Habari wana JF.
Tuache Siri kwenye vitu muhimu wakuu hasa kwenye family issues. Kuna partner wangu mmoja hapa kariakoo wiki mbili zilizo pita tulikuwa tunazungumzia kuhusu usiri wa pesa tunazo weka Bank . Jamaa akanambia kahifadhi milioni 28 bank na mke wake hajamwambia hivyo katika familia yake hakuna mwenye taarifa hizo zaidi yake. Tugapipiga story pale na kushauriana mambo mengi ikiwa pia inatakiwa kuweka wazi baadhi ya mambo muhimu Kwa familia. Sasa juzi suddenly mshikaji kapata ajari na tumesha mpoteza(kafariki). Niliwaza vitu vingi Sana hivyo nimeleta hii thread hapa ili tujifunze kitu bank wananufaika na pesa na sio mke au watoto.
So the moral of this story is Let's not keep important family matters a secret. Imagine umejenga hakuna uliye mshirikisha, una pesa bank hakuna uliyemshirikisha, una MTOTO njee hakuna uliyemshirikisha, unabiashara hakuna uliyemshirikisha ukipotea suddenly it's worthless. TUPUNGUZE AU KUACHA KABISA SIRI kwenye mambo ya FAMILIA.
Hakika.Lazima kuwepo na Mipaka:-
1. Yapo mambo ambayo ni lazima yanapaswa yawe Siri, na yaendelee kubaki kuwa Siri daima au yanapaswa yawe Siri kwa muda fulani fulani tu.
2. Pia, yapo Mambo ambayo hayapaswi kuwa Siri, yanapaswa kuwekwa wazi.
3. Jambo au factors za Msingi za kuzingatiwa kukuongoza katika kuamua Jambo fulani aidha liwe Siri au liwe wazi, ni kutokana na unyeti wa jambo lenyewe, faida na hasara za kuwa Siri au wazi, Usalama wako binafsi pamoja na Usalama wa Watu wengine wote watakaoguswa na Jambo hilo, n.k.
TANBIHI:- USIRI ndiyo silaha nzito zaidi kuliko zote kabisa hapa duniani. Wewe binafsi ndio muamuzi wa mwisho ni kwa namna gani hasa unaweza kuitumia vizuri silaha hii.
Hata mimi mkuu, yaani kuliko kuamini kiumbe kiitwacho mwanamke ambaye ukifa anaenda kuolewa na mtu mwingine na ku spend pesa zako ulizomwachia na bwana mpya bora hele iliwe na benki.Hata mimi kwenye mambo ya pesa hua siwaamini hawa viumbe mimi wife mda wote namlilia njaa kila mda nalalamika sina hela😀😀 ila akiomba kitu nampa ila always story ni sina hela. Shida ya hawa viumbe akijua una hela anaanza kukupigia hesabu hela zako akuwekee demand zake ambazo hata yeye ameshindwa kutimiza kwa hela yakr wewe ndio umtimizie😹😹
Huo ni undezi.Ndiyo hicho ninachokisema hapa.
Sure.Yuko sahihi 100%
Kwa sababu
Katika uendeshaji wa fedha +Familia ni jambo gumu sana hasa katika zama hizi za watu wasio na utu.
Anaweza kuwa mtoto ama Mke wako pesa ikawa na Thamani kwake kuliko wewe mwenye pesa.
Katika mazingira kama hayo unapaswa kutumia akili kuendesha familia ya dizaini hiyo.
Tunakuwa na marafiki na Ndugu Pia,Katika has kuna watu mtu anakuwa anamuamini ambaye Anakuwa anajua siri zake ambazo hata familia Haijui. Inapotokea shida kama hiyo watasaidia walio baki.
Kuwa msiri kuna muda inatusaidia Sana.
Walio wasiri wengi wamefanikiwa.
Kama ukishidwa Kwa mke mwambie mama mzazi.Kuna thread jamaa mmoja alileta, alilalamika hela yake haitoshi matumizi.
![]()
Watumishi wa serikali mliwezaje kutoboa, mbona mimi naenda kushindwa
Habari za jioni. Nimeshindwa kupata usingizi kutokana na wimbi la mawazo. Wakuu Take home yangu 613K Mimi ajira mpya mwaka jana ila nimekuwa na wimbi la mawazo na kuona kama sitaweza kutoboa labda nIpate washauri wengine wa maisha labda. Nnafanya kazi mkoani,ila kadri siku zinavyoenda ninaona...www.jamiiforums.com
Wanaume wengi wakamshauri amfiche mweke mshahara wake, ili asiwe na mategemeo makubwa.
Watu wengi walionekana kukubaliana na hilo, sasa kipi ni kipi?
Ukishidwa mke mwambie hata Mama mzazi Siri zako.Hata mimi kwenye mambo ya pesa hua siwaamini hawa viumbe mimi wife mda wote namlilia njaa kila mda nalalamika sina hela😀😀 ila akiomba kitu nampa ila always story ni sina hela. Shida ya hawa viumbe akijua una hela anaanza kukupigia hesabu hela zako akuwekee demand zake ambazo hata yeye ameshindwa kutimiza kwa hela yakr wewe ndio umtimizie😹😹