Tusiendelee kupiga kelele kuhusu Chatto!

Tusiendelee kupiga kelele kuhusu Chatto!

Ule usemi maridadi kabisa naona unatumika vizuri kabisa hapa ......KELELE ZA CHURA HAZIMZUII TEMBO KUNYWA MAJI. Pigeni kelele zote lakini CHATO lazima isimame. over.
 
Pamoja na kukamua korosho bado PhD yenyewe ina mushkeli

Korosho zenyewe alizosomea kashindwa kuziuza zimeishia kuozea kwenye maghala huko
Hapo ndipo unapopata uthibitisho wa udhaifu wa elimu ya Tz! Korosho zinaoza wakati tuna mtaalamu wa elimu ya juu wa kuzalisha mafuta kutokana na korosho.
 
Hello JF,

Sijui kwa nini naamini mkuu wetu ameamua ku act Childish!, Inavyoonekana baada ya zile projects za mwanzo kupigiwa kelele,kumemfanya mkuu wetu awe REBELLIOUS kama jinsi teenagers wanavyokuwaga rebellious,ukimkataza asifanye hiki ndio kwanza anafanya....sijui stratergies za ku deal na mtu kama huyu..but i think tuanze kumuignore, hata akifanya nini huko Chatto tusipige kelele. Badala ya topic za kulalamika kuhusu Chatto tuandike jinsi watanzania wenzetu wangefaidika kwa kufanyiwa hiki au kile,this might compel him to shift from being resistant person to be co operative person....

Karibuni,tujadili jinsi ya ku deal na Rebellious president!

Kaamua awe mkuu wa wilaya moja tu nchini!

Ndio alichoona anaweza!

Wakati hiyo ni kazi ya mkuu wa wilaya!
 
Kwani si amebakiza mwaka mmoja aondoke au atapata 5 mingine amalize aondoke ? .
 
Ujamaa umewaharibu watu yaani unaiongelea nchi kama vile mali ya ukoo kwamba watu waoneane huruma. Usichokijua hizo sehemu zilizoendelea kwa kiasi kikubwa ndizo zinazochangia pato la taifa hasa kwenye makadirio ya kodi na huoni kwa mantiki yako ni kama uonevu ???.

Kingine Pesa ya umma inapaswa kuwekezwa pahali ambapo pana uhakika wa marejesho makubwa ambayo yanaweza kutumika kuleta Huduma za kimaendeleo sehemu zisizo na fursa kubwa za kiuchumi. Hiyo ni concept ndogo sana za uchumi na uwekezaji ambayo ni vyema kuijua. sipingani na mtu yoyote kupeleka maendeleo sehemu yoyote ila sio halali yake itokane na mawazo kama yako


swali la nyongeza mkuu, uwanja mkubwa wa mpira chato unaoukalibia benjamini mkapa, utasaidiaje kuongeza pato la taifa
 
swali la nyongeza mkuu, uwanja mkubwa wa mpira chato unaoukalibia benjamini mkapa, utasaidiaje kuongeza pato la taifa

Aliyefikiria kujenga sidhani kama alifikiria pato la taifa zaidi kuliko kuuendeleza mji wenyewe. Mji wa chato ni mdogo sana sanaaaa kuweza kutoa return ya uwekezaji kama huo. Hicho tu kwa elimu yangu ndogo tu
 
Acheni wivu mbona na nyie mmewekewa stiegler gorge!(pun intended)
 
unasema uongo, kweli sijafika kanda ya ziwa ila kusini huku panatisha mikoa ua mtwara lindi ni hatari huwezi pafananisha na kanda ya ziwa huko raia wanabonyeza kinoma
Kusini kuna mikoa mingapi masikini na kanda ya ziwa hipo mingapi masikini kwa mujibu wa takwimu?
 
Back
Top Bottom