Tundu Lissu: Paper Tigers wanatushauri tususie chaguzi zijazo ili CCM wapite bila kupingwa

Weupe sana sema wanategemea polis na kitu kingine walishajipanga haya na wana jua hakuna cha kuwatisha kumbuka pale mwanzo uhakiki wa silaha ulifanywa nchi nzima wee unafikiri ilikuwa lengo gani kufanya vile
Watapunguza idadi ya majimbo yaendane na idadi ya policcm, Kwa sasa kuyathibiti yote policcm hawatoshi.Na wananchi hawatokubali kuchaguliwa viongozi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukisoma sayansi huwezi kutanana na Lenin, mwanamutapa kingdom, French revolution, Ottoman empire, rise and fall of kingdom, freedom fighter, peoples power,nk hio ni misamiati sawa na chloroquine,ukisoma kemia utaishia kuchanga watu kama tunavochanganya madawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuelewe mazingira yetu, tujielewe sisi wenyewe na tuwe na nidhamu ndani na nje ya Chama.

Asante raisi wa Tz 2020
 
Unapotaka jumuiya ya kimataifa ione yafanyikayo ktk nchi yako dhidi ya chama tawala ukidai wanaminya demokrasia, jumuiya ya kimataifa wanaangalia kila neno lako, unapowaita hao chama tawala MACCM, watajua nawe kuna kitu hakiko sawa na hna substance ktk hoja zako bali chuki binafsi.
 
Naomba na mimi kuchangia mjadala huu kidogo. Na mapema kabisa niwaombe radhi wote nitakaowakwaza, kwa sababu nafikiri nitakachosema kitawakwaza wengi humu.

Nimefuatilia mjadala wa yaliyojiri Korogwe Vijijini na nikiri nimeshuhudia utoto wa kisiasa wa kutisha na kusikitisha sana. Nimeona kile ambacho Lenin alikiita 'an infantile disorder' miaka mia moja iliyopita. Naomba kufafanua.

Sheria ya Uchaguzi na Kanuni zake zinaelekeza kwamba mgombea anatakiwa kuwasilisha fomu za uteuzi kabla ya saa kumi ya siku moja kabla ya siku ya uteuzi.

Sheria inasema fomu za uteuzi zitakabidhiwa kwa Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo. Maadili ya Uchaguzi yameelekeza wazi kwamba Msimamizi wa Uchaguzi anatakiwa awepo ofisini kwake wakati wote anaotakiwa ili kupokea fomu za uteuzi za wagombea.

Kwa hiyo, kitu cha kwanza cha kujiuliza ni je, mgombea wetu alipeleka fomu zake za uteuzi kwa wakati uliowekwa kisheria au hakufanya hivyo???

Kama alifanya hivyo, je, kwa nini fomu zake hazikupokelewa??? Kama hakufanya hivyo ni kwa nini na lawama iangukie wapi???

Baada ya kupata jibu la swali la kwanza, swali la pili ni je, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo alikuwepo ofisini kwake kwa wakati wote aliotakiwa kuwepo ili kupokea fomu za uteuzi za wagombea???

Kama alikuwepo je, alipokea fomu za uteuzi za wagombea kama inavyotakiwa na Sheria??? Kama hakuwepo, je, ni kwa nini na lawama iangukie wapi???

Kwa ninayoyasoma mitandaoni, mgombea wetu alipeleka fomu zake za uteuzi kwa wakati muafaka. Na wala hakuwa peke yake, walikuwepo wagombea wa CCM na ACT-Wazalendo.

Kwa ninayoyasoma mitandaoni, wagombea walipofika ofisini kwa Msimamizi wa Uchaguzi wakakuta hayupo ofisini kwake wakati aliotakiwa kuwepo. Inasemekana alikuwa ameitwa kwa Mkuu wa Wilaya.

Fomu za mgombea wetu na wa ACT-Wazalendo hazikupokelewa lakini, somehow, fomu za mgombea wa CCM zikabandikwa ukutani na mara akatangazwa kuwa amepita bila kupingwa!!!!

Je, aliyekosea hapa ni nani??? Je, ni mgombea aliyepeleka fomu zake za uteuzi kwa wakati??? Je, ni Katibu wa Wilaya ya Korogwe Vijijini au wa Mkoa wa Tanga??? Au Katibu wa Kanda ya Kaskazini huko Arusha??? Au Katibu Mkuu na maafisa wake Dar Es Salaam??? Au Mwenyekiti wa Chama ambaye yuko kortini Kisutu kila siku???

Jibu la baadhi ya 'Marafiki wa BAVICHA Original' humu ndani ni kwamba viongozi wetu, hasa wa juu, ndio waliosababisha yote haya!!! Sio Msimamizi wa Uchaguzi aliyekimbia ofisi wakati anaotakiwa awepo ili kupokea fomu za uteuzi.

Sio Magufuli aliyejaza makada wa CCM walioshindwa uchaguzi uliopita kama Wakurugenzi wa Halmashauri na, kwa hiyo, kuwafanya wasimamizi wa uchaguzi.

Sio mapolisi waliotumwa kwenda kuwatawanya wagombea ambao fomu zao za uteuzi hazikupokelewa.

Wale waliopewa jukumu la kupokea fomu za uteuzi za wagombea wote na Sheria za nchi yetu; na Bosi wao aliyewakataza hadharani kutenda haki, hao hawana lawama.

Wahalifu halisi hawana makosa; waliofanyiwa uhalifu ndio wanaolaumiwa na hawa wanaojiita wanaCHADEMA au marafiki wa BAVICHA Original.

Halafu tukisema kuna watu wanamtumikia shetani kwa kuelewa au kutokujielewa, people take offence.

Halafu 'Marafiki' hawa wanaleta vihoja kwamba haya yanatokea kwa sababu ya Katibu Mkuu wa sasa; hayakuwa yanatokea wakati Dr. Slaa akiwa Katibu Mkuu, etc.

Wenye hoja za aina hii wanafikiria wanajua, ni werevu, wasomi, n.k. Ni wajinga wasiojua wasemalo.

Kabla hamjasema sana muwe mnawauliza akina Tony Komu na Joe Selasini na James Mbatia na wengineo ambao wameshiriki hizi vita tangu kabla ya kuingia mfumo wa vyama vingi vya siasa.

Au sisi wengine, mimi mmojawapo, ambao tumeshiriki kwenye uchaguzi tangu mwaka '95. Haya ya sasa sio mapya sana.

Hii habari ya wasimamizi wa uchaguzi kukimbia ofisi zao ili wasipokee fomu za uteuzi za wagombea wa upinzani haikuanza Korogwe Vijijini. Ilikuwepo tangu mwaka '95 wakati wa Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi.

Wagombea wetu kuwekewa mapingamizi ya ajabu ajabu na kuenguliwa kiharamia na maCCM kupitishwa bila kupingwa haikuanza na Magufuli na watu wake. Ilianza Ali Hassan Mwinyi akiwa Rais na Ben Mkapa mgombea Urais.

Wagombea wa CCM kutangazwa kwa nguvu haikuanza na Magufuli. Ilianza Mkapa akiwa Rais na baadae ikarithiwa na Kikwete na imepokelewa na Magufuli. Kumbukeni ya marehemu Shelembi wetu Shinyanga Mjini mwaka '10 na ya David Kafulila mwaka '95 wakati Rais akiwa Kikwete.

Kuna wakati maCCM, wakisaidiwa na mapolisi kama ilivyo sasa, walikuwa wanateka magari ya Tume yenye masanduku ya kura halali na kuyabadilisha na masanduku yenye kura haramu kwa lengo la kuwashindisha wagombea wa CCM.

Wagombea au wabunge wetu kujiuza kama malaya kwa maCCM haikuanza na akina Waitara na ole Kalanga. Tuliwahi kuwa na wabunge kama Makongoro Nyerere na Dr. Masumbuko Lamwai na Danhi Makanga na Daniel Nsanzugwanko huyu huyu wa CCM ya sasa. Nani anayewakumbuka tena???

Tuliwahi kuwa na wanamageuzi maarufu kama Prince Bagenda na Chief Abdallah Fundikira na wengineo wengi walioishia kujiuza CCM.

Licha ya haya yote, hatukuwahi kufikiria kuacha kushiriki kwenye chaguzi za marudio au Uchaguzi Mkuu.

Tulijua uchaguzi ni vita, na vitani kuna kushinda au kushindwa; kuna kufa au kujeruhiwa au kutekwa, na kuna kuua au kujeruhi au kuteka.

Hawa 'Marafiki' waliokuja jana na leo asubuhi wameshuhudia tukipigwa na Magufuli na watu wake wa CCM ya sasa na tayari wanatushauri tunyanyue mikono juu na kusalimu amri mbele ya watesi wetu.

Wanatushauri tususie chaguzi zijazo ili maCCM yapite bila kupingwa kwenye nafasi zote nchi nzima. Wanatumia maneno makali yenye kuonyesha wana msimamo mkali na ujasiri ambao hatujawahi kuona wakiuonyesha kwa vitendo mahali popote.

These are all Paper Tigers, chui wa makaratasi aliowasema Mwenyekiti Mao Zedong. Tukiwasikiliza imekula kwetu na maCCM watachekelea all the way to the bank.

Tufanyeje???

Niliizungumzia hii wiki iliyopita na sina haja ya kuirudia hapa. Tujielewe na tuelewe hali yetu ya sasa relative to hali ya jana na ya juzi.

Tunaelewa hali yetu ya sasa kwa sababu kila mmoja wetu anaona yanayotendeka. Hata hivyo, uelewa wetu wa sasa hautoshi kututabiria kesho yetu.

Ili tuelewe kesho yetu itakuwaje, ni lazima tuelewe jana na juzi yetu ilikuwaje. There's no telling the future without knowing the past and understanding the present.

Tusikubali ujasiri feki na ushauri wa sumu wa hawa wanaojiita 'Marafiki' zetu. Tusikubali kutengenezewa ugomvi wa bure baina yetu na viongozi wetu na hawa wanaojifanya wana uchungu na Chama.

Tusikubali kupotezewa focus kwa kuaminishwa kuwa adui ni Mbowe au Mashinji au Mnyika; wakati adui halisi ni yule aliyemuua Mawazo na kumpoteza Ben Saanane au kumjeruhi Tundu Lissu.

Tuelewe mazingira yetu, tujielewe sisi wenyewe na tuwe na nidhamu ndani na nje ya Chama.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Tundu Lissu umeongea kwa hasira zenye ukweli ndani yake ila umesahau jambo moja kwamba;
"...a small minorty consisting members of Economic Elites and Policy Planning Networks are the one who hold most POWER no matter what happens in ELECTIONS..." (Elite theory)
 
Hao unaosema MACCM ndio viongozi wetu,sidhani kama unaweza kutoa kejeli kwa wakoloni na mabepari ambao hushirikiana kuuibia nchi yetu kwa mikataba yetu mibovu! Acha dharau kwa viongozi!
 
Ajabu kwa kweli mtu aliyepo kwenye matibabu nje ya nchi eti ndio anona anaujua ukweli kuliko waliokuwepo eneo la tukio. Halafu hii mindset ya kuona Chadema haikoseagi hata siku moja ndio inayowamaliza kila siku.

Ww lazima utakuwa ni mzee, hii ni dunia ya utandawazi, habari zinafika kote duniani kirahisi. Juzi kombe la dunia limefanyikia Russia, watu wako hapa nchini wanachambua matukio ya huko kama walikuwa Russia. Kipi kitashindikana kwenye hayo ya Korogwe?
 
Naomba na mimi kuchangia mjadala huu kidogo. Na mapema kabisa niwaombe radhi wote nitakaowakwaza, kwa sababu nafikiri nitakachosema kitawakwaza wengi humu.

Nimefuatilia mjadala wa yaliyojiri Korogwe Vijijini na nikiri nimeshuhudia utoto wa kisiasa wa kutisha na kusikitisha sana. Nimeona kile ambacho Lenin alikiita 'an infantile disorder' miaka mia moja iliyopita. Naomba kufafanua.

Sheria ya Uchaguzi na Kanuni zake zinaelekeza kwamba mgombea anatakiwa kuwasilisha fomu za uteuzi kabla ya saa kumi ya siku moja kabla ya siku ya uteuzi.

Sheria inasema fomu za uteuzi zitakabidhiwa kwa Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo. Maadili ya Uchaguzi yameelekeza wazi kwamba Msimamizi wa Uchaguzi anatakiwa awepo ofisini kwake wakati wote anaotakiwa ili kupokea fomu za uteuzi za wagombea.

Kwa hiyo, kitu cha kwanza cha kujiuliza ni je, mgombea wetu alipeleka fomu zake za uteuzi kwa wakati uliowekwa kisheria au hakufanya hivyo???

Kama alifanya hivyo, je, kwa nini fomu zake hazikupokelewa??? Kama hakufanya hivyo ni kwa nini na lawama iangukie wapi???

Baada ya kupata jibu la swali la kwanza, swali la pili ni je, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo alikuwepo ofisini kwake kwa wakati wote aliotakiwa kuwepo ili kupokea fomu za uteuzi za wagombea???

Kama alikuwepo je, alipokea fomu za uteuzi za wagombea kama inavyotakiwa na Sheria??? Kama hakuwepo, je, ni kwa nini na lawama iangukie wapi???

Kwa ninayoyasoma mitandaoni, mgombea wetu alipeleka fomu zake za uteuzi kwa wakati muafaka. Na wala hakuwa peke yake, walikuwepo wagombea wa CCM na ACT-Wazalendo.

Kwa ninayoyasoma mitandaoni, wagombea walipofika ofisini kwa Msimamizi wa Uchaguzi wakakuta hayupo ofisini kwake wakati aliotakiwa kuwepo. Inasemekana alikuwa ameitwa kwa Mkuu wa Wilaya.

Fomu za mgombea wetu na wa ACT-Wazalendo hazikupokelewa lakini, somehow, fomu za mgombea wa CCM zikabandikwa ukutani na mara akatangazwa kuwa amepita bila kupingwa!!!!

Je, aliyekosea hapa ni nani??? Je, ni mgombea aliyepeleka fomu zake za uteuzi kwa wakati??? Je, ni Katibu wa Wilaya ya Korogwe Vijijini au wa Mkoa wa Tanga??? Au Katibu wa Kanda ya Kaskazini huko Arusha??? Au Katibu Mkuu na maafisa wake Dar Es Salaam??? Au Mwenyekiti wa Chama ambaye yuko kortini Kisutu kila siku???

Jibu la baadhi ya 'Marafiki wa BAVICHA Original' humu ndani ni kwamba viongozi wetu, hasa wa juu, ndio waliosababisha yote haya!!! Sio Msimamizi wa Uchaguzi aliyekimbia ofisi wakati anaotakiwa awepo ili kupokea fomu za uteuzi.

Sio Magufuli aliyejaza makada wa CCM walioshindwa uchaguzi uliopita kama Wakurugenzi wa Halmashauri na, kwa hiyo, kuwafanya wasimamizi wa uchaguzi.

Sio mapolisi waliotumwa kwenda kuwatawanya wagombea ambao fomu zao za uteuzi hazikupokelewa.

Wale waliopewa jukumu la kupokea fomu za uteuzi za wagombea wote na Sheria za nchi yetu; na Bosi wao aliyewakataza hadharani kutenda haki, hao hawana lawama.

Wahalifu halisi hawana makosa; waliofanyiwa uhalifu ndio wanaolaumiwa na hawa wanaojiita wanaCHADEMA au marafiki wa BAVICHA Original.

Halafu tukisema kuna watu wanamtumikia shetani kwa kuelewa au kutokujielewa, people take offence.

Halafu 'Marafiki' hawa wanaleta vihoja kwamba haya yanatokea kwa sababu ya Katibu Mkuu wa sasa; hayakuwa yanatokea wakati Dr. Slaa akiwa Katibu Mkuu, etc.

Wenye hoja za aina hii wanafikiria wanajua, ni werevu, wasomi, n.k. Ni wajinga wasiojua wasemalo.

Kabla hamjasema sana muwe mnawauliza akina Tony Komu na Joe Selasini na James Mbatia na wengineo ambao wameshiriki hizi vita tangu kabla ya kuingia mfumo wa vyama vingi vya siasa.

Au sisi wengine, mimi mmojawapo, ambao tumeshiriki kwenye uchaguzi tangu mwaka '95. Haya ya sasa sio mapya sana.

Hii habari ya wasimamizi wa uchaguzi kukimbia ofisi zao ili wasipokee fomu za uteuzi za wagombea wa upinzani haikuanza Korogwe Vijijini. Ilikuwepo tangu mwaka '95 wakati wa Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi.

Wagombea wetu kuwekewa mapingamizi ya ajabu ajabu na kuenguliwa kiharamia na maCCM kupitishwa bila kupingwa haikuanza na Magufuli na watu wake. Ilianza Ali Hassan Mwinyi akiwa Rais na Ben Mkapa mgombea Urais.

Wagombea wa CCM kutangazwa kwa nguvu haikuanza na Magufuli. Ilianza Mkapa akiwa Rais na baadae ikarithiwa na Kikwete na imepokelewa na Magufuli. Kumbukeni ya marehemu Shelembi wetu Shinyanga Mjini mwaka '10 na ya David Kafulila mwaka '95 wakati Rais akiwa Kikwete.

Kuna wakati maCCM, wakisaidiwa na mapolisi kama ilivyo sasa, walikuwa wanateka magari ya Tume yenye masanduku ya kura halali na kuyabadilisha na masanduku yenye kura haramu kwa lengo la kuwashindisha wagombea wa CCM.

Wagombea au wabunge wetu kujiuza kama malaya kwa maCCM haikuanza na akina Waitara na ole Kalanga. Tuliwahi kuwa na wabunge kama Makongoro Nyerere na Dr. Masumbuko Lamwai na Danhi Makanga na Daniel Nsanzugwanko huyu huyu wa CCM ya sasa. Nani anayewakumbuka tena???

Tuliwahi kuwa na wanamageuzi maarufu kama Prince Bagenda na Chief Abdallah Fundikira na wengineo wengi walioishia kujiuza CCM.

Licha ya haya yote, hatukuwahi kufikiria kuacha kushiriki kwenye chaguzi za marudio au Uchaguzi Mkuu.

Tulijua uchaguzi ni vita, na vitani kuna kushinda au kushindwa; kuna kufa au kujeruhiwa au kutekwa, na kuna kuua au kujeruhi au kuteka.

Hawa 'Marafiki' waliokuja jana na leo asubuhi wameshuhudia tukipigwa na Magufuli na watu wake wa CCM ya sasa na tayari wanatushauri tunyanyue mikono juu na kusalimu amri mbele ya watesi wetu.

Wanatushauri tususie chaguzi zijazo ili maCCM yapite bila kupingwa kwenye nafasi zote nchi nzima. Wanatumia maneno makali yenye kuonyesha wana msimamo mkali na ujasiri ambao hatujawahi kuona wakiuonyesha kwa vitendo mahali popote.

These are all Paper Tigers, chui wa makaratasi aliowasema Mwenyekiti Mao Zedong. Tukiwasikiliza imekula kwetu na maCCM watachekelea all the way to the bank.

Tufanyeje???

Niliizungumzia hii wiki iliyopita na sina haja ya kuirudia hapa. Tujielewe na tuelewe hali yetu ya sasa relative to hali ya jana na ya juzi.

Tunaelewa hali yetu ya sasa kwa sababu kila mmoja wetu anaona yanayotendeka. Hata hivyo, uelewa wetu wa sasa hautoshi kututabiria kesho yetu.

Ili tuelewe kesho yetu itakuwaje, ni lazima tuelewe jana na juzi yetu ilikuwaje. There's no telling the future without knowing the past and understanding the present.

Tusikubali ujasiri feki na ushauri wa sumu wa hawa wanaojiita 'Marafiki' zetu. Tusikubali kutengenezewa ugomvi wa bure baina yetu na viongozi wetu na hawa wanaojifanya wana uchungu na Chama.

Tusikubali kupotezewa focus kwa kuaminishwa kuwa adui ni Mbowe au Mashinji au Mnyika; wakati adui halisi ni yule aliyemuua Mawazo na kumpoteza Ben Saanane au kumjeruhi Tundu Lissu.

Tuelewe mazingira yetu, tujielewe sisi wenyewe na tuwe na nidhamu ndani na nje ya Chama.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna Swali moja tu ambalo halijibiwi na hata kwenye hili andiko halijagusiwa... Kwanini tumerudisha fomu za uteuzi siku ya mwisho kabisa? Au sheria za uchaguzi zinataka uchukue fomu na kurudisha siku hiyo hiyo. Otherwise, haya maneno meengi ya lissu ni porojo tu.

Kwasababu kama tunajua hizi figisu zote kwanini hatuchukui fomu na kuzirudisha mapema?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuanze na ufafanuzi huu wa Lissu. "Mgombea anatakiwa kuwasilisha fomu ya uteuzi kabla ya saa kumi, SIKU MOJA kabla ya SIKU YA UTEUZI"
Rejea clip ya kiongozi wa kanda Chadema, kwa nini wagombea walirudisha fomu Siku ya uteuzi na si siku moja kabla ya siku hiyo?

Hata wa ccm alirudisha siku hiyohiyo na akatangazwa kupita bila kupingwa! !
 
waliomshambulia TL wamepata walichokitaka,walitaka kuipiga sehemu ya ubongo inayohusika na reasoning ili jamaa hashindwe kujenga hoja,sijaona kitu cha muhimu alichoongea jamaa tokea aende Nairobi then Brussels.MBOWE SIO MTU
Akili yako imeteguka utaonaje umuhimu wa alichoongea Lisu
 
Dawa ni kufanya maamuzi magumu.

Bila na wao kupata misukosuko, kamwe hawawezi kuja kwenye meza ya mazungumzo wala kuona umuhimu wa kutusikiliza(these people are callous and therefore they are enjoying what they are doing).

In short, this regime is worse and needs special treatment(they deserve similar treatment).
Magufuli ni Dikteta mshamba Sana, huyu tukimchekea atatumaliza wote, cha msingi tuunde strategies zetu kuhakikisha kuwa tukipoteza na wao wapoteze

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom