Uchaguzi 2020 Tundu Lissu V/S uongozi CHADEMA: Inasikitisha sana kuona Tundu Lissu akifanya kampeni zake bila viongozi Wakuu wa chama

Kwa upande mwingine, ni vyema viongozi wasiongozane sana na Lissu kwani ni yeye pekee mwenye immunity ya kumwaga sumu anavyojisikia. Wengine wakiwepo anapotiririka wanaweza kutafutiwa sababu za kuwekwa ndani au kudhuriwa ili kuvuruga kasi ya kampeni. Badala ya TL kusonga mbele akaishia kufuatilia wenzake vituo vya polisi.
 
Lissu kanipiga block twitter hata sielewi kosa langu.


IMG_20201014_125838_664.JPG
 
Chadema kabla ya kurejea Lisu ilikuwa imejaa hofu na kukata tamaa. Lisu ameleta ujasiri na ndiyo maana anapata mapokezi ya nguvu Sana.

Bila Lisu, Magufuli angeacha kupiga kampeni maana alikuwa ameshafanikiwa kuwatisha viongozi wote wa Chadema.

Dakika za mwisho kabisa Mbowe akavunjwa mguu na kumpakazia kuwa alilewa.
Yaani nchi hii kila mtu ana mwogopa Magufuli ksipokuwa Tundu Lissu peke yake.

Laiti kama Lissu asingerudi, Magu asingepiga hata kampeni maana alidhibiti kila mtu ndio maana hata uchaguzi alitangaza kwa mbwembwe akijua utakuwa mteremko tu.

Kinana alijaribu kuwapa onyo kuwa uchaguzi hauwahi kuwa rahisi.

Wamefanya siasad wenyewe miaka 5, wamenunua wabunge, wamepora media na magazeti yote, wamewafunga wengine, kuua na kupiga risasi watu.

Ila leo ngoma mbichiiii, wanatumia nguvuuu kuubwa kwenye kampeni .

Wameshindwa kuwekeza kwa watu, wanategemea nguvu ya Dola ndio maana hali ni tete. 90% ya Kizazi chochote kipya mostly hawaipendi CCM, hata ikitumia miguvu kushinda uchaguzi huu CCM haina maisha marefu. Bad enough ni kwamba Magu kavuruga mpaka jumuiya za kimataifa zilishajua demokrasia Tanzania ni ya kuchongachonga sana ili kuombea misaada.
 
Mbowe ana hasira sana mwaka huu hela zimemtoka sana! Matajiri na wafadhili wao wa nje hawajawapa mahela mwaka huu! Ndio maana unaona Mbowe kanuna sana kaona bora aende kupigania ubunge.
Yaani aache kampeni kwenye jimbo lake aje aungane na mtu aliyeonesha uwezo mkubwa kumzidi Magufuli? Unaumwa mavi wewe!
 
Well done Lissu, kwa kuwaonyesha viongozi wa juu Chadema, kuwa umefanikiwa kukipeleka chama kwa wananchi kila kona ya nchi hii.
Hili silielewi kwa miaka takribani mitatu Lissu alikuwa mgonjwa nje ya nchi na amerudi siku chache kabla ya uchaguzi. Ni wazi kimantiki kuwa kama chama kimepelekwa kwa wananchi kila kona ya nchi hii ni wengine waliofanya kazi hii.

Tusisahau Mbowe amekaliwa vibaya na chama dola hai hivyo ushiriki wake kwenye kampeni za Lissu hauwezi kuwa full time. Naamini ndio walivyo jipanga zidi ya washindani wao.
 
Acha kueneza uwongo. Viongozi wote ni wagombea. Katibu Mkuu nakumbuka ilielekezwa humu abaki ofisini kuweka mambo sawa. Ndio maana mnamuzi muhimu km ya kusimamishwa siku 7 Mwenyekiti alitolea ufafanuzi mzuri. Huu ndio uongozi.

Lakini kila kitu naona kinaenda vizuri sana.

Uliza na vyama vingine vipoje.

Hongera sana Mbowe kwa Uongozi mzuri.
 
Kampeni sio jukwaani mkuu. Huyo Mbowe unayejaribu kumzodoa hapa ndio anayepambana kutafuta mianya ya pesa kwa ajili ya Lissu sio tu kwenye kampeni ila toka yupo mahututi Nairobi.

Mnyika na Kigaila wanabaki makao makuu sababu kulikua na shida ya coordination chaguzi zilizopita maana kila kiongozi alikua jimboni.
Ila Mnyika ndio anayekua anafanya paperwork yote na organization kwa majimbo yote akisaidiana na Makatibu wa kanda zote 10.

Chama ni kma mwili kila kiungo kina kazi yake mahali pake huwezi sema kwa kuwa jicho limeona hatari basi ndio la muhimu kuliko mshipa wa fahamu uliosafirisha senses kutoka jichoni hadi kwenye Medulla kuchakata ni hatari gani ambayo jicho imeiona!

So CHADEMA inamhitaji lissu na Mbowe kwa pamoja. Na hakuna ambaye wa muhimu kuliko mwenzake. Maana chama ni zaidi ya jukwaani.

Maoni yangu ni hayo tu
 
Back
Top Bottom