Tupinge malipo ya rada kama tulivyopinga dowans(richimondi) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tupinge malipo ya rada kama tulivyopinga dowans(richimondi)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by UMMATI, May 19, 2011.

 1. U

  UMMATI Member

  #1
  May 19, 2011
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni sawa pesa ya rada ilichukuliwa serikalini tunakubali, lakini serikali haina duka wala shamba. Chanzo cha pesa za rada ni kodi za wananchi. Serikali ilipewa dhamana ya kuongoza matumizi sahihi ya kodi zile za wananchi lakini kwa tamaa na njaa za viongozi wa CCM wakaona vema kudhulumu wananchi wake. Serikali iliyoiba kodi hizo za rada ndio hiyohiyo leo inasema inauchungu na wananchi, tena asilimia kubwa ya wahusika ndio haohao leo wanalilia pesa hizo walipwe tena. Mbaya zaidi hakuna hata mwizi mmoja aliyechukuliwa hatua za kisheria hadi sasa. Nyepesi nyepesi za uswazi zinasema jamaa wanazihitaji kwa ajili ya uchaguzi 2015, je hii ni haki?.
  Wanajamii tukomae pesa wasilipwe mafisadi, bali tuwaunge mkono wakoloni wetu pesa wapewe wananchi direct.:pound:
   
 2. Double X

  Double X Senior Member

  #2
  May 19, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mpuuzi MEMBE anajifanya ana uchungu sana na izo pesa, si amkamate chenge na idrisa rashid wapo wanatanua hapa hapa mjini??? izo pesa zirudishwe kupitia charity org mana zikipelekwa tena serikalini hakuna chochote kitakachofanyika. mwenye no ya membe anisaidie tafadhali.
   
 3. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Wakoloni wana akili sana. Maana wameona majamaa yatachakachua , yakabuni njia sahihi. Pesa zipite kwenye NGO. Sasa Membe anafura nini? Mbona hajawahi kukunja ngumi na kugonga meza kulaani wezi wa rada?
  Haki ya Mungu, upole wote ule ni ilikuwa janja, ila sasa ameguswa!
  Safi sana Cameroon.......
   
 4. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #4
  May 19, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  wenzetu wamewajibisha watu na taasisi zao. sisi huku ambako shughuli nzima ilitokea, wote waliohusika wako safi na salama. na bado tunadai chenji yetu...!!! Bongo bwana
   
 5. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Naomba tu kuuliza, baada ya Mh Membe kuwafokea BAE je wameufyata na kuzileta huo mpunga, mbona sisikii tena juu ya mwendelezo wa tamthiliya hii au sirikali yetu imeamua kuviminya vyombo vya habari visiripoti tena (incl BBC)???
   
 6. F

  FUSO JF-Expert Member

  #6
  May 19, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,867
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  • Unaambiwa kwamba umetapeliwa wewe unabisha
  • Waliokwambia wanafanya utafiti na wanarudi kwako kukuhakikisha kwamba bwana umetapeliwa na ushahidi ni huu hapa pamoja ya kiasi cha pesa.
  • Wewe bado huamimi amini unajiuliza hivi mimi kweli naweza kutapeliwa?
  • Wakwambia sasa ndugu yangu tunakurudishia hizi pesa zote ila hatukupi wewe moja kwa moja mfukoni kwako bali tutawalipia watoto wako ada, mavazi, matibabu na mambo mengine ya kijamii
  • Wewe unaruka mita mia -"nipeni hizo ni pesa zangu" na nawaambia kama mnataka kuelewane vibaya nyie jaribuni kuwapa wanangu muone.. nyie mna uchungu wa wanangu kuliko mimi?
  duh kweli bongo tambarare...
   
 7. K

  KALABASH JF-Expert Member

  #7
  May 19, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Sawa kabisa.Waingereza shikilieni uzi huo huo. Fedha zisirudshwe serikalini. Membe awapeleke watuhumia mahakamani halafu atakuwa na moral authority ya kuzungumzia hizo hela. Membe anaelewa kabisa maana ya kuwa na ubalozi wa uingereza hapa Tanzania. Hao jamaa wanaelewa na wanajua kabisa nini kitatokea hizo billioni za rada zjkipitishiwa serikalini.
   
 8. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mbunge wa Musoma mjini amesema kuwa kabla ya kuanza kujadili pesa za rada tuhakikishe kuwa waliosababisha zipotee nao wanapotelea jela.
   
 9. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #9
  Jun 24, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,249
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Yuko sahihi kabisa huyu kamanda! Naishangaa kabisa serikali yetu inang'ang'ani chenji wakati haiamini kama kulikuwa na rushwa ktk ununuzi wa dude hilo!
   
 10. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,377
  Likes Received: 3,140
  Trophy Points: 280
  Mimi ntajaribu kufikiria kuanza kujadili kuwa serikali ina haki ya rejesho la pesa za rada baada ya kuridhika pasi na shaka kwa kunitajia wale waliorejesha pesa za epa ni akina nani na ni pesa kiasi gani na ziko wapi????,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,vinginevyo serikali hii ya kifisadi ya ccm na kikwete haistahili kabisa kugusa pesa hizo..............bora uingereza waaamue km walivyofanya kenya kuwa hakuna kuipa serikali isipokuwa wayape mashirika yasiyo ya kiserikali..............km serikali ilikuwa na haki mbona haijawahi kudai wala kufanya uchuinguzi wowote?.........serikali kiburi namna hii inatakiwa kuchinjiwa baharini tu ndiyo jibu la yote tunayozungumza.................
  Kweli ccm ni pasua kichwa................yaani bado wanaendelea kukinga mikono zitue ttu kiwete atoe mgawo kwa mafisadi wenzake basi
   
 11. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Amesema bila nidhamu hakutakuwa na maendeleo......amehoji iwaje ,mawaziri waisifie china?????wakati china imejenga mifumo ya nidhamu....mla rushwa ananyongwa.......
   
 12. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #12
  Jun 24, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wabunge wengine hawana budi kumuiga mbuge huyu, maana wakisubiri tamko la Membe kuhusu suala hili la malipo ya chenji ya rada kupewa mda wa kugadiliwa watasubiri mpaka nabii Isa atakapokuja mara ya pili; kwani haiwezekani Anne Makinda akaruhusu mjadala ambao kwa vyovyote vile utamgusa pabaya Chenge ambaye ndiye aliyemsawazishia njia ya kuukwaa uspika
   
 13. kibonga

  kibonga Senior Member

  #13
  Jun 25, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 144
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Chenge ndio mwenyekiti wa kufuatilia chenchi ya RAda (Nchi hiyoo........ oooo inayoyoma.........ndugu.:israel:
   
 14. kibonga

  kibonga Senior Member

  #14
  Jun 25, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 144
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kuna lugha ya kuongea na mawe (huwa yanazungumza) fuatilia:music:
   
 15. KELVIN GASPER

  KELVIN GASPER JF-Expert Member

  #15
  Jun 25, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 962
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 60
  Huyu kamanda namfagilia sana. Jana ilikuwa siku yangu ya kwanza kumsikia anazungumza. what impressed me ni pale walipokwenda kumchangisha mchango wa mafuta ya mwenge, yeye akawaambia hawapi pesa ila watafute kidumu akawanunulie hayo mafuta ya mwenge. Jamaa wakakataa. Akawaambia mwenge utakapofika maeneo ya kwake wauzime kisha wakauwashe mbele kwa mbele. Ninauliza ripoti ya mapato na matumizi ya michango ya mafuta ya mwenge ipo? Au ni mradi wa Ma RC na Ma DC?
   
 16. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #16
  Jun 25, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kuna baadhi ya watu wamefilisika eti kwa kukataa kuchangia mafuta ya mwenge......wamebambikiziwa kodi za ajabuajabu huko Kilosa....hadi leo wapo hohehahe......
   
 17. Kulikoni Ughaibuni

  Kulikoni Ughaibuni JF-Expert Member

  #17
  Jun 25, 2011
  Joined: Dec 12, 2007
  Messages: 235
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 60
  Kabla ya kuwaletea habari na picha kuhusu ziara ya wabunge kadhaa waliokuja hapa Uingereza kufuatilia malipo ya fedha za rada,ninaomba kuweka bayana mtizamo wangu katika suala hili.Kwanza,naona kilichofanywa na wabunge hao ni mithili ya kuuza ng'ombe kwa ajili ya kesi ya kuku.Nilitamani walioongea na wabunge hao kuwauliza umuhimu wa wao kuwepo Uingereza muda huu ambapo kikao cha Bunge la Bajeti kinaendelea huko Dodoma.Kuna dharura gani kwa wao kuja hapa muda huu badala ya kusubiri kikao hicho cha Bunge kimalizike?Je wanawatendea haki wapiga kura wao?Na nani anawawakilisha wapiga kura wao wakati huu?

  Nimesema hii ni sawa na kuuza ng'ombe kwa ajili ya kumudu kesi ya kuku kwa vile kila mbunge aliyekuja analipwa mamilioni ya fedha kama posho za kujikimu.Waheshimiwa hawa wanadai fedha za rada zitatumika kuendeleza elimu ya watoto huko nyumbani.Swali la kwanza,kwanini wasingeokoa fedha zinazotumika kama posho zao kwa muda wote watakapokuwa hapa Uingereza,kisha fedha hizo zikaelekezwa kwenye elimu ya watoto wetu huko nyumbani?Binafsi,nadhani suala hilo lingeweza kabisa kushughulikiwa na ubalozi wetu hapa Uingereza unless watuambie kuwa hawana imani na utendaji kazi na Balozi wetu Peter Kallaghe (ambaye ninamfahamu vizuri kuwa ni mchapa kazi mahiri tangu alipokuwa huko Foreign Affairs na Ikulu).

  Lakini la muhimu zaidi ni ukweli kwamba historia inatufundisha kwamba fedha za aina hii husihia mifukoni mwa wajanja wachache.Sana sana zitawezesha kumalizika kwa ujenzi wa mahekalu ya vigogo,kama sio kuongeza idadi ya nyumba ndogo zao na misururu ya magari yao ya kifahari.Hivi waheshimiwa hawa wanaweza kutuambia kwanini wanatolea macho hayo mamilioni ya rada ilhali wameshindwa kuhoji kuhusu marejesho ya fedha za EPA?Vipi kuhusu zile fedha za mfuko wa pembejeo?Vipi kuhusu "stimulus package" yetu ya kizushi?

  Let's be honest,na nilitegemea sana wanahabari waliotuwakilisha kwenye press conference ya wabunge hao wangeibua hoja hizi,waheshimiwa hawa wamekuja Uingereza kutalii tu.Period!So far,katika habari husika hawatuelezi namna gani ujio wao utawezesha fedha hizo kupatikana,na kutuhakikishia kuwa kweli zitaelekezwa kwenye elimu ya watoto wetu.Remember,kamwe tatizo la viongozi wetu halijawahi kuwa kwenye upungufu wa maneno matamu bali utekelezaji wa ahaid wanazojiwekea wao wenyewe.

  Anyway,naomba kuwasilisha habari husika kama nilivyotumiwa na Miss Jestina

  Na kwa kumalizia,tuache kumchosha Mungu kwa kutaka aibariki nchi yetu ilhali sie wenyewe hatujibidiishi kuifanya Tanzania kuwa lulu ya Afrika na pengine dunia kwa ujumla.Au tunamtaka Mungu aibariki nchi yetu ili mambo yakizidi kwenda mrama tumlaumu yeye badala ya kujilaumu kwa uzembe wetu?

  Pia naomba kutoa wito kwa wanahabari wenzangu (hoping hamto-mind kukosolewa),let's go beyond the "photo-op" cancer inayowasumbua wengi wa wanahabari wenzetu huko nyumbani.Picha ni muhimu lakini la muhimu zaidi ni kuwabana viongozi wababaishaji kila wanapojipendekeza kuleta porojo zao.Mtakumbukwa kwa kuuwakilisha umma vyema na sio picha.Sorry guys,I think you could have done better than just reporting what they said.You just gave them a free pass na pengine bado hawaamini kama wamesalimika kuulizwa maswali magumu na Watanzania waliopo "dunia ya kwanza".

  CHANZO: http://www.chahali.com/2011/06/ziara-wa-wabunge-kudai-fedha-za-radana.html
   
 18. z

  zamlock JF-Expert Member

  #18
  Jun 25, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  awawezi kuzipewa kwa sababu tumeshatuma mail sana BAE system isiwape pesa serikali yetu ya ccm kwa sababu azitawafikia walengwa
   
 19. z

  zamlock JF-Expert Member

  #19
  Jun 25, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  awawezi kuzipewa kwa sababu tumeshatuma mail sana BAE system isiwape pesa serikali yetu ya ccm kwa sababu azitawafikia walengwa
   
 20. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #20
  Jun 26, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
Loading...