mwallu
JF-Expert Member
- Sep 5, 2013
- 6,787
- 4,207
Nashukuru Mungu kampeni dhidi ya ukatili wa kijinsia imepamba moto,pengine itasaidia kufuta kabisa ukatili dhidi ya wanawake na watoto.Mie nachukia sana ukatili dhidi ya mtu yeyote bila kujali jinsia.
Kuna huu ukatili kwa mwanamke kipindi cha ujauzito: kuna wanawake wengi wamepitia ukatili huu kwa namna tofauti tofauti..(kutokumjali mjamzito ni ukatili wa hali ya juu sana)
Dada yangu mie alipobeba ujauzito wake wa pili shemeji yetu alibadilika sana,kwanza akwa mkali kama pilipili kichaa,dada akimuomba amletee ukwaju anakataa,ubuyu hataki ,hata zile ice cream za bakhresa akawa mbishi kuleta.Tukimuuliza kwa nini anamfanyia hivyo mwenzie anasema dada anatumia mimba kumpanda kichwani.
Hakuna siku iliniuma sana kama ile dada alipomfumania shemeji akiwa restaurant ya jirani na nyumbani kwao,mida ya saa moja jioni,yuko na mwanamke wanalishana kwa midomo,cha ajabu shemeji wala hakushtuka,ndo kwaanza akaanza kumgombeza dada kafata nini hapo,dada alipoanza kugomba pale aliambulia makofi na mateke ya kumtosha tu hadi akazimia.
Alizinduka baada ya masaa matatu akiwa hospitali..na shemeji hakuonekana nyumbani wiki nzima.
Ilibidi dada arudi nyumbani..mpaka amejifungua,hataki tena kurudi kwa shemeji.Wakina mama wanamshauri arudi tu kwa mumewe maana huyo ni mumewe.
Baada ya Kujifungua Shemeji anakuja nyumbani kila jioni..na zawadi nyingi nyingi tu.
Wewe,jirani,ndugu jamaa yako,je alishawahi kupitia ukatili wowote au changamoto zozote kutoka kwa mwenzi wake kipindi cha ujauzito? alikabiliana nazo vipi? baada ya ukatili huo ndoa ama mahusiano yaliendelea?
ccKaizer ladyfurahia Passion Lady Lady Docto Arushaone Erickb52 Sungura2013 Mapi amu Husninyo Heaven on Earth DEMBA miss strong Baba V Mentor Excel Mamndenyi Ablessed Kongosho Rich woman kiwatengu shansarie miss chagga et al

Last edited by a moderator: