TUNDU LISSU V/S UONGOZI CHADEMA
Inasikitisha sana kuona Tundu Lissu akifanya kampeni zake bila viongozi wa kuu wa chama, wale wana gombea ubunge tunajua hawawezi kuwepo kila pahali, lakini wangeweza kujumuika naye sehemu muhimu kwa muda mdogo au siku moja, pia kuna wale wasio gombea ubunge, kama akina Mnyika na wazee wakiostaafu. Watu wengi wanjiuliza kuna nini kinachoendelea.
Siasa zinakuwaga na mambo mengi ya kimiujiza na mbinu nyingi za kukwamishana na kusaidiana, Hata hivi sasa hatuoni Chadema na ACT wakijengana.
Lakini kitu tunachokiona na kushangazwa nacho, ni kuwa LISSU amekuwa A ONE MAN SUPER SHOW, anafanya kampeni zako kwa ufanisi na ameweza kuwavutia watu zaidi ya hata CHADEMA ikiwa na viongozi wake wa juu.
Hii inaonyesha kuwa Chadema bila Mbowe inawezekana, Hata iwapo Lissu atashindwa kwenye kura, basi wanachama wa chadema, safari hii wanaweza kumlazimisha Mbowe amuachie Uwenyekiti wa Chama Lissu, na chama kitoke majombo ya Kilimanjaro na Arusha, na kiwe cha Kitaifa, kama kampeni za LISSU zilivyo.
Well done Lissu, kwa kuwaonyesha viongozi wa juu Chadema, kuwa umefanikiwa kukipeleka chama kwa wananchi kila kona ya nchi hii.