Tuseme tu na ukweli Mawaziri na Wabunge wa CCM waliokuwepo awamu ya tano walikuwa wakatili!

NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
1,281
2,020
Ukiacha yule Marehemu Mpendwa wetu Mh. Mbunge Bilago aliyefariki labda na wale wa upinzani kidogo - Mawaziri na hata wabunge waliokuwepo katika awamu ya Mwendazake walikuwa wakatili sana. Ndiyo wengi wamepata sababu ya kumsema mwendazake kama ndiyo chanzo cha kila kitu. Mimi ninakataa - wabunge hawa na mawaziri hawakuwa na chochote cha kupoteza - mshahara wa mwezi milioni kumi na moja (11ml) na maposho mengine kibao atamkumbukaje Mwl anayelipwa shilingi laki 2.

Hawakujali kabisa maslahi ya watumishi na hata sasa wanaendelea kutokujali. Wanalipana miposho tu halafu watumishi wa umma ndiyo imekuwa mavictims wa kila baya linalotendwa na Serikali. Watumishi wa Umma hawafikiriwi kabisa kuhusu maslahi yao - hakuna kuongeza watumishi - kuna upungufu mkubwa lakini ubinafsi umewatwala Mawaziri na Wabunge hawalisemi hili kabisa. Wao wanataka delivery tu bila kuangalia maslahi ya watumishi.

Chukua mfano mmoja tu wa malipo ya penshni - kadri Serikali inavyoajiri ndivyo watumishi wanaoajiriwa wanavyoweza kuchangia vizuri zaidi kwenye Mifuko ya pensheni. Na kadri unavyopandisha mishahara ndivyo pia na michango ya pensheni inavyoongezeka. Kwa sasa watumishi hawapandishiwi mishahara unafikir michango kwenye Mifuko ya pensheni itakuwaje? Wanaostaafu ni wengi kuliko wanaoajiriwa serikalini unategemea kweli huo Mfuko wa PSSSF utalipa nini sasa? Yaani kelele ni nyingi kuwa PSSSF inakufa! - fedha zimechotwa!

Wala tatizo la msingi halisemwi - Wachangiaji kwenye Mifuko ya pensheni na wanaostaafu wanategemeana sana - inatakiwa wanaoajiriwa wawe wengi kuliko wanaotoka lakini pia mishahara inapaswa kupanda kila wakati - wale wanaotoka ni yamkini mishahara yao inakuwa ni midogo kuliko yule atakayetoka kesho au keshokutwa na yamkini inasababisha yule anayechangia leo aweze kumlipa yule anayekula pensheni yake leo. Sasa hamna nyongeza na pia hamna kuajiri unategemea nini sasa kwenye kulipa penshni hapo?

Hayo yote yameletwa na Mawaziri na Wabunge wakatili na wabinafsi wa awamu ya tano - hawakuwepo kabisa katika na nafasi sehemu ya kuwatetea watumishi. Watumishi hawa hawakuwa sehemu ya wale waliofikiriaka ni walalahoi - watumishi walichukuliwa ndiyo maadui wa walalahoi. Awamu hiyo ama hakika ilitengeneza taswira mbaya sana kwa watumishi.

Watumishi wakaonekana kama vile wamnyoshwa na hiyo awamu - si Waziri si Wabunge wote ni kuwaangukia ubaya tu watumishi wa umma. Hata karani au Mlinzi wa Mahakama na alionekana kama mnyanyasa wanyonge - ama kweli hali ilikuwa mbaya sana.

Kwa sasa baada ya Mwendazake kuondoka basi hata Spika wao naye anaonekana kubadili mtazamo! Akili inamrudia sasa - yaani Mwenyezi Mungu huyu sijui kwa nini huwa harudishi wafu waje wajionee mienendo ya marafiki zao. Yaani hata Ndugai? Yaani hata akina Heri James, yaani hata akina Kigwangala?

Kikubwa Mei Mosi hiyo hapo imefika! Hamna dalili kama mishahara ya walalahoi hawa itaongezwa au utamaduni wa Mwendazake utaendelea? Yaani kazi kweli kweli!

Hamna Waziri wala Mbunge ambaye aliwasemea wafanyakazi awamu ya tano na hili limeandikwa vizuri sana na inabaki kuwa historia, kwani wanafiki wa mwendazake wanazidi kuonekana! Juma lijalo tutawapata na wengine - bado tunamalizia na Kichere!
 
Back
Top Bottom