Tusimdhihaki Mungu kiasi hiki

Tusimdhihaki Mungu kiasi hiki

Mtoa mada ameweka maandishi ya kutukumbusha nashangaa watu wanaompinga eti ooh Mungu ni wa huruma mara usihukumu..... Hivi kuhukumu maana yake nini?
Kama hali ndio hii bas hata kanisani hatutakiwi kwenda maana ni nani aliye msafi kama Mungu? Mwenye ujasiri wa kusimama na kukemea uovu. Ndio Mungu ni wa huruma lakini ni huyohuyo ndo amesema kila alitajaye jina lake na auache uovu..... Tena anasema 'lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia,mtu aliye mnyonge,mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu'. Tu wenye dhambi.......lakini tusing'ang'anie kutenda uovu kwa sababu Mungu anasamehe.
 
Mungu huwa anakasirika?Huyu Mungu anayekasirika ndo yuleyule mwenye Upendo usio na mipaka ambaye ametuamuru tuwasamehe wenzetu saba mara sabini kwa siku?Kwaiyo Mungu huyu ana akili,hisia na mwili kama sisi binadamu?
We naye unachanganya mada. Kwani kukasirika kuna uhusiano gani na kuwa na mwili kama binadamu?? Ni sayansi gani inayosema ili uwe na hasira ni lazima uwe na mwili?

Pili ni kwa nini unadhani ukiwa na upendo huwezi kukasirika?
 
Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi?.....Warumi 6 kaendelee

Duh... Twin uko deep!

Haya endelea na huu mstari pia...

Warumi 6:12
Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake;
 
Hivi Babu zetu kabla ya kuletewa dini za magharibi na Uarabuni walikuwa wanaabudu Mungu yupi? Na kwanini sisi ndo tuletewe dini kwanini sisi tusingepeleka kwao?
Japo naabudu katika dini niliyozaliwa nikaikuta lakini kuna vitu huwa vinanitatza sana.
Anayeelewa hapa anisaidie.

Watu wanagombana, sijui mungu wangu ni Mulungu, wengine Allah, wengine mara oh Allah sio Mungu, n.k. Museveni aliwahi kuwalaumu wazungu kuhusu kubembeleza ushoga Afrika. Akawa anawashangaa watu wa mataifa ya mashariki na magharibi ya dunia kutuambia kipi ni halali na kipi ni haramu sisi waafrika wakati sisi tuna haramu zetu ambazo hatujazipeleka mashariki wala magharibi ya dunia na kuwabembeleza au kulazimisha wazikubali. Mambo ya unaabudu Mungu yupi ni swala la kiimani tu kwa hiyo mi nakushauri kama kuna Mungu ambaye unaona ukimuomba anakusaidia we muabudu huyohuyo. Mawazo yako ya kina (subconscious mind) yameisha muweka kuwa huyo ndio mpango mzima labda kama unaweza kufuta na kuanza kuamini vinginevyo upya na nafsi yako isikusute. Ila usiamini katika miujiza. Kuna watu kama Dynamo na Chris Angel, n.k wanapaa, kutembea juu ya maji, n.k. Hiyo ni elimu tu na yeyote anaweza kuwa nayo akakudanganya kuwa mungu wake ndio 'habari ya mjini'. Jiamini kwanza wewe kama wewe halafu uchague njia sahihi kwa mujibu wako wewe mwenyewe. Mi naona sisi waafrika hatuna hulka ya kupeleka imani zetu kwa watu wengine. Binafsi naziheshimu sana ijapokuwa wengine wanafikiri ni uchawi. Katika Hinduism, 90% ya rituals zao ni zilezile ambazo babu zetu walizifanya ila bongo wanaita uchawi. Walio ishi India kwa muda mrefu au waliofanya kazi kwenye ofisi za wahindi kwa muda mrefu wanalijua hili. Ukiondoa mambo ya kuabudu wanyama kama moja ya miungu mambo mengine ni yaleyale.
 
Mtoa mada ameweka maandishi ya kutukumbusha nashangaa watu wanaompinga eti ooh Mungu ni wa huruma mara usihukumu..... Hivi kuhukumu maana yake nini?
Kama hali ndio hii bas hata kanisani hatutakiwi kwenda maana ni nani aliye msafi kama Mungu? Mwenye ujasiri wa kusimama na kukemea uovu. Ndio Mungu ni wa huruma lakini ni huyohuyo ndo amesema kila alitajaye jina lake na auache uovu..... Tena anasema 'lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia,mtu aliye mnyonge,mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu'. Tu wenye dhambi.......lakini tusing'ang'anie kutenda uovu kwa sababu Mungu anasamehe.

Well said Twin... Ila nina kesi na wewe!!
 
Rozari, Stickers, Kanzu, Joho n.k havimfanui mtu kuwa msafi hivyo huwezi kuhukumu kutokea vitu hivyo...

Mungu ninayemjua hutazama moyo wa mwanadamu na hupendezwa na moyo ule ulio msafi wenye kufanya ibada ipasayo
kwa kuwa una moyo safi tembea uchi basi. Au vaa gauni kama ww ni mwanaume
 
Mungu wetu si Mungu wa dhihaka wala maskhara na ndio maana tunaambiwa katika maandiko matakatifu kuwa Mungu hadhihakiwi

Kama huamini MUNGU je?! Maana wengine tunaamini na vitu tuvionavyo na macho yetu, yawe mazuri au mabaya...
 
Pia kuna hili suala la baadhi ya wapuuzi kuwa wanataja jina la mwenyezi mungu ktk thread au comment zao za kipuuzi,mfano mtu anaandika upuuzi wake usio na maana halafu ana attach na picha then anacomment kwaku sema "neema za allah"
 
Duh... Twin uko deep!

Haya endelea na huu mstari pia...

Warumi 6:12
Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake;

Hahahah...hamna twin....
Kweli kabisa....watu wanaona raha tu dhambi itawale miili yao....mtu mwenye hofu ya Mungu dhambi ikiingia inampa shida tena haoni raha kutembea katika dhambi simply bcoz Mungu anasamehe....tunatakiwa tudumu katika kujitakasa na si kuhalalisha uovu..
 
Pia kuna hili suala la baadhi ya wapuuzi kuwa wanataja jina la mwenyezi mungu ktk thread au comment zao za kipuuzi,mfano mtu anaandika upuuzi wake usio na maana halafu ana attach na picha then anacomment kwaku sema "neema za allah"Hakika hii kufuru ya hali yajuu na mtu mwenye tabia yakuandika upuuzi huu bac hana tofauti na makafiri na nihalali kumwita kafiri coz amekidhi vigezo vyakuitwa KAFIRI

Sheikh kipozeo huyo sio sisi
 
Mathayo 12
39--Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona.

40--Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi.

41--Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nao watawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona.

42--Malkia wa kusini atasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, naye atawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu yeye alikuja kutoka pande za mwisho za dunia ili asikie hekima ya Sulemani, na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.

43--Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate.

44--Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa.

45--Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.
 
mungu wetu ni wa kusamehe ayo yote, ndio maana anasema njooni ninyi nyote wenye kuelemewa na mizigo nami nitawapumzisha.
 
Tambua kuwa sheikh kipozeo alitamka neno neema za Allah akiwa msikitin wala hakuwa Jf.Iweje nyie mlitamke ndani ya jf haliyakuwa hamna jukwaa linalozungumzia dini ya mwenyezi mungu?Na walaaniwe wale woote wanaotafuta umaarufu wakijinga kwakulitaja jina la mwenyezi mungu muumba wa mbingu na Ardhi pa1 na vilivyomo ndani yake
Sheikh kipozeo huyo sio sisi
 
Back
Top Bottom