa kukanusha na kuweka data au hoja zako kupingana na za hao Mashaikh. Kwani kwa kukataa kwako kuchangia umelinyima taifa lako na wasikilizaji wengi wa Radio hiyo haki yao ya msingi ya uhuru wa kujieleza na kutoa maoni na vile vile kupata habari sahihi.
Lakin kwa hitimisho lako kuwa una imani kuwa Radio hiyo ina wasikilizaji wachache nafikiri sio SAHIHI. Kwani kwa kulijua hilo ungepata nafasi ya HARAMBEE walioitisha ya uanzishwaji wa IMAAN TV ungegundua mengi sana.
Kwa Taarifa RADIO Hiyo sasa inapatikana mtandaoni na kila mtu duniyyani anaweza kuisikiliza 24Hrs lakin pia wanaanzisha TV IMAAN na soon itakuja juu.
Kwa dondoo kidogo Taarifa waliyoitoa kwenye vyombo va habari ambavyo vingi hawajaiweka ipitie kwenye gzeti la KISIWA au AN Nuur. yote yapo kwenye mtandao.
Kumbuka kuwa uandishi wa habari wa kweli ni ule unaotoa nafasi ka pande zote kujieleza au kutoa maoni yao kiusawa na kuleta changamoto kwa jamii ili kupata habari sahihi. Kuficha habari ni dhambi kubwa na ufisadi kuliko ule wa EPA.