Tundu Lissu: Prof. Kabudi ni bingwa wa kuchapia, hasa kwa watu wasiomuelewa au walio wavivu wa kusoma au wenye uelewa wa juu juu

Hawa ndo wasomi tunao wahitaji katika taifa, watu walio na uwezo wa kujenga hoja na kuchambua na hatimae kutoa taarifa sahihi ambayo italinufaisha taifa sio tu kwa elimu lakini pia kwa hasara zisizokuwa na kichwa wala miguu, lakini katika nchi yetu inatokea watu fulani kwa maslahi yao wenyewe wanataka kuwaangamiza na Mungu nae ana makusudi yake bado wapo kwa mara nyingine tunashudia usomi sio kuwa na vyeti vingi vya udoctor au uprofesor bali uelewa
 
Nimeona clip ya Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Pala Kabudi akitoa 'lecture' bungeni juu ya masuala mbali mbali ya kisheria na kikatiba.

Clip hiyo imeanzia katikati, kwa hiyo ni vigumu kwangu kufahamu hoja ya msingi iliyomfanya azungumze alichozungumza. Hata hivyo, nimevutiwa na alichokisema juu ya mamlaka ya Rais ya kutunga sheria. Ndicho ninachotaka kukizungumzia kwa ufupi hapa.

Kabla sijafanya hivyo niseme tu kwamba Prof. Kabudi ni bingwa wa kuchapia, hasa kwa watu wasiomuelewa au walio wavivu wa kusoma au wenye uelewa wa juu juu, hasa wa masuala ya kikatiba na kisheria. Naomba hoja yake juu ya mamlaka ya Rais ya kutunga sheria kama mfano.

Prof. Kabudi amedai Rais ana mamlaka ya kutunga sheria kwa kutumia decrees, instruments na proclamations. Hajafafanua matumizi ya hizo decrees, instruments na proclamations. Kwa kumsikiliza tu, mtu asiyejua mambo haya anaweza kufikiria, kimakosa, kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano ana mamlaka ya kutunga sheria juu ya jambo lolote, wakati wowote kwa kutumia hizo njia tatu. Ukweli ni kwamba mamlaka ya Rais ya kutumia instruments na proclamations yanahusu mambo mahsusi ambayo yametajwa kwenye Katiba. Instrument (waraka) au proclamation (tangazo) ni njia au namna tu anayotumia kutekeleza mamlaka yake. Katiba yenyewe ndio inayofafanua mamlaka gani yatekelezwe kwa kutumia instrument na yapi yatekelezwe kwa kutumia proclamation.

Kwa mfano, Rais ana mamlaka ya kutangaza hali ya hatari kwa mujibu wa Katiba. Sasa Rais anatekeleza mamlaka hayo kwa kupitia tangazo (proclamation) ya hali ya hatari.

Tangazo hilo sio source ya mamlaka yenyewe, source ni Katiba na Sheria ya Ukasimishaji wa Mamlaka ya Uwaziri. Proclamation ni ushahidi tu kwamba Rais ametumia mamlaka yake ya kikatiba.

Mfano mwingine. Rais ana mamlaka kikatiba ya kuunda au kuvunja ofisi za umma, i.e. Wizara, n.k. Katiba yenyewe imeelekeza kwamba Rais atatumia instrument (waraka) pale anapounda Wizara, kufafanua majukumu yake, etc.

Maana ya kusema hivi ni kwamba kama Katiba haijasema kwamba Rais atatumia utaratibu fulani katika kutekeleza jukumu lake fulani kikatiba, yeye hawezi kujiamulia kutumia utaratibu wa instrument au proclamation katika kulitekeleza jukumu hilo.

Kwa mfano, Rais hateui Majaji au Mawaziri au Wakuu wa Wilaya au Mkoa au Makatibu Wakuu wa Wizara au watendaji wa taasisi mbali mbali za umma kwa kutumia instruments au proclamations.

Kwa upande mwingine, Rais hana mamlaka kabisa, kwa Katiba ya sasa, ya kutunga sheria kwa kutumia decrees. Decrees (amri) ni Sheria zinazotungwa pale ambapo hakuna Bunge la kawaida kwa sababu yoyote ile. Mfano mzuri ni tawala za kijeshi au za kimapinduzi kama ilivyokuwa Zanzibar kati ya miaka ya '64 na '79.

Sasa ilikuwaje Mwalimu Nyerere akatunga Sheria mbili kwa kutumia decree mwaka '64??? Jibu ni Mapinduzi ya Zanzibar ya Jan. '64, na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa Aprili ya mwaka huo huo.

Kwa sababu ya Mapinduzi, Bunge la kawaida la Zanzibar lilivunjwa na badala yake Baraza la Mapinduzi likajipa madaraka ya kutunga sheria kwa kutumia decrees.

Na mara baada ya Muungano kuzaliwa, hakukuwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya kutunga sheria zinazohusu masuala ya Muungano.

Hivyo Mwalimu Nyerere alipewa mamlaka hayo kwenye Hati ya Makubaliano ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ili kumwezesha kutunga sheria zinazohusu masuala ya Muungano wakati wa kipindi cha mpito mara tu baada ya Muungano.

Mamlaka hayo yalifikia mwisho wake mwaka '65 ilipotungwa Katiba ya Mpito ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tangu wakati huo Rais hana tena mamlaka ya kutunga sheria kwa amri (decrees).

Mwisho, ni muhimu kuelewa kwamba mamlaka ya Rais ya kutumia instruments na proclamations yanahusu tu mambo yaliyotajwa kwenye Katiba. Nje ya mambo hayo, Rais hana mamlaka anayoyazungumzia Profesa Kabudi.

Tatizo wewe ndiye unayejua kila kitu na kumkosoa kila mtu.unataka kila mtu akuamini kuwa wewe unajua zaidi.

Kumbuka wapo watu wanaojua pia wako kimya.kuwa ujuzi wako unapotosha watu wasiojua.
Pona salama...uendelee kuwa aminisha wachache juu ya ujuzi wako.
 
Tatizo wewe ndiye unayejua kila kitu na kumkosoa kila mtu.unataka kila mtu akuamini kuwa wewe unajua zaidi.

Kumbuka wapo watu wanaojua pia wako kimya.kuwa ujuzi wako unapotosha watu wasiojua.
Pona salama...uendelee kuwa aminisha wachache juu ya ujuzi wako.
Katetemeke Kagera we mhaya! Bado tu!
 
Asante lissu nilishaingizwa chaka na huyu kanjanja kabudi sijui kwann mh kabudi anataka kujivunjia heshima aliyojijengea kwenye bunge la katiba sasa hv anatumia nguvu kubwa kujivunjia heshima anaiporomosha kwa kasi ya dream liner
 
Yericko Nyerere gombea uenyekiti wa Chadema .

Huyu Lisu kumbe nae hafai tu anaropoka mno.
 
Mheshimiwa Lissu, siyo kila jambo linalosemwa na waziri wa sheria siku hizi lazima ulijadiri, subir upone mjadiliane naye pale bungeni.
Kama wewe unaona hayakuhusu kalale, nyie green guard hata nchi ikiendeshwa kinyume cha katiba mko salama maana mmehakikishiwa kulindwa kwa mema na maovu mtakayotenda. Kaa kimya unapoona yanayojadiliwa yamekuzidi uelewa.
 
Back
Top Bottom