Tundu Antipas Mungwali Lissu, (Mb-Chadema) na msemaji wa kambi ya upinzani katika wizara ya katiba na sheria, jana akiwasilisha hotuba ya kambi ya upinzani ya wizara ya hiyo alisema kati ya mengi mambo ya upotofu, upotoshaji hivyo itahalis tukisema Tundu Lissu amepotoka.

Katika hotuba hiyo , wakati akitoa maelezo kuhusu mswada wa kuandaa utaratibu wa kutoa maoni ya mabadiliko ya katiba mpya ya JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, Mhe. Lissu alisema muswada huo bado una dosari hivyo kambi ya upinzani haikubaliani nao.

Kati ya dosari nyingi alizozitaja miongoni mwao ni uwepo au ushiriki wa Zanzibar kama mshiriki kamili wa mustakbai wa mabadiliko ya katiba hiyo. Mhe. Lissu alipotoka na kujipotosha aliposema:

a). kuwa mamlaka sawa aliyopewa rais wa Zanzibar na rais wa muungano hayakubaliki kwa kuwa yamefanywa "...kuwaonea huruma Wazanzibari baada ya kulalamika, kwa vile ilitosha rais wa zanzibar "...kuhusishwa tu.." na siyo kuwa na mamlaka sawa na rais wa muungano.

b). Wazanzibari wasishirika katika mchakato wa marekebishoa ya katiba katika mambo ya Tanzania bara kama vile Tanzania bara ilivyokuwa haikushirika katika mabadiliko ya katiba yao (mabadiliko ya kumi ya ktiba ya zanzibar ya 1984).

c). Katika uamuzi wa kupitisha katiba kilelezo "utaweka rehani " mustakbali wa mabadiliko hayo kwa vile iwapo Wazanzibari wakikataa na wabara wakikubali katiba hiyo haitapita, hivyo mchakato huu usiwekwe reheni na "siasa za Zanzibar".

MAWAZO YANGU:

Naamini Mhe. Tundu Lissu amefanya upotofu wa makusudi na anayefanya upotofu wa makusudi hawa amepotoka yy mwenyewe kwa vile:

a. Mhe. Lissu anajuwa kuwa muungano huu umeundwa kwa mkataba na siyo katiba na mkataba huo ndiyo unaotoa usawa wa mamlaka za nchi mbili kati ya Jamhuri ya watu wa zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika, katika yale mambo tuliyokualiana likiwamo la katiba ya Jamhuri ya Muungano.

b. Ushiriki wa Zanzibar katika mabadiliko ya katiba ya muungano siyo wa "hisani" bali haki yao na usawa walionao kwa mujibu wa makubaliano ya muungano na katiba hii hii mbovu, Mhe Lissu, kusema kuwa Zanzibar isihusike na mambo yasiyo kuwa ya muungano katika katiba hii ni kauli yakichekesho na aibu (nachelea kusema ya kipumbavu) kutoka kwa kinywa cha mwanasheria msomi aliyebobea. Mhe. Lissu anajuwa kuwa kinachofanyiwa marekebisho/mabadiliko hapa ni KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA SIYO YA TANGANYIKA?

Hapa alikuwa Mhe, Lissu, aje na hoja nyingine ya IPO WAPI KATIBA YA TANGANYIKA WAKATI ZANZIBAR WANAYO KATIBA YAO? ambayo itakuwa na mambo ya Tanganyika kama vile Zanzibar na Wazanzibari haitawahusu.

Ndiyo hapa wazanzibar wanapata na watapata uhalali wa kuikubali au kuikataa katiba ya JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, ambayo hatutakubali tena iingizwe mambo yasiyokuwa ya muungano, hivyo wala hatutakuwa na sababu ya kuyagusa.

c. Mhe. Lissu, anasema mambo kwa ujumla jumla, nani ataweka rehani hapa upitishwaji wa katiba hii? ni Wazanzibari au walioweka utaratibu huo kuwa katiba hiyo haitatumika mpaka ipate ridhaa ya pande mbili za muungano na kila upande kivyake! kwa akili ya Tundu Lissu watakao kataa ni wazanzibari tu,wakikataa Watanganyika je? si na wao watakuwa wameweka rehani mustakabali wa mabadiko haya kwa "siasa za Tanganyika?"

Hata hivyo, bado nakubaliana na maelezo mengine ya Mhe. Tundu Lissu kuwa mchakato huu uwape fursa watanzania waamuwe kama wanautaka muungano na wa aina gani?

Naona hueleweki hata kiswahili cha kuandika tu kinakupa shida ndugu, hebu sema ww wazo lako nini kati ya alichokisema Tundu Lissu, maana kwako ww kwakuwa anapiga makelele bungeni ndiyo ana "reason" hata kama anaongea upuuzi tu!
Rais wa Zanzibar ni waziri katika serekali ya JMT ni makosa makubwa sana kumpatia madaraka sawa na rais wa JMT.Zanzibar walibadili katiba yao wakaunda serekali ya umoja wa kitaifa Tanzania bara haikuhusika kuwamulia jambo lolote Zanzibar iweje mambo yasiyohusu muungano waZanzibar watuamulie ?.
lussu kwa kimakunduchi ni mbwa koko na tundu ni dema ie kitu kilichotoboka , kisicho na maana[/QUOTE]
Nakubaliana na wewe kabisa.
Hakika ugonjwa alionao Tundu Lissu ni sawa na ule wa WaTanganyika wengine kuogopa kutaja utaifa wao Kwa maana UTANGANYIKA na kuwa muwazi na kunena bayana pasi na khofu kuwa Kuwepo na Serikali ya Tanganyika ambayo ndanimwe itashughulikia mambo ya Tanganyika ambayo hayamo kwenye muungano kama ilivyo SMZ na kisha kuwepo na JMT.
Lakini haiwezekani na wala haingii akilini mambo ya JMT waZanzibar wasishiriki. Hii itakuwa ni kinyume kabisa cha katiba. Kwani hata muungano wenyewe pamoja na kuwa ni mkataba lakini vile vile ni BATILI
Kwani baada ya kufikiwa kwa Muungano mwaka 1964, Baraza la Kutunga Sheria la Zanzibar ambalo lilikuwa ni Baraza la Mapinduzi halikupewa nafasi ya kuridhia Muungano huo.
Ni lazima Baraza la kutunga sheria la Zanzibar kwa sasa ambalo ni Baraza la Wawakilishi lipewe nafasi ya kuridhia mkataba huo ili kuupa uhalali wa kisheria kwa upande wa Zanzibar,
Yasingekuwamo katika katiba ya Muungano wala Zanzibar isingeyaamuwa kama yale ya Zanzibar yalivyokuwa hayamo katika katiba ya Muungano wakayaamuwa wenyewe, yatakapoingizwa tena katika katiba mpya Zanzibar itayaamuwa kwa kuyakataaa, kwa hiyo hapa kuna tatizo la kimfumo wala siyo Zanzibar kama mwamuzi!
Ni kweli wewe una muono wa upenda mmoja .I though maandiko yote uliyo andika hapa yana point kumbe nikama wale wanaona amkia na matumbo yao kwenye supu ya utumbo.Pole sana kwa upupu huu rudia tena kumsikiliza Lissu uache kukurupuka .
Namuunga mkono lisu mia kwa mia, alichoengea mambo ya msingi, na huo usawa wanaotaka wazbr mbona haupo! Kwani wao wenyewe tunawasikia wakilalama kwy mambo kazaa ya kazaa kama vle kuna mbunge alihoji juu ya timu ya taifa kutokuwa na mchezaji kutoka kwy club za znz, hata pia kulalamikia kwy mambo mengi tu ya kudai wabara wanawanyonya waznbr. Mi naona bora hata huo muungano uvunjwe kila mtu afe na chake.

Wazanzibari wamekuwa wakisema kila mara wanapopata nafasi ya kuzungumzia muungano kwamba hawautaki. Lakini akitokea mtu wa bara akagusia juu ya huo muungano hasa ushiriki wao katika mambo yasiyo ya muungano wanakuja juu kama moto wa kifuu.

Pamoja na faida zilizopatikana na zinazoendelea kupatikana kwa Tanganyika na watanganyika kutokana na huu muungano kama vile za kiulinzi na kiusalama kama tunazoelezwa,kwa hapa tulipofika ni afadhali wabaki na zanzibar yao na sisi tubaki na Tanganyika yetu. Hatuna sababu ya kuendelea kuwalea wazanzibar, hapo tulipofika inatosha wachukue hamsini zao na sisi tuchukue hamsini zetu.

Tatizo Wazenji hawataki m2 wa Bara awasemee, hata kama huyo m2 yupo right kiasi gani! Wanakuwa na ka-element fulani ka udini, na huku bara -wanavyoamini- wengi ni makafir! Au GREAT THINKERS wengi wa huku ni makafir. Hawataki mwongozo utoke kwa makafir hata kidogo, ndo dini ye2 inavyo2ongoza, au 2nafikiri ndivyo inavyo2ongoza! lnafika wakti wazenj wengi wanaona bora hata kuongozwa tokea Oman kuliko tokea huku bara ( land of Qafirs) ambako possibility ya kuwa na Prezidaa Kafir ni kubwa. Sometimes, sorry, MOSTLY, udini unadumaza sana maendeleo na FIKRA +ve. 2naogopa tu kusema sana.l
Rais wa Zanzibar ni waziri katika serekali ya JMT ni makosa makubwa sana kumpatia madaraka sawa na rais wa JMT.Zanzibar walibadili katiba yao wakaunda serekali ya umoja wa kitaifa Tanzania bara haikuhusika kuwamulia jambo lolote Zanzibar iweje mambo yasiyohusu muungano waZanzibar watuamulie ?.