Tusemezane: Waziri wetu wa Mambo ya Nje,Prof.Kabudi amekosea nini na wapi kwenye hotuba yake kule Kenya? 'Washika bango' mnajijengea mazoea mabaya

Petro E. Mselewa

Verified Member
Joined
Dec 27, 2012
Messages
9,249
Points
2,000

Petro E. Mselewa

Verified Member
Joined Dec 27, 2012
9,249 2,000
Niliposoma humu kuwa eti Waziri wetu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba J.A.M. Kabudi ' ametia aibu' nchi kule Kenya, nikasita kuamini au kutoamini kwakuwa sikuwa nimeiona au kuisikia hotuba yenyewe. Baada ya kuiona na kuisikia hotuba husika, sioni hoja za wasema-hivyo.

Katika hafla hiyo ya Uwasilishaji wa Ripoti ya BBI pale Bomas Kenya, Prof. Kabudi, kama Mwakilishi Maalum wa Rais Magufuli alipata nafasi ya kutoa neno mbele ya halaiki iliyokuwepo pale ikiongozwa na Rais wa Kenya, Makamu wa Rais wa Kenya na Kiongozi wa Upinzani wa Kenya.

Kwanza, Prof. Kabudi alianza kumshukuru Mwenyezi Mungu; kumshukuru Rais wa Kenya na hata Rais Magufuli kwa uwepo wake pale kwenye jambo muhimu kwa Kenya, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. Pili, alionyesha kwa mifano uhusiano wa kindugu uliopo kati ya Kenya na Tanzania.

Tatu, Prof. Kabudi aliwafikishia Wakenya salamu za Rais Magufuli hasa kuwaunga mkono Umoja wa Mataifa na kuwafikishia ujumbe wake ambao ulijikita katika kuwataka wajirekebishe na kusonga mbele pamoja wakiwa wamoja. Akawasihi waweke mbele maslahi ya nchi yao badala ya wao mwenyewe kwakuwa nchi huanza.

Prof. Kabudi, pamoja na mambo mengine, alionesha tofauti kati ya Tanzania na Kenya kuhusu makabila na ukabila ambao huathiri pakubwa siasa na utengemano wa kitaifa nchini Kenya. Akawasihi kutoyaweka makabila mbele na juu ya Kenya. Wakati wote wa neno lake, alishangiliwa na meza Kuu pamoja na kaumu mzima iliyokuwepo. Alishangiliwa kwa ukweli wake ambao hakuwa anapepesa kuutoa.

Hafla ile haikuwa ya kuzungumzia mikataba ya kimataifa na hivyo kuzungumzia mikataba hakukuwa mahala pake. Hafla ile haikuwa kuzungumzia uchaguzi na hakufanya hivyo. Sasa amekosea nini na amekosea wapi? Hata mwishoni alifikisha ujumbe wa wazi wa moja kwa moja kwa Rais Kenyatta, Makamu wa Rais Ruto na Mzee Raila Odinga na wote waliukubali na kuufurahia wakichagizwa na shangwe za wananchi wao.

Prof. Kabudi hapaswi kuponzwa na ukweli wake kwa ndugu zetu Wakenya. Hapaswi kuponzwa na uwazi wake wa kuufikisha ukweli. Hafla ile ililenga kupata maridhiano na umoja ili kusonga mbele kama Wakenya. Ndiyo maana kaumu nzima ilishikana mikono na kumfuatilia Prof. Kabudi aliyewaongoza katika kauli na ahadi za kujenga Kenya mpya.

Tabia ya kuona kila kauli ina makosa ni kujenga tabia mbaya na inayotesa. Washika-bango muwe makini na mjiepushe na tabia zisizojenga!


Pia soma
 

VAPS

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2012
Messages
3,191
Points
2,000

VAPS

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2012
3,191 2,000
Alituwakilisha vema,kwa kusema ukweli kwa dhamira njema na mpangilio mzuri.Pia upande wa imani aliwaunganisha Wakenya kwa agano la umoja ambalo ni sala. Wengi wanao mnanga wanamuona mnafiki kwa kutoshauri mema katika taifa letu nadhani tuna Watanzania wengi waugwana sana wanakosa jukwaa la kuongelea. Kabudi anadhamira njema na ametumia vema jukwaa la Kenya kwa kusema BBI si ya Wakenya pekee bali EAC pia, hivyo basi kafikisha ujumbe kwetu pia Watz hususani mkuu wetu ajitathimini.
 

GUSSIE

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Messages
2,793
Points
2,000

GUSSIE

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2014
2,793 2,000
Umeshinda mkuu

Kwa hiyo ulitaka watu wasifikiri zaidi kwa jicho la tatu

Aliyoongea Kenya kuhusu maridhiano Yeye anashauri Tanzania maridhiano

Mkuu wewe Baba wa nyumba unaongoza kwa kujikojolea kitandani na mwanao anaona kila siku unaanika godoro la mikojo, Unawezaje kumshauri mtoto wako anayekojoa bahati mbaya mara moja kwa mwezi?

Kenya wana matatizo yao sisi tumeanza kuyatengeneza kwa kasi na sasa tumewazidi

Think twice mkuu
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
32,884
Points
2,000

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined Sep 22, 2008
32,884 2,000
Tabia ya kuona kila kauli ina makosa ni kujenga tabia mbaya na inayotesa. Washika-bango muwe makini na mjiepushe na tabia zisizojenga!
Naunga mkono hoja. Kuna watu humu ni pinga pinga, wao kazi yao ni kukosoa tuu kila kitu na kupinga kila kitu, ukiwasahihisha, hawachelewi kukuita gamba, na ukisifia jema lolote la awamu hii, huchelewi kunyooshewa kidole kuwa unatafuta uteuzi.

P.
 

Nkanini

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2017
Messages
1,747
Points
2,000

Nkanini

JF-Expert Member
Joined Jun 6, 2017
1,747 2,000
President Kenyatta kuwa jukwaa moja na opposition leader na wote wakaonyesha kuwa Kenya comes first!!!,je kuna uwezekano hili kutokea kwenye nchi yetu ?jibu ni NO na sio rocket science kutambua hivyo.na tuache siasa tuongelee ukweli ,suala la uchumi kukua na wananchi kuona matunda yake sisi bado sana ,angalia Kenya,Zambia ,wapo mbele mno.
 

Taso

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2010
Messages
2,053
Points
2,000

Taso

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2010
2,053 2,000
Sasa amekosea nini na amekosea wapi?
Kama unatuuliza sisi kakosea wapi, then unajijibu mwenyewe, then unatuuliza tena, basi hujui unachokisema, andishi lako lote ni moot point, na upeo wako wa uandishi na ujengaji hoja ni finyu kama njegere.

Ungesema kwenye kichwa cha habari, Kabudi hajakosea. Na ndani ya andishi lako usiulize tena "hapo kakosea wapi," maana unajenga hoja kwamba alichofanya ni chema.
 

jd41

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2015
Messages
3,111
Points
2,000

jd41

JF-Expert Member
Joined Aug 23, 2015
3,111 2,000
....mida flani nimeskia kumbe hiyo hafla/shughuli aliyoalikwa Kabudi Kenya ilikuwa inahusu maridhiano, sasa Prof kuzungumzia issue ya ukabila Kenya, hakukosea kwa sababu huo ukabila ndio unaowafanya wakenya kutafuta hayo maridhiano.
 

Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Messages
1,216
Points
2,000

Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined Oct 30, 2018
1,216 2,000
Ni ujinga kwenda kujenga kwa jirani huku kwako kumebomoka.

Anawaomba wakenya wawe wamoja huku nyumbani kwao Tanzania tunagawanywa kwa msingi wa kisiasa. Wakenya hawakukufika hapo kwa siku moja, walianza hivi hivi, mara wakikuyu, mara wajaluo, mara wakalenjin mara sijui nani mwisho ndio unaona wamefikia hapo.

Kabudi kaenda kenya kuwaonyesha kua wao wamejaa udhaifu, wamejaa matatizo huku akijaribu kuionyesha Tanzania kama a perfect country, kila kitu kinaenda smooth.

Kabudi hana cha kuwafundisha wakenya,
 

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Messages
20,600
Points
2,000

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2015
20,600 2,000
Ni wivu tu!

Kuna watu wanashindana naye, hata mimi nilishangaa, jana Tundu Lisu na yeye katafuta TV Kenya KTN na kuhojiwa eti anawashukuru Wakenya walivyomuuguza na kumchangia damu, sawa lakini vipi hiyo timing?
Nafikiri waliumia sana walivyoona Heshima aliyopewa P.Kabudi na kwamba nchi ilikuwa inamjadili.
Inashangaza sana hawa jamaa wanashindana na mtu halafu usikute P.Kabudi mwenyewe wala hajui kama kuna watu wanajishindanisha naye.
 

Kilatha

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2018
Messages
1,580
Points
2,000

Kilatha

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2018
1,580 2,000
It is not good diplomatic etiquette to criticise other nations directly especially of their social challenges kama vile viongozi wao awafanyi juhudi zozote za kutatua hilo.

Kabudi hakuwa akihamasisha au kushauri wakenya kuongeza umoja kwa maneno ya kistaarabu bali alikuwa kama akikosoa matatizo yao na kuwataka viongozi wafanye zaidi; many people don’t like that it is considered disrespectful.

Ni kama kukaripia watoto wa wenzako au kushauri/kuponda bila ya kuombwa jinsi ambavyo watu wanavyolea watoto wao.
 

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Messages
43,920
Points
2,000

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2010
43,920 2,000
Kipi hicho Mkuu?
anaposema Kenya waache siasa za chuki na wawe na mshikamano at the same time tunamuona Raila na Uhuru wameketi kwenye meza moja.

Je kwa tanzania ameshawahi kuhubiri upendo huo dhidi ya rais kukaa na wapinzani???
 

Forum statistics

Threads 1,380,914
Members 525,916
Posts 33,783,827
Top