Tusiotumia pombe njoni tupeane pole

WENGI walitumbukizwa kwenye ulevi ama na marafiki zao au jamaa zao.Na walikunywa pombe kwa kutaka sifa waonekane nao wapo kwenye ulevi,mwisho walijikuta wamezoea kunywa na wanakuwa na hamu ya kunywa kila siku kuacha inakuwa shughuli pevu
 
Simba akiingia kichaka cha mbwa mwitu haponi,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asilimia kubwa ya watu ninaowafahamu ni wanywaji wa pombe,na nmeishi na wanywaji miaka mingi,babu yangu alikuwa testa wa kijiji,lakini sjawahi hata kuwa na mawazo ya kutaka kuja kujaribu,na sina mpango huo,Natumia mmea tu,poleni nyie mnaotumia kimea.
 


Sent using Jamii Forums mobile app
 
[
NB: sinywi pombe kwa sababu sina sababu ya kunywa pombe .

[emoji1] [emoji1] [emoji106] [emoji106]
 
kila mtu na starehe yake
anaetumia jasho lake
na hayo ndio mapenzi yake..

[emoji481] [emoji481] [emoji481] [emoji481]
 
Pole,nilipata taabu sana kuacha pombe,nilivyotoka kuacha nilijihisi mnyonge sana maana marafiki zangu ilikuwa ni kama wimbo kila nikiwa nao wananipondea,kuna mitaa nilikuwa napita nikaacha kabisa nikihisi kila mtu ananisema mimi,lakini nilizoea ikafika mahali nikaanza kuwaona wanaokunywa pombe ni watu wa hovyo tu,kwani kuna baa nilikuwa naingia mpaka najiuliza hivi ilikuwa ni akili yangu kweli...

Sony Z3
 
Unajua usipotumia pombe unaonekana mshamba hususani ukiwa na kampani ya wanywaji,imeshanitokea sana napotoka out na marafiki tukiwa bar au club na wao wakaagiza Bia,wanakuona wa ajbu sana kutotumia pombe.kuna mmoja aliniambia inabidi nitumie dompo na sio soda.Hahahahaha
 
Kwanza huwa nawashangaa walevi huwa wanapata raha gani wakati mijipnmbe yenyewe michungu haswa.
Huwezi jua uzuri wa ngoma mpaka utakapoingia kuicheza.


ONYO: kunywa kupita kiasi ni hatari kwa afya yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…