Tupike nyama pori mzuri kwa ugali

Tupike nyama pori mzuri kwa ugali

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
33,977
Reaction score
67,599
Hellow wapendwa poleni na kazi leo tunapika nyama pori mzuri kwa ugali

Kwanza chemsha hii yangu sio ngumu kuiva ata mvuke peke yake unaivisha

wakati nyama iko jikoni niliandaa viungo vyangu kama unavyo viona hapo chini vzr vitunguu maji viwe vingi sana kuna watu wanatumia kitunguu kimoja kwa mboga mbili mimi nimetumia vitatu vitunguu kwenye mboga ni vizuri sana
1745511957748.jpeg

Baada ya hapo nikaanza kukaanga nyama kwanza baada ya mafuta kupata moto vizuri
1745512037824.jpeg

Nilikaanga kwa muda mpaka nilipoona nyama imeanza kuwa na rangi ya blown

1745512090367.jpeg

Kisha nika weka viungo vyangu vyote kwa wakat moja hapo
1745512141385.jpeg

Nika vichanganya vizuri kisha nikaweka nyanya nilio brend na wakati na brend nyanya naweka mafuta kidogo ili nyanya iwe mzuri zaidi

1745512212783.jpeg

Baada ya hapo nyanya kuiva nikaweka limao kidogo na source kama unayo unaweka pia nikaweka na pilipili
1745512297531.jpeg
Nyama yangu teyari kwa ugali unaweza kula kwa ndizi za kukaanga au choma pia unaweza lia na wali au chips karibu sana umeme ukirudi tutasonga ugali kwa leo inatosha. 😂
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom