Ablessed
JF-Expert Member
- Mar 19, 2013
- 4,616
- 3,502
Pole kwa uliyopitia na hongera kwa kupita salama. Nijuavyo mimi wanawake hatufanani hata kwenye mambo ya kawaida sasa inawezekana hata tuwapo wajawazito pia hatufanani kwani kila mmoja wetu ana experience ya peke yake . Kuna wengine hulia sana wakati wa kujifungua na wengine huwa kimya kabisa kama kwamba hana maumivu na wengine kipindi cha ujauzito huwa na nguvu ya kufanya kila kitu wengine hapana. Ninachoweza tu kusema tuko tofauti hata sijui kwanini labda malezi na koo tunazotoka .hakuna shida sunian kama watu kushindwa kuvumiliana, muda mwingine mimba ina maudhi madogo madogo lkn yenyen karaha kuliko kawaida na ukiichezea waweza kumpanda mtu kichwan.
sitak kumsema huyu mwanamke vibaya lkn inawezekana mtoa mada akaangalia upande mmoja tu wa sh. ageuze na upande wa pili tuone hali halisi.
nimezaa mara 3 na katika mara zote, nilijitahd sana kutokuwa msumbufu manake i used to tell myself mimba sio ugonjwa na wala sio umwinyi. papo mahal diabetes ilinisumbua sana lkn hata hapo sikujiendekeza manake kwanza kwa kujua niko na diabestes halafu ni mjamzito nilikuwa nashindw akumwomba Mungu anipe moyo wa subira, na uvumilivu na anio0ngoze jins ya kuishi ili nisiwe mzigo kwa yyte yule............
diabetes ilinichukua kiasi kwamba nikawa sina nguvu na mimba ni miez sita, ila nilijisemea sitak huruma zisizo na sababu i did let my hubby kwenda safari kikazi nikabaki nyumban na hali ambayo hata yy hakuwa anajua hatma yake the only thing i said to him ni kwamba kuish na kufa yote yapo mikononi mwa alotuumba so hata kama nikigoma asiende ni wazi kwamba hana msaada kwa wakati huo.
nakumbuka nilipoandikiwa siku ya kulazwa baada ya hali kuwa mbaya sana yeye hakuwepo lkn nilitoka na mwanangu mkubwa hadi hosp na Dr wakaona wanilaze i just told my kids watulie home waniombee sihitaj chakula wala nguo za kubadili i will manage to do my washing alone nikiwa hosp. waliona kama najitesa lkn nilitaka kuwa mzima so kulea ugonjwa sikupenda kabisa.
najifungua mtoto kwa CS niko pake yangu, na wanakuja wananikuta nimepakata kichanga na maisha yakasonga mbele.......toka hapo nilijifunza jambo kubwa sana kwamba muda mwingine haliz a mimba tukiziendeleza zina tukomesha na abadan MIMBA IKIINGIA HUWA INAKUULIZA NIKUWEZE AMA UNIWEZE?? UKIIAMBIA NIWEZE BASI HAMNA RANGI UTAACHA ONA NA MAUDHI YOTE YA DUNIA YATAKUWA JUU YAKO NA UKIIAMBIA NAKUWEZA UTAIWEZA NA HAITAKUWA KARAHA KWAKO.
huyu kaka kmpiga mkewe ni kosa sana, lkn take it from hakumpiga kwasababu aliona raha bali aliumia kuona ambavyo mkewe tena mjamzito kajipeleka kuumia mwenyewe ninja uhakika hilo jambo la kumfumania huyu shemej hakutaka na alitaka ajipooze ila kwa usiri sasa alipotokea mkewe akaona kwann amekuja kujiumiza kwa mambo kama haya?? nimejaribu tu kufikiri kwa njia pana zaid .
am sorry kama mtakwazika
Namshukuru mkwe wangu na mume wangu kwani daima walikua pamoja nami hata kwa mtoto wa mwisho. Ni kweli kuna wamama wanapitiliza lkn bado tuwahurumie ule mziki mnene. Sisi wamama wa sasa tujitahidi kuwafundisha uvumilivu watoto wetu wa kike na wa kiume .Kama ulivyoeleza maelezo haya akiambiwa kila mara mtoto wa kike naamini hawezi kujiachia kipindi chake kitakapofika. Na mtoto wa kiume pia tusimwache nyuma tumfundishe namna ya kubehave wakati mkewe awapo kwenye hali hii. Hapo tutapata mazao bora.