Tundu Lissu unakumbuka kitu?

Tundu Lissu unakumbuka kitu?

Katiba ya sasa Rais anamteua mkuu wa polisi
ni rahisi kwake kumpa amri

ingekuwa katiba hana mamlaka ya kumteua mkuu wa polisi ingekuwa rahisi kuliko sasa
katiba ni mchakato mrefu, hata kama ingepita isingeanza kutumika hapo hapo
 
Ajabu zaidi, wabunge wa ukawa pia including lisu waliafiki katiba isiweke mifumo ya kuwawajibisha wabunge wanaoshindwa kutimiza wajibu wao wa kuwawakilisha wananchi bungeni.
 
uko sahihi

Compromise

You can't get all at once.hasa katika mazingira ya kuwa minority kwenye representatives house
 
The Boss lakini bado UKAWA WaPo kwenye track wanachotakiwa sasa kufanya ni kutia presha ya katiba mpya...najua CCM watakurupuka na kuitisha Kura ya maoni kwa ajili ya katiba ya sitta...katiba ya Sita ikipita watakuwa wameyapata hayo unayoyasema...strategists wajipange vizuri
 
Kumpa lawama Tundu lissu ni kumuonea... Maana Lissu ni mgonjwa ana hitaji matibabu.
 
Tukumbuke tunapochangia hoja zinazohusu maslahi ya nchi yetu tutumie nafsi ya kwanza umoja na wingi sio ya tatu,kwani faida ikipatikana ni yetu sote sio ya lissu,isitoshe lissu hana shida sana kama baadhi yetu.
 
Mbona kuna mambo mengi yako kwenye katiba hii mazuri na yanavunjwa waziwazi?.Suala la katiba mpya au ya zamani halina maana kama viongozi walioko madarakani hawaheshimu katiba.Itoshe kusema kuwa,katiba haiheshimiwi kwa sababu suala la kuandamana au kufanya mikutano ya kisiasa limeelezwa vema kwenye katiba ya sasa na ni haki ya kila mtu.Hamna ca katiba mpya wala cha nini hapa.
 
Siamini sana katika kususa kwa sababu ina matokeo hasi, lakini pia kushiriki ili kupata katiba nafuu siyo garantii kuwa itafuatwa kwa sababu hata hii isiyo nafuu haifuatwi
 
Walipiga kura mpaka mahujaji mpaka marehemu ungetegemea nini hapo hata wangekuwepo?

Ndalama,
Hii hoja haina mantiki hata chembe. Awe Lissu wawe UKAWA kubakia ndani na kutozungumza habari za Tanganyika isingebadili kitu. Ma-CCM ndo walikuwa wengi kwenye Bunge la Katiba na hili lilifanywa maksudi na Mwenyekiti na Rais Mstahafu Jakaya Kiwete.
Kura ndo kila kitu katika upigaji kura kwa maamuzi ndani ya Bunge/Vikao na kwa msingi huo hata UKAWA wasingelitoka nje bado isingeleta matokeo chanya. CCM walikuwa wamedhamiria tangu awali kutoikubali RASIMU YA KATIBA YA WARIOBA kwa namna yoyote ile!!

Ndiyo maana leo hii mtu kama MAKONDA aliye mpiga na kumdhalilisha Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Warioba ameteuliwa kuwa DC na baadaye RC wa Mkoa wa Dar kama PONGEZI YA KUMPIGA NA KUMDHALILISHA Jaji Warioba!!!!!

Kuna watu wanafiki kama HUMPHREY POLEPOLE aliyeipinga kwa nguvu zote Rasimu ya Warioba kwa sasa nasikia naye ni DC wa Musoma Mjini!!!!!!

Lakini kama hiyo haitoshi bado nina hakika hata kama Rasimu hiyo ingelipita na kuwa Katiba Rasmi ya JMT bado isingesaidia. Rais tuliye naye kwa sasa haheshimu UTAWALA WA SHERIA NA KATIBA kitu ambacho kwa Magufuli alishakifuta kwenye kumbukumbu zake tangu azaliwe !! Hivo tusidanganyane hapa.
 
Umeongea vizuri sana mkuu. Nakubaliana na wewe. Very well thought!! Ila wapo wale watakaokupinga kwasababu wanazozijua wao.
 
Mkuu, Wanasiasa wengi wa Tanzania hawana vision, wao wanachoangalia ni sifa za wakati uliopo. Ndo maana nakuwa mgumu sana kuamini kile wanasiasa wanachokisema, huwa nabakia kuwa mtu huru tu nisiye na upande wowote.


I share your sentiments mkuu. Kuna shida kubwa kwenye political machineries zetu hapa nchini.
 
Bado katiba hii yenye viraka chungu nzima pamoja na ubaya wake inaruhusu maandamano na mikutano ya vyama vya upinzani ambayo hakuna yoyote mwenye ruhusa ya kuwaamulia wapinzani nini cha kuzungumza kwenye mikutano yao na wapi pa kufanyia mikutano yao bila kujali kama wana mbunge kwenye jimbo husika au la. Na yeyote anayewazuia wapinzani kufanya hivyo anakiuka katiba ya nchi.
Hupo BAK mambo yanaenda ila Katiba hii, na Tume hii ndio iliofanya Chadema wawe na Wabunge bungeni pamoja na CUF...
 
Tatizo la Chadema wanapenda shortcut, mfano walijijenga zaidi ya miaka 20, wakiwa wenyewe na nguvu, ghafla wanamchukua Lowasa.. Hii ni shortcut iliowagharimu sana.. Ni bora wangebaki na SLAA naamin wangekua na Wabunge wengi kuliko CCM..
 
Tatizo la Chadema wanapenda shortcut, mfano walijijenga zaidi ya miaka 20, wakiwa wenyewe na nguvu, ghafla wanamchukua Lowasa.. Hii ni shortcut iliowagharimu sana.. Ni bora wangebaki na SLAA naamin wangekua na Wabunge wengi kuliko CCM..

Adharus,
Huwa nawashangaa wa Tanzania wa aina yako ambao kufikiri kwao ni kudogo sana,
Hivi kwa akili yako unaweza kusema ujio wa Lowasa CHADEMA ulikigharimu chama kweli???
You must be joking. Kura nyingi walizowahi kupata CHADEMA katika miaka 20 ilikuwa ni milioni 2.7 mwaka 2010 Mgombea Urais akiwa Dr. SLaa. Mwaka jana 2015 CHADEMA walipata jumla ya KURA MILIONI 6+ almost 40% ya total votes na Wabunge wengi zaidi kuliko wakti mwingine wowote pamoja na CCM kuchakachua.
 
mkuu Boss I beg to differ,kiongozi aliyepo madarakani haheshimu katiba/sheria.mfano kuhusu vyama vya siasa/budget kupitishwa na Bunge ya kuhamia Dodoma etc.pia katiba kwa nchi zetu inatungwa kukidhi matakwa ya chama kinachotawala na viongozi wake.umewahi jiuliza kwanini sheria kandamizi zipo toka enzi za Nyerere ambaye wengi wanamuona ni Saint? kwanini hakujenga taifa lenye katiba ya kuwapa wapibzani wake/wananchi kila wanachoona kinawafaa? UKAWA waliona mbali mnoo.hiyo katiba ya ccm haitapita kwenye referendum labda waihujumu.pia haitadumu wakihujumu kura za maoni ya katiba
 
kama suala la Tanganyika na Zanzabar ccm kwa nguvu yao waliamua wanachotaka, hata hivyo vingine unavyovizungumzia walikuwa na uwezo wa kufanya wanavyotaka , bunge liliangalia maslai ya ccm kubaki madarakani daima, wasingeweza kufanya kama unavyofikiri
 
Back
Top Bottom