Tundu Lissu Umepotoka!

Junius

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2009
Messages
3,183
Points
1,170

Junius

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2009
3,183 1,170
Tundu Antipas Mungwali Lissu, (Mb-Chadema) na msemaji wa kambi ya upinzani katika wizara ya katiba na sheria, jana akiwasilisha hotuba ya kambi ya upinzani ya wizara ya hiyo alisema kati ya mengi mambo ya upotofu, upotoshaji hivyo itahalis tukisema Tundu Lissu amepotoka.

Katika hotuba hiyo , wakati akitoa maelezo kuhusu mswada wa kuandaa utaratibu wa kutoa maoni ya mabadiliko ya katiba mpya ya JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, Mhe. Lissu alisema muswada huo bado una dosari hivyo kambi ya upinzani haikubaliani nao.

Kati ya dosari nyingi alizozitaja miongoni mwao ni uwepo au ushiriki wa Zanzibar kama mshiriki kamili wa mustakbai wa mabadiliko ya katiba hiyo. Mhe. Lissu alipotoka na kujipotosha aliposema:

a). kuwa mamlaka sawa aliyopewa rais wa Zanzibar na rais wa muungano hayakubaliki kwa kuwa yamefanywa "...kuwaonea huruma Wazanzibari baada ya kulalamika, kwa vile ilitosha rais wa zanzibar "...kuhusishwa tu.." na siyo kuwa na mamlaka sawa na rais wa muungano.

b). Wazanzibari wasishirika katika mchakato wa marekebishoa ya katiba katika mambo ya Tanzania bara kama vile Tanzania bara ilivyokuwa haikushirika katika mabadiliko ya katiba yao (mabadiliko ya kumi ya ktiba ya zanzibar ya 1984).

c). Katika uamuzi wa kupitisha katiba kilelezo "utaweka rehani " mustakbali wa mabadiliko hayo kwa vile iwapo Wazanzibari wakikataa na wabara wakikubali katiba hiyo haitapita, hivyo mchakato huu usiwekwe reheni na "siasa za Zanzibar".

MAWAZO YANGU:

Naamini Mhe. Tundu Lissu amefanya upotofu wa makusudi na anayefanya upotofu wa makusudi hawa amepotoka yy mwenyewe kwa vile:

a. Mhe. Lissu anajuwa kuwa muungano huu umeundwa kwa mkataba na siyo katiba na mkataba huo ndiyo unaotoa usawa wa mamlaka za nchi mbili kati ya Jamhuri ya watu wa zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika, katika yale mambo tuliyokualiana likiwamo la katiba ya Jamhuri ya Muungano.

b. Ushiriki wa Zanzibar katika mabadiliko ya katiba ya muungano siyo wa "hisani" bali haki yao na usawa walionao kwa mujibu wa makubaliano ya muungano na katiba hii hii mbovu, Mhe Lissu, kusema kuwa Zanzibar isihusike na mambo yasiyo kuwa ya muungano katika katiba hii ni kauli yakichekesho na aibu (nachelea kusema ya kipumbavu) kutoka kwa kinywa cha mwanasheria msomi aliyebobea. Mhe. Lissu anajuwa kuwa kinachofanyiwa marekebisho/mabadiliko hapa ni KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA SIYO YA TANGANYIKA?

Hapa alikuwa Mhe, Lissu, aje na hoja nyingine ya IPO WAPI KATIBA YA TANGANYIKA WAKATI ZANZIBAR WANAYO KATIBA YAO? ambayo itakuwa na mambo ya Tanganyika kama vile Zanzibar na Wazanzibari haitawahusu.

Ndiyo hapa wazanzibar wanapata na watapata uhalali wa kuikubali au kuikataa katiba ya JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, ambayo hatutakubali tena iingizwe mambo yasiyokuwa ya muungano, hivyo wala hatutakuwa na sababu ya kuyagusa.

c. Mhe. Lissu, anasema mambo kwa ujumla jumla, nani ataweka rehani hapa upitishwaji wa katiba hii? ni Wazanzibari au walioweka utaratibu huo kuwa katiba hiyo haitatumika mpaka ipate ridhaa ya pande mbili za muungano na kila upande kivyake! kwa akili ya Tundu Lissu watakao kataa ni wazanzibari tu,wakikataa Watanganyika je? si na wao watakuwa wameweka rehani mustakabali wa mabadiko haya kwa "siasa za Tanganyika?"

Hata hivyo, bado nakubaliana na maelezo mengine ya Mhe. Tundu Lissu kuwa mchakato huu uwape fursa watanzania waamuwe kama wanautaka muungano na wa aina gani?
 
KALYOVATIPI

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2011
Messages
1,416
Points
0

KALYOVATIPI

JF-Expert Member
Joined Aug 11, 2011
1,416 0
sasa muungano wa nchi 2 nchi moja imejadili katiba na wananch wake wamepiga kura ya maoni na wamepata katiba yao sasa kuna ubaya gani kwa sehemu moja ya muungano nayo wananch wake wakihusika na kupiga kura ya katiba inayowahusu haraf hawa ambao mwanzo wameshajadili ya kwao wakajadili yanayowahusu ktk katiba? wewe GAMBA uwezi kuelewa.
 
Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2010
Messages
6,942
Points
0

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Joined Nov 14, 2010
6,942 0
Vipi utakua ushapata supu kweli kama si mlo wa mchana wa leo?? Tundu Lissu akili yake ni darasa ndefu kwako tena kwa miaka mingi sana tu hadi uje ukawa kwenye tawi moja na yeye kimawazo, upeo na maono. Hebu kajipumzishe pembeni kidogo na hayo maoni ya KI-KOMEDI.

Ni vema ukaelewa ya kwmba Wa-Tanzania hatuko kwa ajiri ya hiyo katiba kuu kuu ambayo wewe waonekana sana kuizungusha kamba shingoni bali ninachojua ni kwamba ni KATIBA lenyewe ambalo lipo kwa ajili yetu sisi hapa. Na kwa mantiki hiyo, ndio maana tunadhamiria kuliandika upya likakidhi matakwa yetu.

Wewe endelea kukalia kutamani kuona Watanzania tukiendelea kutekeleza matakwa ya KATIBA kamaambavyo mkubwa wako Selina amekua akijiabudia kila kukicha.
 
Naona hueleweki hata kiswahili cha kuandika tu kinakupa shida ndugu, hebu sema ww wazo lako nini kati ya alichokisema Tundu Lissu, maana kwako ww kwakuwa anapiga makelele bungeni ndiyo ana "reason" hata kama anaongea upuuzi tu!
 
Wezere

Senior Member
Joined
Nov 2, 2010
Messages
110
Points
195

Wezere

Senior Member
Joined Nov 2, 2010
110 195
Mh.. may be pana ukweli kiasi fulani kama ndo alichokimaanisha, lakini haya umesema wewe ngoja nisikie na ya upande wa pili i will be back
 
Ngongo

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2008
Messages
12,968
Points
2,000

Ngongo

JF-Expert Member
Joined Sep 20, 2008
12,968 2,000
Rais wa Zanzibar ni waziri katika serekali ya JMT ni makosa makubwa sana kumpatia madaraka sawa na rais wa JMT.Zanzibar walibadili katiba yao wakaunda serekali ya umoja wa kitaifa Tanzania bara haikuhusika kuwamulia jambo lolote Zanzibar iweje mambo yasiyohusu muungano waZanzibar watuamulie ?.
 
SOKON 1

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2010
Messages
1,123
Points
1,225

SOKON 1

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2010
1,123 1,225
acha kupotosha jamii kwani Tundu Lisu amesema wanzazibari washirikishwe ktk maswala ya Muungano tu na naya Tanzania bara yabaki ya bara kama walivyofanya wanzibari ktk kura za maoni na kubadilisha katiba yao. So ndivyo Tundu Lisu alivyosema.
 
Ndole

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2011
Messages
348
Points
195

Ndole

JF-Expert Member
Joined Jul 1, 2011
348 195
Samahani jamani mimi sijawahi kuisoma katiba ya Zanzibar. Naomba mnisaidie kidogo, kwenye katiba ya zanzibar hakuna sehemu inayoelezea mambo ya muungano? Kama kipo je watu wa Tanganyika huwa wanashirikishwa kukibadilishwa inapotakiwa kufanya hivo?
 
Brakelyn

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2009
Messages
1,257
Points
1,250

Brakelyn

JF-Expert Member
Joined Oct 6, 2009
1,257 1,250
Lissu hajasema kuwa muungano ni mbaya na haufai, bali amesema tuangalie ni vitu gani vihusike kwenye muungano na vipi visihusike kwenye muungano,,usikurupuke, elewa kwanza kilichoongelewa.........
 
Junius

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2009
Messages
3,183
Points
1,170

Junius

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2009
3,183 1,170
..... iweje mambo yasiyohusu muungano waZanzibar watuamulie ?.
Yasingekuwamo katika katiba ya Muungano wala Zanzibar isingeyaamuwa kama yale ya Zanzibar yalivyokuwa hayamo katika katiba ya Muungano wakayaamuwa wenyewe, yatakapoingizwa tena katika katiba mpya Zanzibar itayaamuwa kwa kuyakataaa, kwa hiyo hapa kuna tatizo la kimfumo wala siyo Zanzibar kama mwamuzi!
 
The Son of Man

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2010
Messages
12,546
Points
2,000

The Son of Man

JF-Expert Member
Joined Feb 9, 2010
12,546 2,000
Umeelewa alichomaanisha kisheria au ndo kujibu swali ambalo hujalielewa.

Watz 2na huu ugonjwa wa kutunga maswali cc wenyewe na kuyajibu as if kuna m2 katuuliza.

Nimemfuatilia sijui dadako Kombani alivyokuwa akijibu hoja kama yuko kitchen party!
 
Barubaru

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2009
Messages
7,162
Points
0

Barubaru

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2009
7,162 0
Tundu Antipas Mungwali Lissu, (Mb-Chadema) na msemaji wa kambi ya upinzani katika wizara ya katiba na sheria, jana akiwasilisha hotuba ya kambi ya upinzani ya wizara ya hiyo alisema kati ya mengi mambo ya upotofu, upotoshaji hivyo itahalis tukisema Tundu Lissu amepotoka.

Katika hotuba hiyo , wakati akitoa maelezo kuhusu mswada wa kuandaa utaratibu wa kutoa maoni ya mabadiliko ya katiba mpya ya JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, Mhe. Lissu alisema muswada huo bado una dosari hivyo kambi ya upinzani haikubaliani nao.

Kati ya dosari nyingi alizozitaja miongoni mwao ni uwepo au ushiriki wa Zanzibar kama mshiriki kamili wa mustakbai wa mabadiliko ya katiba hiyo. Mhe. Lissu alipotoka na kujipotosha aliposema:

a). kuwa mamlaka sawa aliyopewa rais wa Zanzibar na rais wa muungano hayakubaliki kwa kuwa yamefanywa "...kuwaonea huruma Wazanzibari baada ya kulalamika, kwa vile ilitosha rais wa zanzibar "...kuhusishwa tu.." na siyo kuwa na mamlaka sawa na rais wa muungano.

b). Wazanzibari wasishirika katika mchakato wa marekebishoa ya katiba katika mambo ya Tanzania bara kama vile Tanzania bara ilivyokuwa haikushirika katika mabadiliko ya katiba yao (mabadiliko ya kumi ya ktiba ya zanzibar ya 1984).

c). Katika uamuzi wa kupitisha katiba kilelezo "utaweka rehani " mustakbali wa mabadiliko hayo kwa vile iwapo Wazanzibari wakikataa na wabara wakikubali katiba hiyo haitapita, hivyo mchakato huu usiwekwe reheni na "siasa za Zanzibar".

MAWAZO YANGU:

Naamini Mhe. Tundu Lissu amefanya upotofu wa makusudi na anayefanya upotofu wa makusudi hawa amepotoka yy mwenyewe kwa vile:

a. Mhe. Lissu anajuwa kuwa muungano huu umeundwa kwa mkataba na siyo katiba na mkataba huo ndiyo unaotoa usawa wa mamlaka za nchi mbili kati ya Jamhuri ya watu wa zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika, katika yale mambo tuliyokualiana likiwamo la katiba ya Jamhuri ya Muungano.

b. Ushiriki wa Zanzibar katika mabadiliko ya katiba ya muungano siyo wa "hisani" bali haki yao na usawa walionao kwa mujibu wa makubaliano ya muungano na katiba hii hii mbovu, Mhe Lissu, kusema kuwa Zanzibar isihusike na mambo yasiyo kuwa ya muungano katika katiba hii ni kauli yakichekesho na aibu (nachelea kusema ya kipumbavu) kutoka kwa kinywa cha mwanasheria msomi aliyebobea. Mhe. Lissu anajuwa kuwa kinachofanyiwa marekebisho/mabadiliko hapa ni KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA SIYO YA TANGANYIKA?

Hapa alikuwa Mhe, Lissu, aje na hoja nyingine ya IPO WAPI KATIBA YA TANGANYIKA WAKATI ZANZIBAR WANAYO KATIBA YAO? ambayo itakuwa na mambo ya Tanganyika kama vile Zanzibar na Wazanzibari haitawahusu.

Ndiyo hapa wazanzibar wanapata na watapata uhalali wa kuikubali au kuikataa katiba ya JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, ambayo hatutakubali tena iingizwe mambo yasiyokuwa ya muungano, hivyo wala hatutakuwa na sababu ya kuyagusa.

c. Mhe. Lissu, anasema mambo kwa ujumla jumla, nani ataweka rehani hapa upitishwaji wa katiba hii? ni Wazanzibari au walioweka utaratibu huo kuwa katiba hiyo haitatumika mpaka ipate ridhaa ya pande mbili za muungano na kila upande kivyake! kwa akili ya Tundu Lissu watakao kataa ni wazanzibari tu,wakikataa Watanganyika je? si na wao watakuwa wameweka rehani mustakabali wa mabadiko haya kwa "siasa za Tanganyika?"

Hata hivyo, bado nakubaliana na maelezo mengine ya Mhe. Tundu Lissu kuwa mchakato huu uwape fursa watanzania waamuwe kama wanautaka muungano na wa aina gani?
Nakubaliana na wewe kabisa.

Hakika ugonjwa alionao Tundu Lissu ni sawa na ule wa WaTanganyika wengine kuogopa kutaja utaifa wao Kwa maana UTANGANYIKA na kuwa muwazi na kunena bayana pasi na khofu kuwa Kuwepo na Serikali ya Tanganyika ambayo ndanimwe itashughulikia mambo ya Tanganyika ambayo hayamo kwenye muungano kama ilivyo SMZ na kisha kuwepo na JMT.

Lakini haiwezekani na wala haingii akilini mambo ya JMT waZanzibar wasishiriki. Hii itakuwa ni kinyume kabisa cha katiba. Kwani hata muungano wenyewe pamoja na kuwa ni mkataba lakini vile vile ni BATILI

Kwani baada ya kufikiwa kwa Muungano mwaka 1964, Baraza la Kutunga Sheria la Zanzibar ambalo lilikuwa ni Baraza la Mapinduzi halikupewa nafasi ya kuridhia Muungano huo.

"Ni lazima Baraza la kutunga sheria la Zanzibar kwa sasa ambalo ni Baraza la Wawakilishi lipewe nafasi ya kuridhia mkataba huo ili kuupa uhalali wa kisheria kwa upande wa Zanzibar,"
 
Pancras Suday

Verified Member
Joined
Jun 24, 2011
Messages
7,772
Points
2,000

Pancras Suday

Verified Member
Joined Jun 24, 2011
7,772 2,000
Hakuna kulemba hapa na huo muungano wenu wa kinafiki ambao wazee waliokufa ndio waliouunda na wengine tumezaliwa tukaukuta tukiwauliza mantiki yake ni nini mnaleta majibu ya kibabaishaji, wazanzibar washasema hawautaki,vilevile na mimi nasema siutaki.<br />
Kama <br />
Tanganyika +Zanzibar=Tanzania<br />
then<br />
Tanzania-Tanganyika=Zanzibar<br />
why not<br />
Tanzania-Zanzibar=Tanzania<br />
Na sasa hivi wazenji wameenda kukaa kikao tuone watakuja na nini kwenye bunge la jioni
 
Mzee

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2011
Messages
13,464
Points
2,000

Mzee

JF-Expert Member
Joined Feb 2, 2011
13,464 2,000
Nadhani hamjamuelewa Mh. Lisu
Anamaanisha Zanzibar wajadili mambo yanayohusu muungano tu
Pia Rais wa Zanzibar ashirikishwe ktk maswala yanahusu muungano
 
Felixonfellix

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2010
Messages
1,670
Points
1,195

Felixonfellix

JF-Expert Member
Joined Feb 16, 2010
1,670 1,195
Kuna haja ya kukaa na kuelewa vyema dhima nzima ya hoja ya Lissu
Kuna mambo aliweka wazi kabisa
Naomba tu mwenye softcopy yote aidondoshe hapa ili ipipitiwe mstari kwa mstari na kisha tuijadili kama tulivyofanya kwa zingine badala ya kunyofoa vipengele vichache tu.

Tundu Antipas Mungwali Lissu, (Mb-Chadema) na msemaji wa kambi ya upinzani katika wizara ya katiba na sheria, jana akiwasilisha hotuba ya kambi ya upinzani ya wizara ya hiyo alisema kati ya mengi mambo ya upotofu, upotoshaji hivyo itahalis tukisema Tundu Lissu amepotoka.

Katika hotuba hiyo , wakati akitoa maelezo kuhusu mswada wa kuandaa utaratibu wa kutoa maoni ya mabadiliko ya katiba mpya ya JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, Mhe. Lissu alisema muswada huo bado una dosari hivyo kambi ya upinzani haikubaliani nao.

Kati ya dosari nyingi alizozitaja miongoni mwao ni uwepo au ushiriki wa Zanzibar kama mshiriki kamili wa mustakbai wa mabadiliko ya katiba hiyo. Mhe. Lissu alipotoka na kujipotosha aliposema:

a). kuwa mamlaka sawa aliyopewa rais wa Zanzibar na rais wa muungano hayakubaliki kwa kuwa yamefanywa "...kuwaonea huruma Wazanzibari baada ya kulalamika, kwa vile ilitosha rais wa zanzibar "...kuhusishwa tu.." na siyo kuwa na mamlaka sawa na rais wa muungano.

b). Wazanzibari wasishirika katika mchakato wa marekebishoa ya katiba katika mambo ya Tanzania bara kama vile Tanzania bara ilivyokuwa haikushirika katika mabadiliko ya katiba yao (mabadiliko ya kumi ya ktiba ya zanzibar ya 1984).

c). Katika uamuzi wa kupitisha katiba kilelezo "utaweka rehani " mustakbali wa mabadiliko hayo kwa vile iwapo Wazanzibari wakikataa na wabara wakikubali katiba hiyo haitapita, hivyo mchakato huu usiwekwe reheni na "siasa za Zanzibar".

MAWAZO YANGU:

Naamini Mhe. Tundu Lissu amefanya upotofu wa makusudi na anayefanya upotofu wa makusudi hawa amepotoka yy mwenyewe kwa vile:

a. Mhe. Lissu anajuwa kuwa muungano huu umeundwa kwa mkataba na siyo katiba na mkataba huo ndiyo unaotoa usawa wa mamlaka za nchi mbili kati ya Jamhuri ya watu wa zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika, katika yale mambo tuliyokualiana likiwamo la katiba ya Jamhuri ya Muungano.

b. Ushiriki wa Zanzibar katika mabadiliko ya katiba ya muungano siyo wa "hisani" bali haki yao na usawa walionao kwa mujibu wa makubaliano ya muungano na katiba hii hii mbovu, Mhe Lissu, kusema kuwa Zanzibar isihusike na mambo yasiyo kuwa ya muungano katika katiba hii ni kauli yakichekesho na aibu (nachelea kusema ya kipumbavu) kutoka kwa kinywa cha mwanasheria msomi aliyebobea. Mhe. Lissu anajuwa kuwa kinachofanyiwa marekebisho/mabadiliko hapa ni KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA SIYO YA TANGANYIKA?

Hapa alikuwa Mhe, Lissu, aje na hoja nyingine ya IPO WAPI KATIBA YA TANGANYIKA WAKATI ZANZIBAR WANAYO KATIBA YAO? ambayo itakuwa na mambo ya Tanganyika kama vile Zanzibar na Wazanzibari haitawahusu.

Ndiyo hapa wazanzibar wanapata na watapata uhalali wa kuikubali au kuikataa katiba ya JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, ambayo hatutakubali tena iingizwe mambo yasiyokuwa ya muungano, hivyo wala hatutakuwa na sababu ya kuyagusa.

c. Mhe. Lissu, anasema mambo kwa ujumla jumla, nani ataweka rehani hapa upitishwaji wa katiba hii? ni Wazanzibari au walioweka utaratibu huo kuwa katiba hiyo haitatumika mpaka ipate ridhaa ya pande mbili za muungano na kila upande kivyake! kwa akili ya Tundu Lissu watakao kataa ni wazanzibari tu,wakikataa Watanganyika je? si na wao watakuwa wameweka rehani mustakabali wa mabadiko haya kwa "siasa za Tanganyika?"

Hata hivyo, bado nakubaliana na maelezo mengine ya Mhe. Tundu Lissu kuwa mchakato huu uwape fursa watanzania waamuwe kama wanautaka muungano na wa aina gani?
 
FJM

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Messages
8,083
Points
1,225

FJM

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2011
8,083 1,225
Inawezekana lugha aliyotumia Mh. Lissu haijawafurahisha baadhi ya wabunge toka Zanzibar, lakini bado nashindwa kuelewa mantiki ya mbunge wa wa kwanza kuchangia leo (sikumbuki jina) kusema aliyosema. Maneno ya ajabu kabisa ya kumtukana Mh Lissu (personally). Kwa upande mwingine huyu mbunge wa Zanzibar bila kujijua anaweza kabisa akawa amewadhalilisha wanaume wa Zanzibar. Maneno kama Tundu 'Lussu' ni yanshusha hadhi ya wanaume wa Zanzibar pamoja na kwamba nia yake ilikuwa kumtukana Mh Lissu. Najua mchana huu wabunge toka Zanzibar wana kikao ni vizuri wajiangalie tena kwenye matumizi ya maneno kwa sababu nina hakina debate ya haya matusi ya leo bado haijaanza. Itazua zogo na ni fedheha kwa bunge kuruhusu lugha kama hiyo. Masikitiko!

NB: Mh. Lissu atoe ombi kwa maandishi kwa Spika au kamati ya uongozi ili Mheshiwa yule AFAFANUE kwa watanzania wote nini maana ya Tundu 'Lusu' maana amesema kule Zanzibar ina maana yake. Nadhani Watanzania wote tuna haki ya kujua nini maana ya maneno aliyotumia Mheshimiwa mbunge.
 
Forum statistics

Threads 1,356,563
Members 518,911
Posts 33,133,274
Top