Kama benki na account vilikuwa siri ya marehemu, msimamizi atapata shida sana kujua kwamba kuna account ya kufuatilia. Huyu wa kwenye mada ni bahati alimwambia rafiki yake, ambaye ataijulisha familia.
Wanaofanya siri kabisa bila kusema popote, wakifa pesa zinabaki kwenye wanayoita dormant account kwa miaka mingi.
Baadhi ya benki, wakishakuwa na dormant account ya muda mrefu, hupeleka emails kwa mhusika mara kwa mara kumtaka aifufue account yake. Au hupeleka monthly statements kwenye email. Ofcourse baadhi wanajaribu simu pia - lakini marehemu hawezi kujibu.
Hivyo ni vema ikiwezekana kumonitor email account na simu za marehemu (japo password zaweza kusumbua) - vyaweza kusaidia.
Hitimisho - tulio hai ni vema tuwe na wosia, au angalau tuhakikishe mtu fulani mwaminifu anajua mali zetu za sirini.