MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 10,250
- 22,320
Ninaandika kwa masikitiko makubwa kufuatia kuona watu mbalimbali maarufu (Public figures) wakitoa matamko yanayokatisha tamaa na kuwakera vijana. Siwezi kurudia yaliyosemwa ila mengi yana ukakasi. Ifike hatua serikali, CCM na upinzani wawe makini sana na watu wote hasa viongozi wanaotoa kauli za kulisema kundi la vijana kwa kukurupuka.
Vijana wa nchi hii ni wazalendo mno na wanaipenda nchi yao. Na wamekuwa watiifu hata kwa maagizo wasiyoyapenda. Wote tunajua vikwazo vilivyopo kwa vijana kwenye ishu za biashara hasa kuaminika na Taasisi za fedha. Tunajua changamoto kubwa ya ajira. Tunajua changamoto za kiafya hasa ya akili kutokana na msongo wa mawazo. Halafu anatokea mjinga mmoja na kuropokea vijana. HII SIO SAWA.
Ninakisihi sana chama changu CCM kushughulika na watu wa aina hii wanaoibua taharuki zisizo za lazima kwa vijana. Ikumbukwe mabadiliko ya kweli ya kisiasa huletwa na vijana kwenye nchi. Vijana wanaweza kubadili mwelekeo mzima wa siasa za nchi wakiamua. Mwaka 2015 tuliona CHADEMA ikibebwa na vijana na wakatutoa jasho. Mwaka 2021 vijana wa Zambia hawakutaka kujua chama tawala cha PF kilijenga barabara ngapi, vituo vya afya na mambo mengine makubwa bali waliamua kuchagua chama cha upinzani UPND na kuwaingiza Ikulu. Vijana wa Zambia walikuwa wakighasiwa na makada wa chama cha PF kwenye shughuli zao. Charles Taylor aliua watu wengi nchini kwake ila baada ya kucheza karata zake vizuri kwa vijana wakamchagua.
Ninashauri viongozi na Public figures watafakari sana kabla ya kuongea lolote kuhusu vijana kwenye media. Vijana wa Tanzania sio wajinga wala wavivu bali wamechagua kuwa wazalendo kwa nchi yao. Wanaipenda Tanzania kuliko inavyodhaniwa.