Mkuu
The Boss naomba nitumbukize senti sumuni katika hili bandiko
1.Historia inatufundisha vema. Kenya walipewa 'katiba ya pembeni' wakakataa, wakakomaa hadi walipopata katiba na kuipigia kura. Hadi hapo wananchi walishinda, kura iliamua tu mwelekeo.
2. Hoja ya Tanganyika ilikuwa nzito na ni nzito kuliko zote zilzokuwepo.
Hakukuwa na marufuku ingawa matumizi ya vyombo vya dola yalikuwa kwa mtu, bado katiba ya Warioba ingalitatua tatizo
3. Hoja ya Tanganyika ilitumiwa na CCM ili kuweza kuvuruga bunge.
Utumbuka k.mwenezi alisema 'Rasimu ya Warioba haikubaliki kwa vyovyote'
4. CCM walikuwa na katiba yao. Kuikubali ni kuwapa uhalali wa kuendelea kulaghai Taifa. Ilikuwa kudharau ya maoni ya watu milioni 45 kwa kukubali maoni ya CCM.
Yaani kupuuza maoni ya wengi kwasababu wachache wamekamata mpini
5. Katiba iliyopo(1977) Pamoja na ubovu wake, haina kipengele kinachozuia mikutano wala kuwaweka watu mahabusu bila sababu za kisheria.
Kwavile imewezekana kukiuka katiba iliyopo hakuna uwezekano, mpya, ingekuja na kitu ambacho kingezuia hali iliyopo.
6. Kama wameweza kuvuruga uchaguzi wa znz unaoongozwa na katiba nini kingewashinda kukiuka hiyo ya Sitta ambayo wametengeneza wao wenyewe
7. Kukubali katiba pendekezwa kungepokonya wapinzani hoja ya katiba.
ccm wanajua katiba inayopendekezwa inaweza kufutwa wakati wowote wapinzani wakiingia madarakani. Kuwapa go ahead ilikuwa kujinyima haki kwa siku za baadaye
8.Ukisoma katiba pendekezwa, mambo yote yanayo favor CCM yapo intact.
Kilichofanyika ni kubadilisha lugha. Kukubali katiba hiyo ni kukubali maoni ya 1977'
9. Kama tunakubali katiba pendekezwa ambayo si maoni ya wananchi bali ya CCM, tunaweza kukasimu madaraka ya halmashauri kuu ya CCM kutenda kwa niaba yetu
10. Tukikubali nusu glasi ya maziwa hata kama ina funza tele,tukubaliane na lolote linalofanya sasa hivi. Tumekubali unyonge, hakuna unyonge afadhali , unyonge ni unyonge
Mandela aliaambiwa na makaburu wamtoe aache siasa, akasema atafia gerezani
Nyerere wamepitia wakati mgumu kudai uhuru, hawakukubali nusu glasi ya maziwa
Huko makaburini watakuwa wanageuka kwa 'ghadhabu' na wangepata fursa ya kurudi, wangetucheka kwa kuridhia unyonge hadi mbavu zipasuke warudi kaburini.