Uchaguzi 2020 Tundu Lissu V/S uongozi CHADEMA: Inasikitisha sana kuona Tundu Lissu akifanya kampeni zake bila viongozi Wakuu wa chama

Mkirindi

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
6,376
2,000
TUNDU LISSU V/S UONGOZI CHADEMA

Inasikitisha sana kuona Tundu Lissu akifanya kampeni zake bila viongozi wa kuu wa chama, wale wana gombea ubunge tunajua hawawezi kuwepo kila pahali, lakini wangeweza kujumuika naye sehemu muhimu kwa muda mdogo au siku moja, pia kuna wale wasio gombea ubunge, kama akina Mnyika na wazee wakiostaafu. Watu wengi wanjiuliza kuna nini kinachoendelea.

Siasa zinakuwaga na mambo mengi ya kimiujiza na mbinu nyingi za kukwamishana na kusaidiana, Hata hivi sasa hatuoni Chadema na ACT wakijengana.

Lakini kitu tunachokiona na kushangazwa nacho, ni kuwa LISSU amekuwa A ONE MAN SUPER SHOW, anafanya kampeni zako kwa ufanisi na ameweza kuwavutia watu zaidi ya hata CHADEMA ikiwa na viongozi wake wa juu.

Hii inaonyesha kuwa Chadema bila Mbowe inawezekana, Hata iwapo Lissu atashindwa kwenye kura, basi wanachama wa chadema, safari hii wanaweza kumlazimisha Mbowe amuachie Uwenyekiti wa Chama Lissu, na chama kitoke majombo ya Kilimanjaro na Arusha, na kiwe cha Kitaifa, kama kampeni za LISSU zilivyo.

Well done Lissu, kwa kuwaonyesha viongozi wa juu Chadema, kuwa umefanikiwa kukipeleka chama kwa wananchi kila kona ya nchi hii.
 
Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
13,581
2,000
Mbowe ana hasira sana mwaka huu hela zimemtoka sana! Matajiri na wafadhili wao wa nje hawajawapa mahela mwaka huu! Ndio maana unaona Mbowe kanuna sana kaona bora aende kupigania ubunge.
 
Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
8,766
2,000
Chadema kabla ya kurejea Lissu ilikuwa imejaa hofu na kukata tamaa. Lissu ameleta ujasiri na ndiyo maana anapata mapokezi ya nguvu Sana.

Bila Lissu, Magufuli angeacha kupiga kampeni maana alikuwa ameshafanikiwa kuwatisha viongozi wote wa Chadema.

Dakika za mwisho kabisa Mbowe akavunjwa mguu na kumpakazia kuwa alilewa.
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
21,130
2,000
Mwenyekiti wa Chadema anagombea ubunge.

Makamu Mwenyekiti ni mgombea mwenza wa Tundu Lissu.

Amebaki Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu ambao wanaratibu kampeni zote.

Viongozi wa kanda, mikoa, na wilaya, wamefanya kazi nzuri na inaonekana ktk kampeni hizi.

Mwaka huu hatujashuhudia kampeni ya mgombea Uraisi ikikwama au kuvurugika kama ilivyokuwa ikitokea mwaka 2015.
 
BUSH BIN LADEN

JF-Expert Member
Mar 16, 2019
3,461
2,000
Hela ya kampeni tu hadi watembeze bakuri hela za kufund uwepo wa viongozi wa chama eneo moja kwa mara moja watazitoa wapi?
 
OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
31,455
2,000
..Mwenyekiti wa Cdm anagombea ubunge.

..Makamu Mwenyekiti ni mgombea mwenza wa Tundu Lissu....
broo unadhani kuna hoja basi hapo. ni binadamu kufanya kila mbinu kukuchonganisha na ndugu zako wa karibu. viongozi wa Chadema maarufu karibu wote wanagombea. Mnyima ndio secretary kuratibu michakato yote. Mwalimu ndiyo huyo. Sijui alitaka nini,btw kwani hao wanaozunguka na Lissu sio viongozi?
 
The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
6,561
2,000
..Mwenyekiti wa Cdm anagombea ubunge.

..Makamu Mwenyekiti ni mgombea mwenza wa Tundu Lissu.

..amebaki Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu ambao wanaratibu kampeni zote.

..Viongozi wa kanda, mikoa, na wilaya, wamefanya kazi nzuri na inaonekana ktk kampeni hizi.

..Mwaka huu hatujashuhudia kampeni ya mgombea Uraisi ikikwama au kuvurugika kama ilivyokuwa ikitokea mwaka 2015.

Hili jibu linajitosheleza 100%

Labda tumuulize mleta mada swali hili;

Ameona timu ya kampeni ya mgombea Urais imekwama?

Mimi naona kila kitu kinaenda vizuri kabisa.

Kampeni zinafanyika kwa ufanisi wa hali ya juu pamoja na ukata wa fedha.

Zinafanyika kwa ufanisi mkubwa kuliko za mgombea Urais wa CCM pamoja na kuwa ana kila kitu fedha, medias, NEC na polisi.

Lakini pamoja na yote haya, hawaonani, wamepoteana kabisa..!!
 
UCD

JF-Expert Member
Aug 17, 2012
7,669
2,000
Ila ninaona sio kwa TL peke yake hata hao wengine hawajasaidiwa na viongozi wastaafu jambo ambalo sio kawaida.
Sijajua mkwamo huo umesababishwa na nini
JK alifungua kampeni huko Lindi, Magula anazunguka Kanda ya Nyanda za Juu (Mbeya, Iringa, Rukwa, Songea na Katavi), Mwinyi yuko Zanzibar, Makamu wa Rais Mstaafu leo yupo Kawe. Unataka wengine wapi sasa?
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
21,130
2,000
broo unadhani kuna hoja basi hapo. ni binadamu kufanya kila mbinu kukuchonganisha na ndugu zako wa karibu. viongozi wa Chadema maarufu karibu wote wanagombea. Mnyima ndio secretary kuratibu michakato yote. Mwalimu ndiyo huyo. Sijui alitaka nini,btw kwani hao wanaozunguka na Lissu sio viongozi?

..Nadhani hata hawaelewi maana na majukumu ya mgombea Uraisi.

..Mgombea Uraisi ni "mpeperusha bendera" wa chama, hivyo anawajibika kuwapigia kampeni wagombea wengine wa chama chake.

..Na utaratibu wa kampeni za mwaka huu unampa mgombea Uraisi muda mwingi zaidi wa kuongea na wananchi na kuinadi ilani ya chama.

..Ukiongeza Mwenyekiti na Katibu Mkuu ktk msafara wa mgombea Uraisi maana yake unapunguza karibu dakika 20 za mgombea kuzungumza na wapiga kura.

..kampeni za mwaka huu za Cdm ziko more efficient na more disciplined.
 
Naby Keita

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
4,911
2,000
Chadema kabla ya kurejea Lisu ilikuwa imejaa hofu na kukata tamaa. Lisu ameleta ujasiri na ndiyo maana anapata mapokezi ya nguvu Sana.

Bila Lisu, Magufuli angeacha kupiga kampeni maana alikuwa ameshafanikiwa kuwatisha viongozi wote wa Chadema.

Dakika za mwisho kabisa Mbowe akavunjwa mguu na kumpakazia kuwa alilewa.
Kwani amekana kua alilewa?
 
Mudawote

JF-Expert Member
Jul 10, 2013
7,816
2,000
TUNDU LISSU V/S UONGOZI CHADEMA

Inasikitisha sana kuona TL akifanya kampeni zake bila viongozi wa kuu wa chama, wale wanao gombea ubunge tunajua hawawezi kuwepo kila pahali, lakini wangeweza kujumuika naye sehemu muhimu kwa muda mdogo au siku moja, pia kuna wale wasio gombea ubunge, kama akina Mnyika na wazee wakiostaafu. Watu wengi wanjiuliza kuna nini kinachoendelea.

Siasa zinakuwaga na mambo mengi ya kimiujiza na mbinu nyingi za kukwamishana na kusaidiana, Hata hivi sasa hatuoni Chadema na ACT wakijengana.

Lakini kitu tunachokiona na kushangazwa nacho, ni kuwa LISSU amekuwa A ONE MAN SUPER SHOW, anafanya kampeni zako kwa ufanisi na ameweza kuwavutia watu zaidi ya hata CHADEMA ikiwa na viongozi wake wa juu.

Hii inaonyesha kuwa Chadema bila Mbowe inawezekana, Hata iwapo Lissu atashindwa kwenye kura, basi wanachama wa chadema, safari hii wanaweza kumlazimisha Mbowe amuachie Uwenyekiti wa Chama Lissu, na chama kitoke majombo ya Kilimanjaro na Arusha, na kiwe cha Kitaifa, kama kampeni za LISSU zilivyo.

Well done Lissu, kwa kuwaonyesha viongozi wa juu Chadema, kuwa umefanikiwa kukipeleka chama kwa wananchi kila kona ya nchi hii.
Mpunga toka kwa beberu, kama 2015 waliuza
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom