TUONGEE KIUME - "Fedha zina tupa Wanawake wepesi "

Kabla hatujafika mbali naomba turudie kusoma kichwa cha Habari .
Kimeandikwa "Pesa zina tupa Wanawake Wepesi "Hakisemi ni Dhambi kuwa na pesa au Kutafuta pesa.

Pesa ni Nguvu . Na nguvu ni kitu Muhimu kuliko kitu chochote hapa Duniani . Hata kabla ya kuanza mfumo wa pesa wa makaratasi na sarafu Tunazo tumia leo pesa zilikuwa zinatumika.

Binaadamu wa kale atumia nguvu na maarifa kama pesa , ili apate chakula ili bidi atumie vitu hivyo viwili ,
Kuwinda sungura au kupanda juu ya mti kuangua fenesi kwa wakati ule hiyo ndiyo Pesa ,

Ukiweka pembeni kazi za Mungu tu ,pesa inaweza kufanya kila kitu kingine kilicho chini ya Jua --Kununua Muda .Kununua Akili .Kununua Afya bora. Kununua .Kununua Heshima, Kununua Fedha zingine ili ziwe nyingi .Yaani inaweza kufanya kila kitu.

Ukiwa na Fedha Utakuwa na Marafiki wengi ,Utapendwa na kila mtu (hata kwa upendo bandia ).. Utaheshimiwa na Kuthaminiwa ,Lakini Changamoto inakuja ni Kwamba Ukiwa na Fedha Kuna Mambo Mengine Hauwezi Kuyapata kiuhalisia
Kwa mfano ---Kumpata mwanamke Ambaye unatamani(Mwanamke wa Ndoto yako) ni vigumu.

Kwanini ?--- Kwa sababu Pesa haina desturi ya kutojificha, Ukiwa na Fedha lazima Watu Watafahamu 'Kwa Jicho la Kwanza watakalo Elekeza kwako' Hata ukijiweka Katikati Ya kundi Kubwa la Watu Fedha Itachomoza Juu na kusema nipo hapa .kwa huyu Bwana.

Hii Maana Yake ni nini? --- Ni kwamba kila Mtu uliyemzidi Pesa atataka kuwa Rafiki yako , Kila Mtu atagiza Kukupenda .Kila Mtu ataigiza kukuheshimu na Kutamani kuwa Karibu yako
Maana Yake ni Kwamba hata kama leo hii ukimtaka Mwanamke Ambaye Yeye Binafsi hakuwa ana hitaji kuwa na wewe kwa Maana ya Upendo , Atakubali tu kwa sababu Kuna kitu kingine ambacho anaweza kupata Ambacho ni Pesa zako .

Na hii ndio sababu Tunasema--PESA ZINA TUPA WANAWAKE WEPESI. .

Mwanamke imara na mzuri ni Yule ambaye ana hitaji pesa sana sana . Lakini hayupo tayari kufanya kinyume na Matakwa yake au Kufanya vitu visivyo mpendeza ikiwemo pia kuwa na Mtu (Mwanaume ) ambaye hampendi ili tu apate hizo pesa ambazo anazihitaji sana.

Mwanamuziki wa Tanzania WAKAZI aliwahi kuandika ---- Mwanamke Mzuri ni Mwenye Tabia njema na Mapenzi Ya Dhati ,na Mapenzi haya nunuliki kwa Fedha ,Unaweza Kununua Tendo la Kufanya mapenzi lakini sio Upendo. .Huo ndio Ukweli

Na hii sio kwamba Tuna-walaumu wanawake Kwamba wanapenda Pesa hapana. .Ukweli ni Kwamba Tunaongelea wanawake kwa sababu hii kolamu ni Tuongee Kiume ..Lakini ukweli ni Kwamba hata Wanawake wenye Fedha , Fedha zao Zina wapa Wanaume dhaifu.

Wanaume walioshindwa Kutafuta Vyao Waano-tegemea Kuhudumiwa .,

Mambo Mawili ya kumalizia ; Kwanza sio Vibaya kuwa na Mwenza mwenye Fedha .

Lakini chakujiuliza, Je uko hapo kwa sababu ya Pesa zake au una sababu zilizo mbali na hiyo Nguvu yake ya kiuchumi ?

Na pili wale Tusiokuwa Angalau ya Nusu ya Tunazo Zitaka Tuendelee Kutafuta kwa jasho na Akili

By :Kelvin Kagambo
Mkuu umenena ukweli
 
Hivi mkuu ili tuseme huyu mtu ana fedha,inabidi labda bank account yake iwe inasoma balance ya kiasi gani??
...Binafsi: niwe na makazi ya kueleweka, yaani kajumba ka kueleweka, kausafiri kakueleweka...Toyota vx, Prado...vitegemezi wrote wapo vyuo vya kueleweka, nabadilisha mbona na kivazi ninapojisikia na Acc zangu mbili tatu zinazomeka jumla ya Milioni 15 na kila usiku zinaongezeka kwa biashara yangu ya bodaboda ama daladala mbili tatu!! Binafsi, naamini hapo nitakuwa nimefika..!!!
 
Unadhani ningeandika hivi kama sikuwahi kuwemo kwenye penzi? Kuna vitu vingi vinavyomfanya KE avutiwe hadi ampende ME na kwa wengi pesa si kigezo cha penzi ila wenye penzi la kitapeli.
I like u👊
Na huo ndiyo ukweli... ndiyo sababu wanakuwa na mahusiano zaidi ya kumi wakitafuta mwanaume mwenye pesa,sasa kama ana pesa halafu muhuni kawapanga kibao hiyo pesa inafaida gani hapo??
Mapenzi ya pesa siyo mapenzi ni kusukuma siku tu ziende...
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom