Money is no more an issue, know how to handle your woman

Mr George Francis

Senior Member
Jun 27, 2022
186
212
MONEY IS NO MORE AN ISSUE, KNOW HOW TO HANDLE YOUR WOMAN.

Leo sikwenda kazini, nikaona nipitepite mtaani kwetu nipige story na marafiki. Nilifika kijiwe kimoja cha bodaboda nikakuta ubishani mkubwa sana.

Mjadala wao mkubwa ulikuwa ni kwanini vijana wengi hawataki kuoa. Sasa kwenye story za watu wengi huwa kunazuka vistory vingine vingi, yaani huyu kaongea hivi na yule kaongea vile ilimradi tu story ziende.

Katika ubishani kuna mmoja akasema,
"Kinachofanya vijana washindwe kuoa ni ugumu wa maisha. Na vijana tulio wengi hatuna pesa na wanawake siku hizi wanajali wanaume wenye pesa.
Jamaa anakazia kuwa 'hapendwi mtu, bali inapendwa pochi' kama huna pesa kupata mwanamke mwenye mapenzi ya kweli hilo sahau."

Na mwingine akadakia, akasema
"Hakuna kitu kama hicho, pesa sio kila kitu. Mtu unaweza kuwa na pesa na bado usipendwe.
Wanawake wanapenda mwanaume uwe handsome boy bwana!! Eti pesa! Pesa kitu gani bwana!!"

Dah! wengine wakaangua kicheko tu,
"Eti handsome boy!!? Hahaha!! Handsome bongo!!!"

Nami nikawa na mambo machache ya kushare na marafiki pale kijiweni.

🕸️Unajua tunawakosea sana wanawake kwa kuwasema kuwa wanapenda sana pesa. Ukweli ni kwamba pesa inapendwa na kila mtu lakini pesa sio sababu ya mwanaume kupendwa au kutopendwa.

🕸️Kama mwanamke anakupenda, atakupenda tu hatakama ukiwa huna pesa, na kama hakupendi basi hakupendi tu hatakama ukiwa na pesa.

🕸️Pesa inaweza kununua penzi (tendo la ngono) lakini haiwezi kununua upendo. Ukitaka penzi la elf moja miatano au elf tatu unapata lakini hakuna kiasi cha pesa kinachoweza kununua upendo.

🕸️Lakini pia mwanaume kuwa handsome au kutokuwa handsome hakuna uhusiano na kupendwa au kutopendwa. Huo ni mwonekano tu ambao unaweza kupotea muda na saa yoyote.

🕳️Je wanaume ambao sio mahandsome hawana wanawake wanaowapenda?

🕳️Na wewe handsome, je vipi ikitokea mwonekano wako ukaharibika huwezi kupendwa tena?

🕳️Je vipi ukiwa fukara na huna pesa huwezi kupendwa?

Upendo ni kitu cha thamani sana kuliko pesa wala mwonekano mzuri. Unaweza ukawa na vyote hivyo na bado mwanamke asikupende. Lakini pia unaweza ukakosa vyote hivyo na bado ukapendwa tu.

🪐Muhimu kujiuliza, tukiondoa pesa kwenye mahusiano ni kipi cha ziada unachoweza kufaya ili kumvutia mpenzi wako kiasi cha yeye kutotamani kukupoteza?

🪐Ni kipi unachoweza kufanya ili kumpa furaha mpenzi wako kiasi cha kumfanya avutiwe zaidi kuwa nawewe?

🪐Ni kipi unaweza kufanya katika kuboresha hali yenu kiuchumi ili kumudu mahitaji yenu ya lazima?

🪐Ni lugha gani unaitumia unapozungumza na mpenzi wako?

🪐 Je, mna mipango gani mizuri kuhusu kesho yenu au kwake ulifuata sex tu?

Mwanamke kuomba pesa kwa mpenzi wake sio dhambi. Kila mtu duniani anahitaji support, hivyo elewa kuwa hata mpenzi wako anahitaji support yako.

Hata wewe unapohitaji support, mwambie tu unahitaji nini kutoka kwake ambacho kipo ndani ya uwezo wake.

Kama ana uwezo wa kukusaidia lakini hataki kukusaidia basi huyo kweli sio mtu wa kujenga naye future ni bukura tu kama bukura wengine hivyo tafuta namna yabkumdhibiti kabla hajamaliza kibubu chako.

Mapenzi yanatengenezwa na mpenzi pia anatengenezwa. Mtengeneze mpenzi wako awe vile utakavyo wewe.

Usitamani wanawake waliotengezwa na wanaume wengine, au wale waliojitengeneza wenyewe. Kuna gharama kubwa utahitajika kulipia na hapo ndio utakuja kulalamika eti wanawake wanapenda pesa.

Nitamatishe kwa kusema kwamba,
"Money is no more an issue, know how to handle your woman."

#No_learnig_No_earning
So We Have To Learn.


NAME: George G Francis
EMAIL: mr.georgefrancis21@gmail.com
a37ea64e2a5b6c348bc284d0e9fe4a67.jpg
 
Back
Top Bottom