naomba twende wote kesho!!
Kupima yataka inataka moyo kama nyendo zako unaju kabisa kwamba zinatia shaka.
Labda mm nitoe ushuhuda wangu namna gani niliweza kupima japo nilikuwa naogopa hicho kitendo kama ukoma. Ni kwamba historia yangu ya nyuma ktk mahusiano haikuwa nzuri sana. Hivyo kampuni ninyofanyia kazi ina utaratibu wa kupima wafanyakazi kila mwisho wa mwaka ili kuendana na siku ya ukimwi duniani trh 1/12 sijui! Ss kila mwaka nikawa napotezea tu. Hapa huwa kuna zawadi nyingi sana na gharama kubwa huwa zinatolewa kama Tv flat za inchi 32, friedge, camera, Simu za bei n.kLeo asubuhi nilitumia usafiri wa jumuia kufika kwenye sehemu yangu ya kibarua.
Nilipanda usafiri huo njiani,kwa bahati mbaya sikubahatika kupata siti nikalazimika kusimama japo kwa nafasi.
Ile kutizama chini kwa maana y alevel sits kwa pembeni namuona dada wa makamo kiasi,amevalia sweater,amejitanda khanga juu na chini...na anatokwa jasho sana.
Anaonekana dhaifu sana na aliyekata tamaa,ana vidonda mdomoni na anajikuna sana,alijikuna kwa kujificha ficha huku akiogopa kuonwa,too bad!
tukafika kituo cha mwisho.alibaki nyuma ili awe wa mwisho kushuka,binafsi roho iliniuma sana si kwa sababu ana ugua ugonjwa niliouhisi,la hasha ila kwa yeye kukosa matibabu sahihi kwa wakati either kwa kutambua au kutokutambua.
Dada huyu nilimfuatilia bila yeye kugundua na alikua anaripoti kituo kimojawapo cha clinic ya dawa za kurefusha maisha,na alikua anaripot kwa MARA YA KWANZA,hii ndio iliyonifanya nije hapa kuandika!
Ndugu amka,usiogope kuijua afya yako,hata ukikwepa muda utakuumbua,itambue mapema na ujipange upya,ukimwi wa miaka hii sio ule wa 88.
Ona sasa dada inavyomcost,laiti angewahi pengine tungekua wote tunaelekea maofisini kuijenga nchi,na clinic inakua ni sehemu tu ya maisha ya akila siku kupata dawa za kuongeza nguvu,pole sana dada yetu.
Wakishapima Asprin na Heaven on Earth naomba mni Cc namimi niende.
Hahahah mimi bibi yenu ataenda badala yangu. Usisahau mimi na yeye ni mwili mmoja.
Tatizo wifi zetu wako wengi wakati mimi bibi yenu yuko mmoja na mmoja peke yake.You see!!! Ndicho nlichokuwa nasema kama wifi yenu akienda kupima kuna haja gani ya mm kwenda tena??!
Wacha niendelee kuijenga nchi bana...
Kupima ni paka pale mtu unaharisha kama ngisi, hivi hivi aisee utakufa kwa kirojo kabla mauti ali mauti kukufikia. Kwanza ukimwi wa siku hizi butuu. Dalili za aliye ambukizwa zinaanza kujitokeza after ten years kupita. Ule ukimwi wa kuanzia 1985 mpaka mwaka 1995 ulikuwa noma. Ukiiukwaa tu miezi sita dalili, mwaka ukiisha unaanza kuharisha, kukohoa koo koo kuuuuu huku unajamba. Mwaka moja na nusu niagieni niagieni mimi nakwenda kwa baba yangu, sito rudiii niagieni niagieni then uyo kwenye kiroba cha rambo kilo saba kwa kaburi kwa heri.
mkonowapaka mi ni katibu tuu nabeba mafile watendaji wa hiyo #teambazazi wanajulikana akina Rogie, Mentor; Kaizer, Asprin, Nicas Mtei, Ben Mugashe, mayenga; watu8; Kipaji Halisi; Mtambuzi; Dark City na KakaKiiza
Tatizo wifi zetu wako wengi wakati mimi bibi yenu yuko mmoja na mmoja peke yake.
Unadhani wasiwasi wetu upo kwa bibi basi!? mi zile hekaheka zako tu unapofanya ukaguzi ndo kidogo zantisha..
Usiku huu uko macho unafanya nini?