Naunga mkono hoja. Kuna watu humu ni pinga pinga, wao kazi yao ni kukosoa tuu kila kitu na kupinga kila kitu, ukiwasahihisha, hawachelewi kukuita gamba, na ukisifia jema lolote la awamu hii, huchelewi kunyooshewa kidole kuwa unatafuta uteuzi.
P.
Nasi tumekuwa na allergy ya kukosolewa kiasi kwamba hata neno "kukosoa" tunajitahidi sana kubadilisha maana yake ili lifanane na kupinga! Maoni tofauti sasa tunaita " kupinga"! Kukosoa ndiyo nguzo ya siasa za ushindani; mtu anayehofu kukosolewa atakuwa na matatizo makubwa sana na hususan hawezi kuwa kiongozi wa kisiasa.