Tusifanye usambazaji wa konekshen za watu kuwa jambo la kawaida, tunaharibu maisha ya watu

Naona tumefanya unyanyasaji wa mtandaoni uonekane kama kitu cha kawaida bila kujali kwa kufanya hivyo tunaweza kuharibu maisha ya watu wengi sana, kwasababu unyanyasaji au bullying kwa kimombo inaathiri sana afya za akili za watu...
Kwa upande mmoja nakuunga mkono kwenye hili hasa kwa wale ambao unakuta pengine ni mtaani limemkuta jambo watu wakarekodi hapo nipo na wewe kwa asilimia 100. Tatizo linakuja kwa hawa sawa ndugu zetu wasanii tena kibaya zaidi wapo ndani, hiyo rekodi walifanya hivo kwa sababu zipi?

Rekodi maana yake ni kuweka kumbukumbu ili ambaye hakuwepo eneo husika aweze kuona au kuapata habari flani. Inasikitisha sana hawa ndugu zetu wao wanaona ni kama kujipaisha kisanii sijui jina kumbe wanajiharibia kimaisha na sifa katika jamii. Labda nikuulize kidogo kuhusu Giggy je ni yeye wa kwanza tukio hilo limetokea? Hapana sasa huoni ni kwamba wao wenyewe ndiyo wanavyotaka?

Kuna msanii mmoja huwa napenda sana nyimbo zake japo siyo shabiki wake nampongeza sana. huwezi kukuta hata siku mmoja anajisifia mitandaoni kama anahiki wala kile au kashfa kama za kuwa na warembo au starehe . Ali Kiba. Ni kwamba naweza msifia kwa kuwa kalitambua hilo hata kama anamakando kando yake lakini amekwepa mitandao ya kijamii. Hawa wengine unakuta mtu mwenyewe hujipost ndiyo garama yake hiyo kusambazwa aka connection.
 
Wasanii wengi ni members wa freemason kule Kuna kitu inaitwa humiliation ritual yaani kutoa kaffara ya kufanya jambo litakalokuumiza ili shetani afurahi.
Kwa wanaume uliwa ndogo ndo maana ya nembo ya jicho,kwa wanawake ujifanya video picha zimevuja
Dooh ninaowaonea huruma ni mke na watoto wako watarajiwa kuwa na mume na baba kilaza kama wewe
 
changamoto ni wao wenyewe inakuwaje mujirekodi au we mdada ambae unarekodiwa una tatizo la akili?hiii siyo kitu sahihi kwani huenda ikawa tabia kabisa ila pia waache ujinga wa kujirekodi watu now wamechafukwa nhivyo wanaifosi furaha au kipato kupitia maisha ya watu wengine.
 
Kwa upande mmoja nakuunga mkono kwenye hili hasa kwa wale ambao unakuta pengine ni mtaani limemkuta jambo watu wakarekodi hapo nipo na wewe kwa asilimia 100. Tatizo linakuja kwa hawa sawa ndugu zetu wasanii tena kibaya zaidi wapo ndani , hiyo rekodi walifanya hivo kwa sababu zipi? Rekodi maana yake ni kuweka kumbukumbu ili ambaye hakuwepo eneo husika aweze kuona au kuapata habari flani. Inasikitisha sana hawa ndugu zetu wao wanaona ni kama kujipaisha kisanii sijui jina kumbe wanajiharibia kimaisha na sifa katika jamii. Labda nikuulize kidogo kuhusu Giggy je ni yeye wa kwanza tukio hilo limetokea? Hapana sasa huoni ni kwamba wao wenyewe ndiyo wanavyotaka? Kuna msanii mmoja huwa napenda sana nyimbo zake japo siyo shabiki wake nampongeza sana. huwezi kukuta hata siku mmoja anajisifia mitandaoni kama anahiki wala kile au kashfa kama za kuwa na warembo au starehe . Ali Kiba. Ni kwamba naweza msifia kwa kuwa kalitambua hilo hata kama anamakando kando yake lakini amekwepa mitandao ya kijamii. Hawa wengine unakuta mtu mwenyewe hujipost ndiyo garama yake hiyo kusambazwa aka connection.
Wanasema "there is no such thing as bad publicity"
 
Naona tumefanya unyanyasaji wa mtandaoni uonekane kama kitu cha kawaida bila kujali kwa kufanya hivyo tunaweza kuharibu maisha ya watu wengi sana, kwasababu unyanyasaji au bullying kwa kimombo inaathiri sana afya za akili za watu.

Siku hizi mambo mengi yapo hadharani na yanaelezewa kwa upana na urefu, Matatizo ya Afya ya Akili iwemo. Ni dhahiri kuwa haya mambo yanaweza muumiza mtu katika fikra yake na kusababisha msongo wa mawazo ambapo unaweza kuharibu mfumo wa maisha ya mtu au mbaya zaidi ukaharibu maisha ya mtu kimoja kuanzia kazini, chuoni, shuleni na hata nyumbani.

Mitandaoni ni moja ya sehemu ambayo tunafanyiana unyanyasaji mkubwa sana, tunatukana na comments za kutisha.

Chukulia mfano Mange alivyopost connection ya Gigy, tukumbuke ni jambo la faragha, halituhusu, yeye kupost na sisi kuendelea kusambaza na kushadadia huku tukituna kwa maneno ya kashfa tayari ni kosa na sio uungwana.

Ni kwasababu hatujiweki katika viatu vyao ndio maana tunaona sawa tu kuendeleza jambo hili, lakini fikiria mtu wako wa karibu leo, mama yako, dada yako au wewe mwenyewe unapatwa na jambo hili utaweza kuhimili manyanyaso na masimango yanayokuja kwako? Sasa kwanini tunaendelea kuwa sehemu ya watu wanaendeleza ukatili huu dhidi ya waathirika hawa?

Tubadilike, jamii bora inaanza kujengwa na wewe.
Hakuna mtuvwa kukutunzia Privacy yako, ni jukumu lako mwenyewe.

Usipojirekodi, jipiga picha na kupost mwenyewe, umma utaziona wapi?

Acha na usiruhusu mtu au usiruhusu mazingira yanayoweza kufanya upigwe au urekodiwe bila ridhaa yako.

Picha/Video chafu mara nyingi huwa ni kwa ridhaa ya muhusika maana atatengeneza mazingira ya kupigwa/kurekodiwa. Ukizuia hayo mazingira itakuwa umezuia na hayo mambo kutokea.
 
Giggy pesa ndio maisha aliyochagua ya udangaji nenda page yake anajipromote sasa sio ajabu kuanika papa na ndala kwenye media.
Labda aamue kumrudia Muumba wake pindi soko lake likidoda.
Maana wakishakosa soko kisa uzee ujifanya kumgeukia Mungu.
 
Back
Top Bottom