Tundu Lissu, tunduni - na Jerry C. Muro

Tundu Lissu, tunduni - na Jerry C. Muro

Asante kwa kuwakumbusha.
Ila zaidi Asante kwa kuendelea kutujuza Lisu ni mtu wa aina gani.
Nasikitika kusema hakika hakufaa kuwa mwanasheria,
Why? He can't and he has never stand on his own words?
Shame at him.

Bado mengi yatajulikana kwakuwa siyo strategic.
 
hapo ndio naisikitikia sana Tz yetu,ushabiki,uroho wa cjui wa kuteuliwa au sijui ni nini, MTU HUYU KAANZA KWA KUTUELEZA TAALUMA YAKE NA KIWANGO CHAKE ATIKA TAALUMA HIYO,kinachonisikitisha zaidi ni mtaluma mbobezi anaanza kupotosha kabisa, kwa mfano, ukisoma taarifa ile sioni mahali ILIPOSEMA POLISI WALILIPUA ISIPOKUWA NAONA "INGAWA NI MAPEMA SANA KUJUA NANI KASHAMBULIA TUNAOMBA VYOMBO VYA USALAMA VIFANYE UCHUNGUZI KWA HARAKA" mwisho wa kunukuu. inasikitisha tuna maprofesional wanaacha kuzienzi taaluma zao wanaanza ushabiki ambao unawashushia kabisa hadhi zao. kuhusu kugoma kwa mawakili alichosema TL ni kwamba mawakili wenzao ambao wana kesi kama wao hawataweza kutekeleza majukumu yao kwa kipindi fulani, hivyo wanaona ili kuwaunga mkono na mawakili wenzao wasifike mahakamani kwa siku hizo mbili. lilikuwa jambo la msingi kujadili tukijikita kwenye ukweli kuliko kuzusha ya kwetu hatulisaidii taifa hili. vinginevyo sisi ni wabaya zaidi kuliko mafisadi na wala rushwa kwa sababu tunazusha mambo yasiyo ya kweli. WAJAMENI TUACHE USHABIKI TUIFIKIRIE ZAIDI MAMA TZ
 
Mimi mtu anayeandika maneno yasiyotakiwa kuandikwa kwa herufi kubwa kwa herufi kubwa, mara moja namtoa katika watu ninaoweza kuwasoma.

Anaonekana hajui kanuni za msingi kabisa za kuandika.

Sasa kama hajui kitu cha msingi kabisa kama kuandika, atakuwa na hoja gani ya muhimu mpya kwangu?

Kwangu mimi niliyemsoma Tacitus, Anaximander na Herodotus? Shakespeare na Shakespeare wa Shakespeare, Plutarch?

Gibbon na Dickens? Twain mpaka Fitzgerald na Steibeck? Aristotle mpaka Russell? Mandela, Nyerere mpaka Mbiti?

Popper mpaka Hegel? Heidegger mpaka Wittgenstein? Einstein mpaka Green? Dirac mpaka Hawking?

Gandhi mpaka Buddha? Ramanujan mpaka Chandrasekar?

Barzun mpaka Mnyampala? Soyinka mpaka Achebe? Murakami mpaka Miguna?

Nihangaike na uharo wa wazi kwa nini?
 
Tundu Lissu, TUNDUNI
Na Jerry C. Muro

Nianze kwa Kutoa pole kwa jumuiya nzima ya wanasheria nchini, pole yangu sio ya tukio la IMMA advocates, Bali pole yangu ni ya kuchagua Rais wa TLS Chama Chenu 'MAHIRI' cha wanasheria Tanganyika - TLS Ndugu Tundu Lissu ambae AMEDHIHIRISHA kuwa ameanza Rasmi Safari ya Kuizika TLS, kupitia taarifa yake kwa vyombo vya Habari kuhusiana na Tukio la IMMA advocates.
Nianze kwa kuweka msingi wa HOJA yangu kuwa sifurahishwi na kilichotokea kwenye IMMA advocates, ila pia SIFURAHISHWI zaidi na "AKILI NDOGO" za Rais wenu katika hatua za AWALI za kushughulikia suala hili.

Mimi ni Profesional communicator kama mwandishi wa Habari, na Nyinyi wanasheria ni Profesional kwenye Sheria, ukisoma na Kusikiliza kwa umakini TAARIFA ya Mhe Rais wa TLS utagundua makosa makubwa sana ya KIUFUNDI ambayo yanaifanya taarifa nzima kuwa kama taarifa ya Mfalme "****" na kwa sisi MAFUNDI wa taarifa tunasema taarifa ikikosewa katika UANDAAJI na UWASILISHWAJI inakuwa imekosa MASHIKO, na hivyo taarifa nzima kuwa BATILI.

KWANINI BATILI
1. Taarifa iliyowasilishwa na Rais wa TLS tayari kwa kiasi kikubwaa ilishatolewa na Chama cha wananchi CUF [HASHTAG]#teammaalim[/HASHTAG], ukisoma taarifa ya cuf ambayo ilitoka siku moja kabla ya hii ya Rais utaona nachosema, ila hii ya Rais imewaka mbwembwe ya Vifungu Vifungu vingi vya SHERIA tu, ila taarifa zote zimeonyesha kuwa IMMA advocate ni WABIA katika kazi mana cuf inatetewa na IMMA advocate na Rais Lissu anatetewa na IMMA advocate hivyo wote WANAOMBELEZA DHORUBA YA MMBIA WAO., japo TLS ni Chama na Lissu ni Rais, na ni mteja wa IMMA katika hoja hii ya kwanza nimalizie kwa kusema tu Hoi taarifa ni BATILI kwa kuwa Imekuwa taarifa ya KISIASA na Imetolewa na wanasiasa wa vyama viwili tofauti, japo Mmoja ni Rais wa TLS, hapa utaona sasa Hatari ya kuwa na Rais wa TLS ambae ni mwanasiasa.

2. Taarifa ni BATILI kwa kuwa imeanza kwanza kwa KUHUKUMU kuwa Ofisi za IMMA advocate zimepigwa BOMU na POLISI, japo hizi ni taarifa za AWALI lakini kwa maoni yangu TAARIFA haikupaswa kujielekeza kwenye kazi za mamlaka nyingine, mana kama mmeshajua waliolipua ni POLISI basi hamkuitaji kutoa taarifa Bali kufuata SHERIA kuwashtaki POLISI.
Katika hoja hii MWENDELEZO wake inasema wanavitaka vyombo husika wakiwemo "WATUHUMIWA" Polisi kufanya uchunguzi, mbele zaidi tena wanataka kukutana na "MTUHUMIWA" boss wao IGP, hivi hii ni SAWA WANASHERIA, mnataka kukutana kufanya nini tena na IGP au mkurugenzi wa usalama wa taifa ambae majuzi juzi hapa wakati wa Sakata la Bombadier Rais "WENU "alishema kuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa" ANAMFUATILIA FUATILIA "sasa iweje Leo aombe mwenyewe kukutana na" MTESI " wake, NDIO MANA NASEMA HAPA KUNA TATIZO YA HIKI CHAMA KUONGOZWA NA MWANASIASA, labda niwakumbushe tu hawa wanasiasa enzi ya Lowassa Walisema" mwizi" alipokwenda kwao wakamuita mfalme wa AMANI hawa ndio wana SIASA.

3. Taarifa ni BATILI, kwa sababu taarifa inataka WANASHERIA kugoma jumanne na jumatano, huu ni MGOMO ambao katika taarifa yao wanaomba ufanywe UCHUNGUZI, lakini pia kwenye taarifa yao wanaomba kuonana na kaimu Jaji Mkuu ambae mmekuja kusema tena hapo Chini ASUSIWE hamtaki kwenda kwenye mahakama anazoziongoza, JAMANI mnajua mnachofanya? Hii ni sawa na KUJITEKENYA MWENYEWE KISHA UKACHEKA MWENYEWE. nadhani Wasomi wana Sheria tukubaliane katika jambo moja MGOMO au KUONANA na "WATESI "wenu huwezi kushika mambo mawili kwa wakati Mmoja lazima MOJA litaponyoka.

4. Hii taarifa ni BATILI, kwa sababu imemtangaza MGOMO pasipo kusema ADUI ni Nani, hivi Hebu tuambieni mnagoma mkilenga KUMUUMIZA Nani? Kuwaumiza wateja wenu walioko MAGEREZANI au? Hivi nyinyi hii kazi ya UANASHERIA ni ya kujitolea katika kazi zenu zote? Hivi hakuna pesa mmechukua za wateja wenu ambazo mnapaswa kuzifanyia kazi, au TUSEME na nyinyi "WEZI" mnachukua hela za wateja wenu kisha mnagoma?
Hebu mtuambie Nani ADUI YENU basi.

MASWALI MAGUMU ZAIDI TLS.

1. Hivi Mbona walipouwawa *WANASHERIA* na *MAWAKILI* nguli nchini, tena waliowasomesha na kuwafundisha *HAMKUGOMA KUSHINIKIZA HAKI ITENDEKE KAMA HIVI LEO,* au mmesahau Vifo vya *"UTATA"* vya Mawakili Marehemu Kapinga, Marehemu Mvungi, Marehemu Mwaikusa? Kwa kuwa mnasahau ngoja tuwakumbushe tu *HAKUNA NAMNA*, Leo hao wazee wamekuwa *"LIABILITY"* kwenu halafu cuf, Lissu, acaccia zimekuwa *"ASSET"*kwenu?

2. Hivi tangu lini mmeanza kushirikiana press releases na vyama vya siasa mfano cuf?

3. Hivi TLS kimekuwa Chama cha Siasa, au kwakuwa Rais wenu ni mwanasiasa?

4. Mnawezaje kuitenganisha TLS na siasa?

5. Katika Sheria kuna neno linaitwa *"INNUENDO"*hivi mnajua maana ya hilo neno katika Sakata hili la IMMA advocate?

6. Hivi mnajua IMMA advocate ni kampuni "inayotajwa" KUCHOTA mabilioni ya fedha za EPA kupitia kampuni ya DEEP GREEN kiasi cha *BIlioni 8* zilichotwa, mnajua hilo? kama hamjui nendeni Brella kisha mkasome anuani za Kampuni ya *DEEP GREEN,* kisha mtangaze *MGOMO.*

7. Hivi mnajua huyu Rais wenu Lissu akiwa Bungeni mwaka 2012 Aliitaja kampuni ya IMMA advocate kuwa ilizitetea kampuni za TanGold na Deep green microfinances *KUCHOTA* pesa za EPA, halafu Leo HAWAHAWA imma advocate ndio wanaomtetea Lissu katika kesi zake?

Hivi mnajua maana ya vita ya *KIUCHUMI,* adui yako anaweza kutumia *MKEO, WATOTO* na hata Ndugu zako ili mradi *APATE USHINDI.*

Mwisho, Nawapenda sana *WANASHERIA,* mana najua mchango wao katika taifa la Tanzania, nawathamini sana Wanasheria wamaotanguliza *UZALENDO* kwa taifa Lao pamoja na changamoto tunazopitia kama taifa Changa, Nawapenda Wanasheria wanaosem *KWELI* kwa maslahi ya taifa Lao na Sio *MATUMBO* yao.

Sasa Sikilizeni, *AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO.LEO TUNDU, TUNDUNI.*

Wasalamu
*Jerry C. Muro*
*28/08 /2017*
Sasa Muro yaani wewe ndio unajiona unayo akili kuliko Lisu au mawakili waliokaa wakaamua hivyo. Wewe kwa akili yako. Ni watu gani wanaweza kwenda kwenye ofisi za Imma wakiwa na Magwanda za kipolisi kama sio jeshi lililotumwa na Bashite. Kwasababu operation zote chafu Bashite ndie anaesimamia. Umesahau issue yako ya matrafiki ulivyokuwa unalialia. Kama unataka cheo. Mfuate MAGUFULI ikulu umlambe miguu lkn sio kwa kuandika utumbo wako hapa. Kama unajua yote hayo nenda Takukuru. Umeanza kujipendekeza muda tu lkn MAGUFULI wala hajakupa hata ubalozi wa nyumba kumi
 
Mwandishi hujui hata Professional inaandikwaje? Zaidi ya mara moja imeandika Profesional!!!!! Au ndiyo wanaita mwandishi kanjanja!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi Muro, hujatukana mtu, umejenga hoja, nawo waje kwa kupanguwa hoja bila matusi..moja baada ya nyingine..Tunasubiri..
Kuna hoja gani hapo. Nikuulize Tundu Lisu ni nani TLS ni nini. Tamko limesomwa na nani?? Aliendaa tamko ni TLS AU LISU. mnapenda za kupewa kwa kujipendekeza pacpo kutumia akili
 
Asante kwa kuwakumbusha.
Ila zaidi Asante kwa kuendelea kutujuza Lisu ni mtu wa aina gani.
Nasikitika kusema hakika hakufaa kuwa mwanasheria,
Why? He can't and he has never stand on his own words?
Shame at him.

Bado mengi yatajulikana kwakuwa siyo strategic.
Hakufaa kuwa mwanasheria ila ni mwanasheria. Kweli ukiwa ccm na akili hulala
 
Kwa kumbukumbu zangu na kama sikosei,Jerry Muro hata uvamizi wa Bashite clouds aliutetea hadharani.

Si hivyo tu,hata Manji alipokamatwa kwa mara ya kwanza kuhusiana na tuhuma za kutumia dawa za kulevya alionekana kuunga mkono kukamatwa kwake pale alipohojiwa channel 10 katika kipindi cha Mada Moto.

Huyo ndio Jerry.

U-DC unatafutwa kuputia migongo ya watu.
Si anamuonea donge Gondwe
 
Jerry Muro ameshindwa kuitengenezea credibility taaluma yake... Kila anapoajiriwa lazima avurunde..

Huku anakogusa haelewi kitu. Anatafuta kiki kwa kila namna

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jerry Muro ndio yule alikamatwaga kwa kula rushwa ya 10mil. au ni mwingine? Na ambaye alikuwa msemaji wa Yanga akafukuzwa!!?
Ndio huyo Mkuu..
Mwandishi wa habari aliyekuwa anatembea na PINGU kama vile yeye ni polisi kutishia wale ambao alikuwa Anawalazimisha kumpa rushwa..
Leo kawa mpayukaji wa kukaripia TLS..
Maisha yanaenda kasi sana.
 
Daaaaah,mr muro Huu ujumbe ni mzito sanaaaa, Kwa nondo hizi mtu aksapot upuuz wa tundu and co' bhaaaas tena, atakua anawapangaji kichwan.. Jerry muro [HASHTAG]#greatthinker[/HASHTAG] haswaaa
 
..Muro nadhani ana tatizo na Tundu Lissu.

..statement ile ni ya Tanganyika Law Society na Tundu Lissu ni mjumbe tu.

..Jerry Muro anajitambulisha kama mtaalamu wa mawasiliano, lakini ameshindwa kuwasilisha hoja kulingana na viwango vya mwanataalum wa mawasiliano.

.."Professional communicator" hawezi kutoa taarifa huku akirusha vijembe "...TUNDU, TUNDUNI" au "AKILI NDONGO"

..muda wote wa andiko lake alikuwa amejificha, lakini mwisho ndiyo akafunua uhalisia wake kwa kumrushia kijembe Tundu Lissu.

..kwa hiyo utaona kabisa Jerry Muro yuko biased. Statement yake haikulenga kuwasaidia TLS bali kumshambulia Tundu Lissu.

..kosa lingine la Jerry Muro ni kuilaumu TLS kwa kutokugoma wakati wanachama wao maarufu walipouawa kutokana na mashambulizi ya kikatili. kwangu mimi hiyo siyo hoja. kama walikosea huko nyuma haimaanishi kwamba hawana uhalali wa kurekebisha makosa yao sasa hivi. Pia nyakati na mazingira ya matukio hutofautiana, na hivyo hati hatua wanazopendekeza TLS lazima zitatofautiana.

Bwana muro c nataka watu waendelee kufa na malaria kisa uko nyuma washakufa hata madakitari bingwa wa magonjwa tena kwa malaria ahaha just ahahaha
 
Tundu Lissu, TUNDUNI
Na Jerry C. Muro

Nianze kwa Kutoa pole kwa jumuiya nzima ya wanasheria nchini, pole yangu sio ya tukio la IMMA advocates, Bali pole yangu ni ya kuchagua Rais wa TLS Chama Chenu 'MAHIRI' cha wanasheria Tanganyika - TLS Ndugu Tundu Lissu ambae AMEDHIHIRISHA kuwa ameanza Rasmi Safari ya Kuizika TLS, kupitia taarifa yake kwa vyombo vya Habari kuhusiana na Tukio la IMMA advocates.
Nianze kwa kuweka msingi wa HOJA yangu kuwa sifurahishwi na kilichotokea kwenye IMMA advocates, ila pia SIFURAHISHWI zaidi na "AKILI NDOGO" za Rais wenu katika hatua za AWALI za kushughulikia suala hili.

Mimi ni Profesional communicator kama mwandishi wa Habari, na Nyinyi wanasheria ni Profesional kwenye Sheria, ukisoma na Kusikiliza kwa umakini TAARIFA ya Mhe Rais wa TLS utagundua makosa makubwa sana ya KIUFUNDI ambayo yanaifanya taarifa nzima kuwa kama taarifa ya Mfalme "****" na kwa sisi MAFUNDI wa taarifa tunasema taarifa ikikosewa katika UANDAAJI na UWASILISHWAJI inakuwa imekosa MASHIKO, na hivyo taarifa nzima kuwa BATILI.

KWANINI BATILI
1. Taarifa iliyowasilishwa na Rais wa TLS tayari kwa kiasi kikubwaa ilishatolewa na Chama cha wananchi CUF [HASHTAG]#teammaalim[/HASHTAG], ukisoma taarifa ya cuf ambayo ilitoka siku moja kabla ya hii ya Rais utaona nachosema, ila hii ya Rais imewaka mbwembwe ya Vifungu Vifungu vingi vya SHERIA tu, ila taarifa zote zimeonyesha kuwa IMMA advocate ni WABIA katika kazi mana cuf inatetewa na IMMA advocate na Rais Lissu anatetewa na IMMA advocate hivyo wote WANAOMBELEZA DHORUBA YA MMBIA WAO., japo TLS ni Chama na Lissu ni Rais, na ni mteja wa IMMA katika hoja hii ya kwanza nimalizie kwa kusema tu Hoi taarifa ni BATILI kwa kuwa Imekuwa taarifa ya KISIASA na Imetolewa na wanasiasa wa vyama viwili tofauti, japo Mmoja ni Rais wa TLS, hapa utaona sasa Hatari ya kuwa na Rais wa TLS ambae ni mwanasiasa.

2. Taarifa ni BATILI kwa kuwa imeanza kwanza kwa KUHUKUMU kuwa Ofisi za IMMA advocate zimepigwa BOMU na POLISI, japo hizi ni taarifa za AWALI lakini kwa maoni yangu TAARIFA haikupaswa kujielekeza kwenye kazi za mamlaka nyingine, mana kama mmeshajua waliolipua ni POLISI basi hamkuitaji kutoa taarifa Bali kufuata SHERIA kuwashtaki POLISI.
Katika hoja hii MWENDELEZO wake inasema wanavitaka vyombo husika wakiwemo "WATUHUMIWA" Polisi kufanya uchunguzi, mbele zaidi tena wanataka kukutana na "MTUHUMIWA" boss wao IGP, hivi hii ni SAWA WANASHERIA, mnataka kukutana kufanya nini tena na IGP au mkurugenzi wa usalama wa taifa ambae majuzi juzi hapa wakati wa Sakata la Bombadier Rais "WENU "alishema kuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa" ANAMFUATILIA FUATILIA "sasa iweje Leo aombe mwenyewe kukutana na" MTESI " wake, NDIO MANA NASEMA HAPA KUNA TATIZO YA HIKI CHAMA KUONGOZWA NA MWANASIASA, labda niwakumbushe tu hawa wanasiasa enzi ya Lowassa Walisema" mwizi" alipokwenda kwao wakamuita mfalme wa AMANI hawa ndio wana SIASA.

3. Taarifa ni BATILI, kwa sababu taarifa inataka WANASHERIA kugoma jumanne na jumatano, huu ni MGOMO ambao katika taarifa yao wanaomba ufanywe UCHUNGUZI, lakini pia kwenye taarifa yao wanaomba kuonana na kaimu Jaji Mkuu ambae mmekuja kusema tena hapo Chini ASUSIWE hamtaki kwenda kwenye mahakama anazoziongoza, JAMANI mnajua mnachofanya? Hii ni sawa na KUJITEKENYA MWENYEWE KISHA UKACHEKA MWENYEWE. nadhani Wasomi wana Sheria tukubaliane katika jambo moja MGOMO au KUONANA na "WATESI "wenu huwezi kushika mambo mawili kwa wakati Mmoja lazima MOJA litaponyoka.

4. Hii taarifa ni BATILI, kwa sababu imemtangaza MGOMO pasipo kusema ADUI ni Nani, hivi Hebu tuambieni mnagoma mkilenga KUMUUMIZA Nani? Kuwaumiza wateja wenu walioko MAGEREZANI au? Hivi nyinyi hii kazi ya UANASHERIA ni ya kujitolea katika kazi zenu zote? Hivi hakuna pesa mmechukua za wateja wenu ambazo mnapaswa kuzifanyia kazi, au TUSEME na nyinyi "WEZI" mnachukua hela za wateja wenu kisha mnagoma?
Hebu mtuambie Nani ADUI YENU basi.

MASWALI MAGUMU ZAIDI TLS.

1. Hivi Mbona walipouwawa *WANASHERIA* na *MAWAKILI* nguli nchini, tena waliowasomesha na kuwafundisha *HAMKUGOMA KUSHINIKIZA HAKI ITENDEKE KAMA HIVI LEO,* au mmesahau Vifo vya *"UTATA"* vya Mawakili Marehemu Kapinga, Marehemu Mvungi, Marehemu Mwaikusa? Kwa kuwa mnasahau ngoja tuwakumbushe tu *HAKUNA NAMNA*, Leo hao wazee wamekuwa *"LIABILITY"* kwenu halafu cuf, Lissu, acaccia zimekuwa *"ASSET"*kwenu?

2. Hivi tangu lini mmeanza kushirikiana press releases na vyama vya siasa mfano cuf?

3. Hivi TLS kimekuwa Chama cha Siasa, au kwakuwa Rais wenu ni mwanasiasa?

4. Mnawezaje kuitenganisha TLS na siasa?

5. Katika Sheria kuna neno linaitwa *"INNUENDO"*hivi mnajua maana ya hilo neno katika Sakata hili la IMMA advocate?

6. Hivi mnajua IMMA advocate ni kampuni "inayotajwa" KUCHOTA mabilioni ya fedha za EPA kupitia kampuni ya DEEP GREEN kiasi cha *BIlioni 8* zilichotwa, mnajua hilo? kama hamjui nendeni Brella kisha mkasome anuani za Kampuni ya *DEEP GREEN,* kisha mtangaze *MGOMO.*

7. Hivi mnajua huyu Rais wenu Lissu akiwa Bungeni mwaka 2012 Aliitaja kampuni ya IMMA advocate kuwa ilizitetea kampuni za TanGold na Deep green microfinances *KUCHOTA* pesa za EPA, halafu Leo HAWAHAWA imma advocate ndio wanaomtetea Lissu katika kesi zake?

Hivi mnajua maana ya vita ya *KIUCHUMI,* adui yako anaweza kutumia *MKEO, WATOTO* na hata Ndugu zako ili mradi *APATE USHINDI.*

Mwisho, Nawapenda sana *WANASHERIA,* mana najua mchango wao katika taifa la Tanzania, nawathamini sana Wanasheria wamaotanguliza *UZALENDO* kwa taifa Lao pamoja na changamoto tunazopitia kama taifa Changa, Nawapenda Wanasheria wanaosem *KWELI* kwa maslahi ya taifa Lao na Sio *MATUMBO* yao.

Sasa Sikilizeni, *AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO.LEO TUNDU, TUNDUNI.*

Wasalamu
*Jerry C. Muro*
*28/08 /2017*

Kwa hivyo lisu anakosa kuitetea IMMMA kwa sabau tu deepgreen walichota hela au 2012 aliisema bungeni, we ni mwaandishi habari I hope ni baada ya kupata zero form four ulikimbilia uandishi, mtu akikosea lazma asemwe na akikosewa lazma asemewe pia
 
Tuangalie tukio lenyewe na upana wa athari zake. Uvamizi wa mabomu/mass killing ni mfumo unaotumiwa na ma terrorist. Hapa kwetu Tanganyika, tunakumbuka ubalozi wa marekani ulivyoshambuliwa kwa mabomu na tuliona jinsi serikali ilivyolishughulikia suala lile. Mh Muro, naomba utuambie kwanini serikali hasa waziri wa sheria au mambo ya ndani wameshindwa kutoa tamko lolote?
Umemwita "mh"? Aisee! Kwa lipi hasa? Huyo Muro ni muongo anayejipendekeza tu. Hana lolote. Anajikakamua ili afanane na watu ila ndiyo hivyo tena. Kesi yake ile ya kujidai mwanausalama na kuomba rushwa akiwa na matapeli wenzie ilifikia wapi?
 
Jerry Muro anashindwa kuelewa kuwa TLS ni taasisi na TL ni mtu binafsi. Msimamo uliotolewa juzi ni msimamo wa taasisi ambayo ina uongozi ambao sio TL peke yake. Maana yake kuna baraza la uongozi linalojumuisha watu kadhaa. Lakini ktk kuwasilisha maamuzi hayo kwa press lazima yasemwe na mtu mmoja ambaye anatoka kwenye baraza la uongozi au msemaji wao mkuu kama yupo na sio lazima TL. Tatizo ninaloliona hapa kwa huyu TOM & JERRY ni kwamba kwa nn TL. Acha kumuonea wivu mwenzako, ya kwako yamekushinda unatafuta kutokea kupitia kwa TL?
 
Back
Top Bottom