Hello
Leo nilikuwa na hamu ya izi mboga maini siyapendi sana ila leo nilikuwa na hamu nayo
Nikachukua maini nikayachemsha baada ya kuya katakata na kutoa lile gamba la maini baada ya hapo nikaanda nyanya karoti na hoho
Baada ya maini kuiva nikaweka mafuta baada ya kuiva nikaweka vitunguu na nikachanganya baada ya muda nikaweka maini nika kaanga pamoja na vitunguu kisha nikachukua nyanya iliyo sagwa vizuri nikaweka kisha nikafunika na kuweka pilipili baada ya hapo nika weka na karot pamoja na hoho ziive
Kama unavyoona
View attachment 3349031
Baada ya hapo nikawa naosha matembele niliyo yachambua vzr kisha nikayaweka yachuje maji
View attachment 3349032
Baada ya hapo nikaanza kupika sasa nikaweka mafuta pamoja na vitunguu
View attachment 3349033
Kisha nikaweka nyanya na kufunika nyanya za matembele sipendi kubrendi nakataka kama ivyo
Tu
View attachment 3349036
Baada ya nyanya kuiva nikaweka tembele sasa
View attachment 3349037
Nikafunika kwa muda kisha nikachanganya na baada ya kuiva nikasonga ugali safi maana murumbee ilianza kuuma sana
View attachment 3349038Karibuni wotee