Vijana msikatishwe tamaa na wazee

singojr

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
5,308
6,884
Wazee wengi wamekuwa na kauli za kuona kuwa vijana tumepotoka, hawana mwelekeo na juhudi kama walizo kuwa nazo.Wanaona vijana hatufai kuongoza taifa, hatuna weledi na nidhamu ya uongozi kama walivyo wao. Lakini ukweli ni tofauti.

Sisi ndio tunaojituma na kujikwamua kiuchumi kielimu na kifikra kuliko wao katika zama zao.

Sis tunahakikisha familia zinakula milo mitatu wakati wazee walijipa umwinyi kwa kuleta mlo mmoja nyumbani tena usio na viwango.

Kwenye familia nyingi sisi ndio tunaosomesha wadogo zao kazi ambayo ilipaswa kufanywa na wazazi(wazee) lakini bado wanatuona wavivu.

Ni wazee wangapi wanajengewa nyumba na vijana wao, Je wao waliwajengea wazazi wao? Katika ujana wao walishindwa lakini bado wanatuona vijana ni wavivu.

Ni wazee wangapi kila siku tunawasikia kwenye dili za upigaji rasilimali za Taifa, lakini bado vijana tunalaumiwa kwa kutokuwa wazalendo.

Vijana wa sasa ndio wanafanya uchumi wa taifa ukue kwa kasi, ndio wanaopambana mpaka usiku wa manane kurekebisha maisha mabovu waliyorithishwa na wazee wazalendo.

Vijana tusikatishwe tamaa juhudi zetu ni kubwa kuliko zao, uzalendo wetu na weledi wetu ni mkubwa kuliko wao.

Tupambane watoto wetu wasiishi maisha mabovu kama yetu.
 
Huko sahihi kijana lakini unajenga juu ya misingi ya wazee! Wazee wakiamua kubomoa misingi hayo mnayojivunia hayawezi kusimama! Sisi tuliwekeza katika misingi hili nyie vijana wetu mkikua mjitambue mpambane mjikwamue na kuwakwamua ambao kwao mmejikuta mmezaliwa
 
Hao vijana kuna wengine au ni hawa wavaa vibukta na visendo vya manyoya?
Haijalishi vijana wanavaa vip ila ni smart generation ,hoa wazee wenu maofisini wanasumbua kutwa mara waandaliwe presentation kweny PowerPoint mara hivi hawana jipya.

Kiufupi wale maprofessor wa zamani elimu yao haiwezi kufanya lolote kweny jamii ya sasa zaidi ya kulaumu vijana ...

Hiki kizazi ndio smart zaid ya kile kilichopita
 
Hapo umezingua kijana!
 
Huko sahihi kijana lakini unajenga juu ya misingi ya wazee! Wazee wakiamua kubomoa misingi hayo mnayojivunia hayawezi kusimama! Sisi tuliwekeza katika misingi hili nyie vijana wetu mkikua mjitambue mpambane mjikwamue na kuwakwamua ambao kwao mmejikuta mmezaliwa
Wazee wengi hawakujenga misingi yoyote ya maana. Ada tu ya 20000 hawakuweza kulipa
 
Umesahau hawa wazee ndo wameharibu uchumi wa hii nchi kwa ujinga wao na fikra za kimasikini na ushamba umwinyi, ubinafsi na uchoyo
Wametupa kazi ngumu hawa wazee waliendekeza sana utelezi, hawakua na akili za uwekezaji yani wao waliona uwekezaji ni wa waarabu na wahindi
Me naamini kwa vijana wasaizi wanaodharauliwa miaka ya badae kutakua na matajiri wakubwa wenye ngozi nyeusi watanzania halisi
 
Wazee wengi hawakujenga misingi yoyote ya maana. Ada tu ya 20000 hawakuweza kulipa
Wewe unaishi wapi? Duniani au angani! Barabara, umeme, shule msingi hadi vyuo, taasisi mbalimbali, sheria na taratibu zote za kuishi kama wanadamu n.k hayo yote ni misingi! Ndo maana unaweza kuongea na kisimu chako cha TECNO ukasikilizwa! Endelea kuvaa mlegezo!
 
Wazee wengi wamekuwa na kauli za kuona kuwa vijana tumepotoka, hawana mwelekeo na juhudi kama walizo kuwa nazo.Wanaona vijana hatufai kuongoza taifa, hatuna weledi na nidhamu ya uongozi kama walivyo wao. Lakini ukweli ni tofauti.
Sisi ndio tunaojituma na kujikwamua kiuchumi kielimu na kifikra kuliko wao katika zama zao.
Sis tunahakikisha familia zinakula milo mitatu wakati wazee walijipa umwinyi kwa kuleta mlo mmoja nyumbani tena usio na viwango.
Kwenye familia nyingi sisi ndio tunaosomesha wadogo zao kazi ambayo ilipaswa kufanywa na wazazi(wazee) lakini bado wanatuona wavivu.
Ni wazee wangapi wanajengewa nyumba na vijana wao, Je wao waliwajengea wazazi wao? Katika ujana wao walishindwa lakini bado wanatuona vijana ni wavivu.
Ni wazee wangapi kila siku tunawasikia kwenye dili za upigaji rasilimali za Taifa, lakini bado vijana tunalaumiwa kwa kutokuwa wazalendo.
Vijana wa sasa ndio wanafanya uchumi wa taifa ukue kwa kasi, ndio wanaopambana mpaka usiku wa manane kurekebisha maisha mabovu waliyorithishwa na wazee wazalendo.
Vijana tusikatishwe tamaa juhudi zetu ni kubwa kuliko zao, uzalendo wetu na weledi wetu ni mkubwa kuliko wao.
Tupambane watoto wetu wasiishi maisha mabovu kama yetu.
Tanzania tuna uhaba wa vijana!
 
Haijalishi vijana wanavaa vip ila ni smart generation ,hoa wazee wenu maofisini wanasumbua kutwa mara waandaliwe presentation kweny PowerPoint mara hivi hawana jipya.

Kiufupi wale maprofessor wa zamani elimu yao haiwezi kufanya lolote kweny jamii ya sasa zaidi ya kulaumu vijana ...

Hiki kizazi ndio smart zaid ya kile kilichopita
Naona umeamua kuwavua nguo kabisa 😎
 
Wewe unaishi wapi? Duniani au angani! Barabara, umeme, shule msingi hadi vyuo, taasisi mbalimbali, sheria na taratibu zote za kuishi kama wanadamu n.k hayo yote ni misingi! Ndo maana unaweza kuongea na kisimu chako cha TECNO ukasikilizwa! Endelea kuvaa mlegezo!
Tulia we mzee ivyo vyote ulivotaja havina ubora hata kidogo kulinganisha miaka 60 ya uhuru
Sheria ni uozo
Elimu imeoza mliruhusu mitaala mibovu itumike
Umeme ndo sio wakuzungumzia
Kua mpole babu bomba kauli zenu si zilikua "mimi nimetafuta vyangu na wanangu watafute vyao " wakati wenzenu waliweka mikakati mizuri kwa vizazi vyao vya badae na maendelea ya uchumi
 
Wewe unaishi wapi? Duniani au angani! Barabara, umeme, shule msingi hadi vyuo, taasisi mbalimbali, sheria na taratibu zote za kuishi kama wanadamu n.k hayo yote ni misingi! Ndo maana unaweza kuongea na kisimu chako cha TECNO ukasikilizwa! Endelea kuvaa mlegezo!
Barabara zipi mmejenga, barabara nyingi zimejengwa kupindi cha Kikwete, Shule nyingi zimejengwa kipindi cha Mkapa na hospital nyingi zimejengwa kipindi cha Magufuli na Samia
 
Back
Top Bottom