Tupinge malipo ya rada kama tulivyopinga dowans(richimondi)

ndugai anasema wapo uk wakiwawakilisha wabunge, inamaana chadema wameunga mkono swala hili? waingereza sio wajinga wanamafile yote ya wahusika wa rada hapo wamewapa tz kamtego tu

siungi mkono fedha hizi zirudishwe serkalini
 
ndugai anasema wapo uk wakiwawakilisha wabunge, inamaana chadema wameunga mkono swala hili? waingereza sio wajinga wanamafile yote ya wahusika wa rada hapo wamewapa tz kamtego tu

siungi mkono fedha hizi zirudishwe serkalini

Mbona hakuna hata mbunge 1 wa chama cha upinzani? Cheo sio mpinzani bali ni mwanasisiem b
 
Wabongo bana..maneno meeengi, lakini ni usanii mtupu..kwa mwendo huu wa bunge tunazidi kupotea tuu.
Nadhani, ni dhahiri kuwa Cheyo dhamira ya kusema uongo kweupe inamsuta..ndiyo sababu anajaribu kwa mbaaali kugusia kwamba upande wa Tz kuna udhaifu pia. Lakini Ndungai na wengine wameamua kuruka kimanga huo ukweli. Kwa upande mwingine, huyu Madam inaonekana ana uelewa mkubwa.. lakini ndiyo hivyo tena alikwisha nunuliwa siku nyingi..hivyo basi ameamua kuwa bega kwa bega na mafisadi. Very sad in deed!!
 
Kwani wameenda kuchukua chenji ipi? Kwani nani alinunua na akaacha chenji? Iyo chenji kwanini aliporudi hakuulizwa chenji iko wapi? Je aliyesahau chenji aliporudi mzazi alimuhadhibu au alimuacha? Je kama aliyeacha iyo chenji dukani alitaka arudi kimya kimya kwa mangi ili awe ananunulia bisi,biscuit na pipi? Kwa nini asiende aliyenunua hapa baba anamtuma mwana mwingne? Mangi akisema simpi uyu/ndugai,ntawapa wanangu/NGOs ziwaletee home kwani hamuaminiki mtapita duka la pili kula pipi' ,mtamaindi? Hapana ,hapa inabidi mtoto akili kwanza kusahau chenji ndo wanafamilia/watz tutamuelewa. Azawaizi,daianeni kimya kimya bila kutupigia kelele!
 
Watanzania bana ukiwasikiliza wakati wakiomba kwa sauti ya huruma utafikiri wana maana wasikilize wanavyosema pesa zitanunua vitabu milioni 4 zitajenga vyoo 2,900 nchi nzima, zitajenga nyumba za walimu 1,196 zitatengeneza madawati laki mbili yote haya utadhani ni ya ukweli.
 
ibu kubwa hatujaona kama serikali kuwa kunavwatu wamehusika na wanastahili kuchukuliwa hatua zakisheria ila tunadai change eti BAE walituibia!! Its funny!
 
Nakumbuka juzi waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa alisema kuwa pesa zote tunapaswa tupewe kupitia serikali yetu na si kupitia NGO'S mbalimbali ili kuweza kusaidia mambo ya kimaendeleo mbalimbali maana hawaiamini serikali yetu tena, lakini waziri amekataa na kusema hawako radhi kuona nchi yetu ikidhalilishwa namna hiyo bora wasamehe hiyo pesa.

Je kwa kauli hii ya waziri unadhani mambo yatakuwa shwari?
 
nina wasiwasi na uelewa wa uyu wazir, kwanza mpaka sasa hajatutajia waliosabisha hii hasara, hajasema mpaka sasa serikali imewachukulia hatua gani! kazi kulalamikia serikali ya uingereza badala ya kuwachukulia hatu hawa watz waliosababisha hii hasara, mwache asuse kwani nani atapata hasara?
 
nina mashaka sana na uelewa wa mh. MEMBE katika masuala muhimu yanayohusu mustakabadhi wa taifa hili na watu wake, M. MEMBE alipaswa kwanza alieleze taifa na bunge kwa ujumla wake ni ni haswa kilichotokea katika sakata la rada.
1. Aeleze uhusika wa tanzania na uingereza katika ununuzi wa rada hiyo.
2.Aeleze namna TAKUKURU kwa upande wa tanzania na SFO kwa upande wa uingereza walivyoshughulikia hilo suala
3.Aeleze huo ujasiri wa kusema kuwa tunadhalilishwa ameupata wapi.

Kwa uelewa wangu mdogo ni kwamba serikali ya uingereza ilipinga vikali tanzania kuuziwa hiyo rada walkidai ni ghali sana ukilinganisha na hali halic ya uchumi wetu, ni kulazimisha kwa baadhi ya vigogo waandamizi wa serikali ya tz wakati huo na wale wa BAE Systm waliofanikisha uuzwaji huu kugawana mlungula.

Serikali ya tanzania iliwahi kukanusha mara mbili kuwa hapakuwepo na RUSHWA wala harufu ya rushwa katika biashara hiyo. Ni juhudi pekee za SFO na wabunge wachache wa uingereza na wapinzani ndani wa bunge la 9 liloweka wazi na kuifanya kazi ya SFO kuwa rahisi kidogo hatimaye ilibainika kuwa rada ile iluzwa kwa bei ya juu sana il baadhi ya waheshimiwa wapate mlungulu. Pia ni juhudi pekee za bunge la uingereza na SFO zilizopelekea BAE kukubali kutoa kitita hicho cha fedha kurudishwa nchin tanzania.

katika masuala haya SERIKALI YA TANZANIA ilikuwa kimya na haikufanya juhudidi zozote za kubainisha ukweli zaidi ya kujitahidi kufisha ukweli,

AIBU YA MWAKA.
Leo linapoibuka suala la kurudisha hela MH. MEMBE ANAIBUKA NA KUTOA MAELEZO MAREFU YASIYOKUWA NA KICHWA WALA MIGUU. ETI TUNADHALILISHWA!!!!!!!!! kwanini tokea mwanzo hakujitokeza hadharani kutoa maelezo ya jinsi maafisa waandamizi wa tanzania kwa kuwataja majina walivyohusika na WIZI huu wa mchana!!!!!!!!! MEMBE ACHA KUTUZUGA NA MANENO YAKO YA KIJINGA. waache waliopambana kupata hizo hela watafakari cha kufanyia, ikiwezekana walipe sehemu ya madeni tunayodaiwa huku ughaibuni au waje waanzishe mradi mkubwa wa baradara na wausimamie wenyewe hadi mwisho. barabara au daraja hilo litaitwa RADAR BRIGE/ROAD

MEMBE UNAJIDHALILISHA MWENYWE.
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Mimi namsapoti waziri membe, kama hizo pesa wataziweka kwenye mashirika yao wenyewe sijui OXFAM halafu wanaishia kuwalipia mishahara waingereza wenzao Pauni 15,000 kwa mwezi! bora wasizilete maana tulisha zisamehe
 
Na. Lula wa Ndali (Raia Mwema)

KAMA umefuatilia japo kwa juu juu kile ambacho kinachosemwa na Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe "fedha zetu za rada" unaweza kujikuta umeamini mambo yafuatayo. Kwamba, kampuni ya BAE Systems ambayo kutoka kwao tulinunua rada ya kuongozea ndege (Watchman Traffic Control System), imeamriwa kurudisha fedha na mahakama.


Pili, fedha hizo zinazorudishwa kiasi cha Paundi milioni 30 hivi, ni zile ambazo tulilipia zaidi ya bei ya rada na hivyo ni "chenji" ambayo ni halali yetu.


Vile vile unaweza kuwa umeaminishwa kwamba fedha hizo ni mali ya serikali; kwani ni serikali ndio ‘iliyoingizwa mjini' , na hivyo ni muhimu fedha hizo kurudishwa "kwa serikali".


Pia unaweza kuwa umeaminishwa kwamba BAE inataka kuziingiza fedha hizi kupitia NGO ya Uingereza au hata NGO za Tanzania.
Kama wewe unaamini jambo lolote ama yote kati ya hayo manne, basi, wewe ni miongoni mwa watu ambao hawataki kutafuta ukweli. Yaani unazugika kirahisi, na yumkini ni miongoni mwa watu ambao ukisikia imesema "serikali imesema" basi huitaji kuhoji tena unaitikia tu "naam".


Naomba mniruhusu nifyatuke kidogo leo. Kama kuna Mtanzania ambaye amewahi kupitia jengo lolote la shule (si lazima awe ameingia na kuketi darasani) na anaamini lolote kati ya hayo, basi, mtu huyo huwa kama mbwa mbele ya chatu; kwani hujikuta akilaanika kifikra kiasi cha kupata kigugumizi cha mawazo. Mambo yote hayo manne hakuna hata moja ambalo ni la kweli.


Kwanza, fedha ambazo BAE imekubali kuzitoa kwa ajili ya "kuwanufaisha watu wa Tanzania" hazikuamriwa na mahakama yoyote ya Uingereza.


Baada ya Taasisi ya UchunguzI wa Makosa makubwa ya Ulaghai (SFO) ya Uingereza kuendesha uchunguzi ulioonesha kuwa rada ya Tanzania iliuzwa kwa bei ghali na kuwa kulikuwa na mazingira ya rushwa hasa kwa kuwepo ushahidi ulioonesha kuwa BAE ilimlipa dalali Shaileth Vithlani mamilioni ya paundi ili kulainisha watendaji wa serikali na kupitisha dili ya ununuzi, uamuzi ulitakiwa ufikiwe.
Na uamuzi huo ni aidha kuleta mashtaka dhidi ya BAE Systems pamoja na mtu mmoja mmoja ndani ya kampuni hiyo au kuachilia. Wasingeweza kuachilia; kwani ushahidi ulikuwa mkubwa.


Hivyo, BAE Systems wakaamua kukaa chini na SFO na kukubaliana mambo mbalimbali ili kesi isiendelee na wasije kuingia gharama kubwa.


Ikumbukwe kuwa wakati SFO inachunguza BAES na sakata la rada, Serikali ya Marekani nayo ilikuwa inaichunguza BAES kupitia Wizara yake ya Mambo ya Sheria. SFO na DoJ ziliamua kukaa na BAES na kuingia makubaliano ya kumaliza uchunguzi uliokuwa unaendelea.
Kwa upande wa DoJ, BAES ilikubali kulipa zaidi ya dola milioni 400 bila kutoa kinga mwamvuli kwa wote waliohusika au kwa makosa yote. Maana yake DoJ wanaweza bado kuleta mashtaka dhidi ya BAES na watendaji mbalimbali kama kuna ushahidi mpya utaibuka kuhusiana na yale waliyochunguza.


Kwa upande wa SFO wao wakaamua kukubaliana na BAES mambo fulani fulani ili kumaliza uchunguzi wao. Mambo kumi na moja yalikubaliwa kati ya BAES na SFO kuhusiana na upelelezi wao wa sakata la rada la Tanzania.

  1. AES watakubali kosa moja kwa mujibu wa sheria ya Uingereza ya Makampuni ya 1985 (kosa linahusiana na mambo ya kihasibu).
  2. Kukubali kwake makosa kutafanyika katika fomu itakayowekwa ambamo masuala ya kesi yataorodheshwa.
  3. Faini ya kosa hilo itawekwa na mahakama.
  4. Kampuni ya BAES itatoa kama hisani (ex gratia) malipo ambayo yatakuwa ni kwa ajili ya kuwanufaisha watu wa Tanzania. Kiasi kitakuwa ni paundi milioni 30 ukiondoa faini zitakazowekwa na mahakama. Namna ya kutoa fedha hizo itakuwa kama itakavyokubaliwa kati ya SFO na BAES. (muhimu kuzingatia kuwa serikali ya Tanzania haitajwi).
  5. SFO haitamshtaki mtu yeyote kuhusiana na utendaji wake kwenye suala hili isipokuwa kwenye masuala ya nchi za Hungary na Czech.
  6. SFO itasitisha uchunguzi wote kuhusiana na BAES.
  7. Hakutakuwa na upepelezi wowote dhidi ya afisa yeyote wa BAES kwa jambo lolote kuhusiana na sakata hili kama lilifanyika kabla ya Feb 5, 2010.
  8. Hakutakuwa na mashtaka yoyote ya madai dhidi ya mtu yeyote ndani ya BAES kwa jambo lolote lilikuwa linachunguzwa na SFO.
  9. Mfanyakazi yeyote wa BAES hatotajwa au kuhusishwa katika kesi yoyote kama mshiriki wa njama zozote katika kesi yoyote ambayo SFO inaweza kuleta ikihusisha watu wengine.
  10. SFO na BAES wote watatoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na makubaliano hayo.
  11. Makubaliano hayo yamefanyika chini ya sheria za Uingereza.
Hayo ndio makubaliano. Makubaliano hayo yalishtua taasisi mbalimbali za kisheria; kwani yalionekana kutoa kinga ya jumla kwa BAES kinyume na makubaliano ambayo BAES iliingia na Marekani.


Makubaliano hayo yalipotolewa hatukusikia serikali yetu (Waziri Membe au Mwanasheria Mkuu) kuyapinga. Hakuna kikundi cha wabunge kilichotumwa kwenda kudai SFO isiingie makubaliano hayo; kwani yalionekana kupendelea BAES, lakini yakaingiwa.


Jambo la pili ambalo yawezekana umeaminishwa ni kuwa fedha hizo ni fedha za "serikali". Kama ambavyo nimedokeza hapo juu, fedha hizo ni hisani toka BAES. Sio malipo ya deni, sio adhabu, sio, sio ishara ya kujirekibisha, na wala si fedha ambazo tulilipa zaidi ya bei ya rada. Hili ni jambo la kueleweka.


Fedha hizi ni fedha za BAES. Fedha ambazo Vithlani alipewa na BAES ili kufanikisha dili la rada ni dola milioni 12.4. Ni muhimu kuzingatia kuwa kampuni ya Vithlani ya Merling International ilisajiliwa Tanzania. Hivyo, kama kuna mtu ambaye serikali ingeweza kumdai fedha yake ni Vithlani.


Hivyo, utaona dola milioni 60 hivi ambazo BAE wamekubali kuwapatia Watanzania zinadizi sana fedha ambazo Vithlani alichukua. Na ndio maana zinawafanya watu watoke mate huko waliko.


Sio fedha za serikali hizi, na serikali yetu haina haki hata kidogo ya kuzidai; lakini serikali ikitaka inaweza kumdai Vithlani au kutaifisha hadi kuku wake na kumrejesha nchini afungwe miaka 1000! Hapo ndio kweli serikali inaweza kujionesha kweli imechukulia suala la rada kwa uzito unaostahili.


Jambo la tatu ni kuwa, Waziri Bernard Membe wanaeneza taarifa kuwa makubaliano hayo yanasema fedha zitaingizwa kwa kupitia NGO ya Uingereza au NGO za Tanzania. Hili si kweli. Makubaliano (kifungu cha tano) yanasema hivi kwa Kiingereza "The company shall make an ex gratia payment for the benefit of the people of Tanzania in a manner to be agreed between the SFO and the Company. The payment shall be £30 million less any financial orders imposed by the court".


Naamini Membe alitafsiri kwa makusudi ex gratia na kuleta kwenye Kiingereza kuwa as charitable walisababisha baadhi yetu kutafsiri kuwa ni "through a charity" ambayo kwenye Kiswahili tukafikiria ni "kupitia NGO".


Neno ex gratia ni neno la kisheria sio neno la hivi hivi tu. Lina maana "kama hisani"; yaani mtoaji wa malipo kwa namna ya ex gratia anafanya hivyo bila kuonekana kuwa amelazimika au amelazimishwa au hata bila kukubali makosa yoyote yale.


Mara nyingi hili linatokea katika mahali ambapo mhusika hajakubali makosa au hana makosa, lakini kitu kibaya kimetokea na hivyo dhamira yake inamtuma kutenda hisani kwa yule aliyeumizwa.


Sio lazima iwe ni kwenye jambo baya. Ex gratia yaweza kutolewa hata kwenye jambo zuri kama kuonesha shukrani. La msingi ni kuwa, mtoaji anatoa wakati mwingine zaidi ya kile anachotakiwa kutoa.


Hivyo, fedha hizo Paundi milioni 25.5 (Mahakama iliweka faini ya paundi laki tano), ni fedha za hisani kwa watu wa Tanzania.
Katika hukumu yake, Jaji Bean anasema hivi baada ya maelezo marefu ya kuelezea hiyo kesi: "The victims of this way of doing business, if I have correctly analysed it, are not the people of the UK, but the people of Tanzania"; yaani "wahanga hasa wa biashara ya namna hii, kwa jinsi nilivyoelewa, siyo watu wa Uingereza; bali watu wa Tanzania".


Utaona kuwa serikali ya Tanzania haikuhusishwa katika sehemu ya kurudishiwa fedha kwa sababu wao siyo waathirika; kwani wao ndio walishiriki kuwaumiza wananchi wao. Sasa wamepata wapi ujasiri wa kudai fedha za waathirika? Iweje walio jeruhi ndio wapewe fedha za pole?


Hili linanikumbusha kisa cha kiongozi mmoja ambaye baada ya kutuhumiwa kumpiga dereva risasi, baadhi ya viongozi wa serikali wakampa yeye ‘pole kwa yaliyomkuta'!


Jambo la nne; nadhani utakuwa umeshapata jawabu kuwa haijaamuliwa mahali popote kuwa fedha hizo ziingizwe kupitia NGO - iwe ya Uingereza au ya hapa nchini. Namna jinsi fedha hizo zitaletwa kuwanufaisha waathirika (Watanzania), ni kwa makubaliano kati ya SFO na BAES - sio mtu mwingine.


Haya yayote yanatufanya tujiulize swali moja kubwa: Kwa nini serikali (kupitia Waziri Membe) imetumia nguvu kubwa (ya kuomba ushirikiano wa wabunge "wote" na kutuma wabunge kwenda Uingereza) kudai kitu cha dezo?


Inakuwaje viongozi wetu wanatumia muda kwenda kubembeleza fedha za hisani zirudishwe kwao wakati wanajua kabisa kuwa kinachorudishwa sio deni wala malipo ya fedha ambazo serikali ilimgawia Vithlani?


Swali hilo ni muhimu; hasa tukiangalia mwitikio wa serikali ile ile kwenye masuala ya ufisadi wa Kagoda kwa mfano. Kagoda walichukua Sh. bilioni 40, lakini hatujasikia timu ya wabunge imejaribu kukaa nao na kuwataka warudishe fedha serikalini, kwanini?


Swali hilo linatufanya tuulize kuhusu mwitikio wa serikali hii hii kwenye suala la Meremeta na mabilioni ya shilingi yaliyochotwa na watu ambao wengine wamekaa humo humo kwenye serikali yao. Kwa nini serikali haikuwadai hawa?


Swali hilo linatufanya tuulize kama kweli hawa watu wana uchungu sana na fedha zetu, kwanini hawakufanya uchunguzi dhidi ya Andrew Chenge ili kuweza kuona mali alizonazo hazijatokana na mipango ya dili hizi; na sio yeye tu; bali na wahusika wengine wote?


Swali hilo linatufanya tuulize kama kweli serikali inaona imeonewa kwa nini haijaleta mashtaka mazito zaidi pamoja na kuifunga kampuni ya Vithlani (kama mwenyewe hajaifunga bado!), na hata kufaitisha mali zake?


Kwa nini katika mashtaka yao dhidi ya Vithlani hakuna mashtaka ya uhujumu uchumi, utapeli, n.k? Hivi kweli tunataka tuaminishwe kuwa kosa kubwa la Vithlani ni hilo la "kumdanganya mpelelezi"?


Hivi kwa nini hiyo serikali haijatoa taarifa yoyote huko Bungeni juu ya harakati za kumsaka Vithlani zimefikia wapi? Kwa nini serikali yetu ilipopeleka ujumbe huko haikupeleka ujumbe wa nguvu Interpol kuulizia na kutilia mkazo suala la kumkamata Vithlani ambaye anadunda tu huko aliko?


Sote tunafahamu sakata la posho za vikao sasa hivi (hatujagusa posho ya mawasiliano!) na jinsi gani mabilioni ya fedha zetu yanapotea kinyemela. Dk. Slaa, juzi, kagusia upotevu wa bilioni zaidi ya 200 ndani ya Jeshi la Polisi na Magereza, kwa nini hatujasikia wabunge wamemuita IGP Mwema kutoa maelezo? Au hizi fedha zinapoliwa na wajanja nchini hatuzihitaji kurudishwa isipokuwa zile za hisani?
Binafsi sitaki tuwe mashujaa wa kwenda kudai vya dezo, lakini vile vilivyo vya haki yetu tunashindwa hata kutoa maelezo! Sitaki kusikia serikali nzima inanyemelea fedha ambazo zinatakiwa kunufaisha Watanzania.


Sitaki kuambiwa kuwa ati leo hii serikali hii hii iliyotetea ununuzi wa kifisadi wa hiyo rada imeshindwa kuliomba radhi Taifa, na badala yake inajifanya kama ‘haijui' kilichotokea! Na kinachoniudhi zaidi ni kuwa wapo watu ambao wanaamini kabisa Watanznaia hawana uwezo wa kumjulisha moja na moja na kupata mbili. Tatizo ni kuwa kweli wapo wengine wenye shida hiyo!


Sasa mimi nina pendekezo. Serikali iachilie hili suala la BAES na SFO na tusubiri tuone wao watakuja na mtindo gani wa kutuletea fedha kwa ajili ya kuwanufaisha Watanzania.
Na badala yake serikali ibane matumizi yake, ifuatilie fedha zetu katika zile kesi mbalimbali, ifanye uchunguzI dhidi ya Chenge na timu nzima iliyohusika na dili la rada, iongeze mashtaka dhidi ya Vithlani, yakiwemo ya uhujumu uchumi, na iwabane wakohoe hadi senti zetu za mwisho.
Twende tudai kilicho chetu kutoka kwa hawa wenzetu. Hilo la Waingereza wanajuana wenyewe; kwani kama ni uzembe ulikuwa wa kwetu!
 
Muhafaka uliofikiwa kati ya Bae System na SFO juu sakata la ununuzi wa rada, na kupata baraka za mahakama, pamoja na mambo mengine unasema kama ifuatavyio: "BAE Systems shall make an exgratia payment for the benefit of the people of Tanzania in a manner to be agreed between SFO and the company. The amount of the payment shall be British pounds 30 million less any financial orders imposed by the court." Kulingana na uamuzi huo, kwanza siyo kweli kwamba fedha walio amuriwa Bae System walipe ni ile ziada iliyolipwa na serikali juu ya bei halali ya rada, bali malipo husika ni hisani tu ambayo serikali haina haki kudai. Pili uamuzi huo unaipa madaraka Bae system kwa makubaliano na SFO kubuni njia muafaka ya kuzifikisha fedha hizo za hisani kwa watanzania. Katika hali hiyo, ni kujidhalilisha sisi wenyewe tunapoanza kupiga kelele tukiitaka serikali ya uingereza na bunge la nchi hiyo kuingilia maamuzi hayo ya mahakama badala ya kumaliza suala hilo na Bae system yenyewe pamoja na SFO.
 
Aiseee kumbe Ex gratia ndiyo inayoitoa udenda serikali yetu du aibu kubwa hata wabunge walioenda kuidai naona kama wametutia aibu watanzania.
 
Membe na Serikali yake wakate rufaa juu ya maamuzi yako kama wanataka!!
 
Membe na Serikali yake wakate rufaa juu ya maamuzi yao kama wanataka!!
 
Back
Top Bottom