Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,842
- 31,075
Baada ya kuisoma hiyo post ya Jerry Muro nilichogundua cha kwanza ni kuwa huyo jamaa lengo lake kwenye hilo bandiko lake ni kufanya personal attack kwa Tundu Lissu badala ya kujadili tukio la kuvamiwa hiyo kampuni ya mawakili wa IMMMA na kulipuliwa.
Hebu tuanze na hilo, Tundu Lissu alisoma taarifa hiyo akieleza wazi kuwa yale yalikuwa maamuzi ya BARAZA LA,UONGOZI LA TLS yaliyofanyika katika kikao chao kilichofanyika jana yake na yeye ameyasoma hayo maazimio ya kikao hicho akiwa ndiye Rais wa hiyo TLS.
Kwa mazingira hayo hapo tunaliona kosa LA kwanza la Jerry Muro la bandiko lake almost lote kumuattack Tundu Lissu as individual badala ya kulaumu BARAZA LA UONGOZI LA TLS!
Kosa LA pili ni kuwa yeye Jerry Muro amejikita zaidi katika kuhukumu kuwa maamuzi yaliyofanywa na Tundu Lissu na TLS "yake" ni maamuzi ya hovyo!
Kwanini nasema kuwa huo mtazamo wa Jerry kuwa haupo sahihi.
Iliyolipuliwa na bomu ni ofisi ya mawakili wa kampuni ya IMMMA na kutokana na tukio hilo LA kigaidi ni kuwa hao mawakili hawataweza kutekeleza shughuli zao kwa kipindi fulani kutokana na vitendea kazi vyao vingi kuwa "destroyed" na mabomu hayo yaliyolipuka.
Kwa maana hiyo naamini kwa kuzingatia kitu kinachoitwa SOLIDARITY, maamuzi ya TLS yako sahihi kwa kuwa yameonyesha MSHIKAMANO kwa tukio hilo la kinyama walilofanyiwa mawakili wenzao.
Tuje kwa upande wa waliotekeleza tukio hilo kuwa wamevalia sare za Polisi. Katika tamko lao TLS haijawahukumu moja kwa moja Jeshi la Polisi kuwa ndiyo waliotekekeza tukio hilo Bali imeomba uchunguzi wa haraka na wa kina ufanyike na vyombo vya usalama ili kuwabaini wale wote waliotekekeza tukio hilo LA kinyama ili waweze kuchukiliwa hatua za kisheria.
Kwa hiyo kwa msimamo huo sioni ni kwa vipi hatua hiyo ya TLS ichukuliwe kuwa imekaa kisiasa kwa mlengo wa Chama Fulani.
Pia nieleze sababu nyingine iliyofanya TLS waamue kuendesha huo mgomo wa siku 2 wa kutohudhuria proceedings zozote zitakazofanyika mahakamani siku hizo ingawa hata na wao wanajua kuwa itakuwa pia na madhara makubwa kwa wateja wao, lakini wakati mwingine kutokana na situation inayokukabili unalazimika kuchukua hatua ambayo ingawa kwa upande mwingine utakuwa na madhara lakini unalazimika kuchukua hatua hiyio ili kutoa shinikizo ili kufanyike hatua za haraka za tukio lililotokea.
Nimalizie pia kwa kueleza ni kwanini wananchi wamepunguza Imani kwa kiasi kikubwa kwa Jeshi LA Polisi kushughulikia matukio ya "design" hii ambayo yana dalili kuwa ni maelekezo toka juu....
Hebu tujiulize ni kwanini wale askari waliovamia kituo cha luninga cha Clouds wakiwa na silaha za moto wakiambatana na mtu mwenye wadhifa mkubwa jijini Dar na kutoa vitisho kwa watangazaji wa kituo hicho kuwa watu hao hawakuwahi kupandishwa kizimbani mahakamani kujibu tuhuma za kosa hilo la jinai?
Tujiulize pia swali la pili ni kwanini yule mtu aliyemtolea bastola Nape Nnauye mchana kweupe pale Protea Hotel na picha zikimtambulisha wazi kuwa yule ni nani, lakini hadi leo Jeshi letu la Polisi halikuwahi kumkamata MTU yule na kumfikisha mahakamani na kujibu tuhuma zake hizo za makosa ya jinai?
Nimalizie na suala la utekwaji wa msanii Roma Mkatoliki na kufanyiwa ukatili wa kutisha, ni kwanini Jeshi letu la Polisi hadi leo limeshindwa kuwakamata watu hao na kuwaburuza mahakamani kujibu tuhuma yao hiyo ya makosa ya jinai?
Ni dhahiri kwa experience ya hayo matukio niliyoyataja yaliyotokea kwenye jiji la Dar yanakuwa yanatia mashaka kuwa hata tukio hili la uvamizi wa kampuni ya mawakili wa IMMMA nalo linaelekea kuwa la "style" ile ile ya hayo matukio ya awali yaliyotokea kwenye jiji hilo.