Tundu Lissu: Paper Tigers wanatushauri tususie chaguzi zijazo ili CCM wapite bila kupingwa

Dawa ni kufanya maamuzi magumu.

Bila na wao kupata misukosuko, kamwe hawawezi kuja kwenye meza ya mazungumzo wala kuona umuhimu wa kutusikiliza(these people are callous and therefore they are enjoying what they are doing).

In short, this regime is worse and needs special treatment(they deserve similar treatment).
zilongwa mbali zitendwa mbali
 
Tangu 1995 hamjajifunza mbinu za kukabiliana na njama hizo zinazojirudia kwenye chaguzi zote ni kielelezo kuwa hata ninyi ni sehemu ya tatizo. Kwanini wagombea wa upinzani wasubiri hadi siku ya mwisho ya kurudisha fomu hizo kumbe kuna mbinu kama hizo kila uchaguzi? Tusidanganyane humu, viongozi wetu na wagombea wanavuta mkwanja mrefu kutoka upande wa pili kwenye hili. Siku ya mwisho utamsikia mgombea akisema nimetekwa, nimenyang'anywa, nimefungiwa chooni, hayupo ofisini. Nini kilikufanya usirudishe fomu jana, juzi, au juzi ileeee?
 
Naomba na mimi kuchangia mjadala huu kidogo. Na mapema kabisa niwaombe radhi wote nitakaowakwaza, kwa sababu nafikiri nitakachosema kitawakwaza wengi humu.

Nimefuatilia mjadala wa yaliyojiri Korogwe Vijijini na nikiri nimeshuhudia utoto wa kisiasa wa kutisha na kusikitisha sana. Nimeona kile ambacho Lenin alikiita 'an infantile disorder' miaka mia moja iliyopita. Naomba kufafanua.

Sheria ya Uchaguzi na Kanuni zake zinaelekeza kwamba mgombea anatakiwa kuwasilisha fomu za uteuzi kabla ya saa kumi ya siku moja kabla ya siku ya uteuzi.

Sheria inasema fomu za uteuzi zitakabidhiwa kwa Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo. Maadili ya Uchaguzi yameelekeza wazi kwamba Msimamizi wa Uchaguzi anatakiwa awepo ofisini kwake wakati wote anaotakiwa ili kupokea fomu za uteuzi za wagombea.

Kwa hiyo, kitu cha kwanza cha kujiuliza ni je, mgombea wetu alipeleka fomu zake za uteuzi kwa wakati uliowekwa kisheria au hakufanya hivyo???

Kama alifanya hivyo, je, kwa nini fomu zake hazikupokelewa??? Kama hakufanya hivyo ni kwa nini na lawama iangukie wapi???

Baada ya kupata jibu la swali la kwanza, swali la pili ni je, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo alikuwepo ofisini kwake kwa wakati wote aliotakiwa kuwepo ili kupokea fomu za uteuzi za wagombea???

Kama alikuwepo je, alipokea fomu za uteuzi za wagombea kama inavyotakiwa na Sheria??? Kama hakuwepo, je, ni kwa nini na lawama iangukie wapi???

Kwa ninayoyasoma mitandaoni, mgombea wetu alipeleka fomu zake za uteuzi kwa wakati muafaka. Na wala hakuwa peke yake, walikuwepo wagombea wa CCM na ACT-Wazalendo.

Kwa ninayoyasoma mitandaoni, wagombea walipofika ofisini kwa Msimamizi wa Uchaguzi wakakuta hayupo ofisini kwake wakati aliotakiwa kuwepo. Inasemekana alikuwa ameitwa kwa Mkuu wa Wilaya.

Fomu za mgombea wetu na wa ACT-Wazalendo hazikupokelewa lakini, somehow, fomu za mgombea wa CCM zikabandikwa ukutani na mara akatangazwa kuwa amepita bila kupingwa!!!!

Je, aliyekosea hapa ni nani??? Je, ni mgombea aliyepeleka fomu zake za uteuzi kwa wakati??? Je, ni Katibu wa Wilaya ya Korogwe Vijijini au wa Mkoa wa Tanga??? Au Katibu wa Kanda ya Kaskazini huko Arusha??? Au Katibu Mkuu na maafisa wake Dar Es Salaam??? Au Mwenyekiti wa Chama ambaye yuko kortini Kisutu kila siku???

Jibu la baadhi ya 'Marafiki wa BAVICHA Original' humu ndani ni kwamba viongozi wetu, hasa wa juu, ndio waliosababisha yote haya!!! Sio Msimamizi wa Uchaguzi aliyekimbia ofisi wakati anaotakiwa awepo ili kupokea fomu za uteuzi.

Sio Magufuli aliyejaza makada wa CCM walioshindwa uchaguzi uliopita kama Wakurugenzi wa Halmashauri na, kwa hiyo, kuwafanya wasimamizi wa uchaguzi.

Sio mapolisi waliotumwa kwenda kuwatawanya wagombea ambao fomu zao za uteuzi hazikupokelewa.

Wale waliopewa jukumu la kupokea fomu za uteuzi za wagombea wote na Sheria za nchi yetu; na Bosi wao aliyewakataza hadharani kutenda haki, hao hawana lawama.

Wahalifu halisi hawana makosa; waliofanyiwa uhalifu ndio wanaolaumiwa na hawa wanaojiita wanaCHADEMA au marafiki wa BAVICHA Original.

Halafu tukisema kuna watu wanamtumikia shetani kwa kuelewa au kutokujielewa, people take offence.

Halafu 'Marafiki' hawa wanaleta vihoja kwamba haya yanatokea kwa sababu ya Katibu Mkuu wa sasa; hayakuwa yanatokea wakati Dr. Slaa akiwa Katibu Mkuu, etc.

Wenye hoja za aina hii wanafikiria wanajua, ni werevu, wasomi, n.k. Ni wajinga wasiojua wasemalo.

Kabla hamjasema sana muwe mnawauliza akina Tony Komu na Joe Selasini na James Mbatia na wengineo ambao wameshiriki hizi vita tangu kabla ya kuingia mfumo wa vyama vingi vya siasa.

Au sisi wengine, mimi mmojawapo, ambao tumeshiriki kwenye uchaguzi tangu mwaka '95. Haya ya sasa sio mapya sana.

Hii habari ya wasimamizi wa uchaguzi kukimbia ofisi zao ili wasipokee fomu za uteuzi za wagombea wa upinzani haikuanza Korogwe Vijijini. Ilikuwepo tangu mwaka '95 wakati wa Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi.

Wagombea wetu kuwekewa mapingamizi ya ajabu ajabu na kuenguliwa kiharamia na maCCM kupitishwa bila kupingwa haikuanza na Magufuli na watu wake. Ilianza Ali Hassan Mwinyi akiwa Rais na Ben Mkapa mgombea Urais.

Wagombea wa CCM kutangazwa kwa nguvu haikuanza na Magufuli. Ilianza Mkapa akiwa Rais na baadae ikarithiwa na Kikwete na imepokelewa na Magufuli. Kumbukeni ya marehemu Shelembi wetu Shinyanga Mjini mwaka '10 na ya David Kafulila mwaka '95 wakati Rais akiwa Kikwete.

Kuna wakati maCCM, wakisaidiwa na mapolisi kama ilivyo sasa, walikuwa wanateka magari ya Tume yenye masanduku ya kura halali na kuyabadilisha na masanduku yenye kura haramu kwa lengo la kuwashindisha wagombea wa CCM.

Wagombea au wabunge wetu kujiuza kama malaya kwa maCCM haikuanza na akina Waitara na ole Kalanga. Tuliwahi kuwa na wabunge kama Makongoro Nyerere na Dr. Masumbuko Lamwai na Danhi Makanga na Daniel Nsanzugwanko huyu huyu wa CCM ya sasa. Nani anayewakumbuka tena???

Tuliwahi kuwa na wanamageuzi maarufu kama Prince Bagenda na Chief Abdallah Fundikira na wengineo wengi walioishia kujiuza CCM.

Licha ya haya yote, hatukuwahi kufikiria kuacha kushiriki kwenye chaguzi za marudio au Uchaguzi Mkuu.

Tulijua uchaguzi ni vita, na vitani kuna kushinda au kushindwa; kuna kufa au kujeruhiwa au kutekwa, na kuna kuua au kujeruhi au kuteka.

Hawa 'Marafiki' waliokuja jana na leo asubuhi wameshuhudia tukipigwa na Magufuli na watu wake wa CCM ya sasa na tayari wanatushauri tunyanyue mikono juu na kusalimu amri mbele ya watesi wetu.

Wanatushauri tususie chaguzi zijazo ili maCCM yapite bila kupingwa kwenye nafasi zote nchi nzima. Wanatumia maneno makali yenye kuonyesha wana msimamo mkali na ujasiri ambao hatujawahi kuona wakiuonyesha kwa vitendo mahali popote.

These are all Paper Tigers, chui wa makaratasi aliowasema Mwenyekiti Mao Zedong. Tukiwasikiliza imekula kwetu na maCCM watachekelea all the way to the bank.

Tufanyeje???

Niliizungumzia hii wiki iliyopita na sina haja ya kuirudia hapa. Tujielewe na tuelewe hali yetu ya sasa relative to hali ya jana na ya juzi.

Tunaelewa hali yetu ya sasa kwa sababu kila mmoja wetu anaona yanayotendeka. Hata hivyo, uelewa wetu wa sasa hautoshi kututabiria kesho yetu.

Ili tuelewe kesho yetu itakuwaje, ni lazima tuelewe jana na juzi yetu ilikuwaje. There's no telling the future without knowing the past and understanding the present.

Tusikubali ujasiri feki na ushauri wa sumu wa hawa wanaojiita 'Marafiki' zetu. Tusikubali kutengenezewa ugomvi wa bure baina yetu na viongozi wetu na hawa wanaojifanya wana uchungu na Chama.

Tusikubali kupotezewa focus kwa kuaminishwa kuwa adui ni Mbowe au Mashinji au Mnyika; wakati adui halisi ni yule aliyemuua Mawazo na kumpoteza Ben Saanane au kumjeruhi Tundu Lissu.

Tuelewe mazingira yetu, tujielewe sisi wenyewe na tuwe na nidhamu ndani na nje ya Chama.

Sent using Jamii Forums mobile app
Moja ya mapungufu ya Lissu ni academic arrogance. Anaweza kuwa na hoja za msingi lakini uwasilishaji wake umetawaliwa na dharau flani. It is as if yeye ni mwenye hakimiliki ya ukweli.

Hilo linaambatana pia na amani yake kuwa siku zote yupo sahihi. Huenda hilo linachangiwa zaidi na aina ya wafuasi wake. You see, tofauti ya wafuasi wa Chadema na wa CCM ni ndogo sana, na kubwa pekee ni pale tu maslahi ya vyama vyao yanapokuwa hatarini.

Kama ambavyo ni mwiko kwa mwana-CCM kumkosoa Jiwe ndivyo ambavyo ni sawa na uhaini kumkosoa Mbowe au Lissu. Hawa "malaika" wapo sahihi siku zote, na kila litokalo midomoni mwao ni sahihi.

Suala la msingi ambalo Lissu analikwepa kwenye povu lake ni kwamba kwanini fomu irudishwe siku ya mwisho ilhali uzoefu umeonyesha uwepo wa hujuma kila inapofanyika hivyo. Labda sheria inataka fomu zirudishwe siku ya mwisho, na badala ya kulalamikia sheria mbaya, jitihada zielekezwe kuibadilisha.

Lissu anarudia kutusimulia historia ya hujuma zinazofanywa na CCM dhidi ya upinzani na kwa namna flani anataka kutuaminisha kuwa yanayojiri kwenye utawala huu wa Magufuli hayana tofauti na yaliyojiri huko nyuma.

Kwa vile wafuasi wake ni kama kondoo, mtazamo huo wa Lissu umekubalika bila kumhoji "Hivi ni mara ngapi amekuwa ukijaribu kutuaminisha kuwa, "HAIJAWAHI KUTOKEA..." kila anapoongelea utawala wa Magufuli?

Na katika hili la kuwa "hayakuanza leo" he is very wrong. Na mtazamo wake huu fyongo kwa bahati mbaya au makusudi is shared na wana-Chadema wengi, kwamba "yalishatokea sana huko nyuma lakini bado tupo hai hadi leo." It is true kuwa hujuma dhidi ya Chadema na upinzani kwa ujumla hazijaanza leo, lakini hizi tunazoshuhudia hazijawahi kutokea.

Never before have we witnessed Great Migration like one inayoendelea. Kibaya zaidi, pomoja na kauli zake za dharau, Lissu ameshindwa kutueleza if the worse is past or yet to come. I would put my bet on the latter.

Ni hivi, lengo la Jiwe ni kuhakikisha upinzani unakufa kwa gharama yoyote ile. Na mkakati wake mkuu ni kuunyong'onyeza upinzani muda huu kiasi kwamba kila mbunge mpinzani atakuwa worried zaidi kuhusu kurudi bungeni kuliko utiifu kwa chama au huduma kwa wanajimbo.

Lissu hawezi kuwaambia wana-Chadema kuhusu uwezekano wa chama hicho kutokuwa na mbunge hata mmoja mwaka 2020, kitu ambacho ndio sehemu muhimu ya mkakati wa Jiwe.

Labda ni sahihi kwa Lissu kuwakebehi wenye hofu kuhusu mustakabali wa Chadema na upinzani kwa jumla lakini mbadala wa kebehi hizo hauwezi kuwa matumaini hewa.

Sawa, hata huko nyuma wapinzani waliwahi kuhama kwenda CCM lakini ni mpuuzi pekee atakayepuuzia ukweli kuwa kasi ya kuhama inayojiri sasa haijawahi kutokea katika historia ya Tanzania. Na kibaya zaidi, dalili za kudhoofika kwa upinzani sio tu ziko wazi bali zinazidi kuongezeka.

Ni rahisi pia kupuuzia uwezekano wa mwendelezo wa trend ya Magufuli ya CCM kushinda kila uchaguzi tangu aingie madarakani. Naam twajua anashinda isivyo halali lakini pia hatujashuhudia upinzani ukisimama kidete dhidi ya matokeo ya uchaguzi usio huru wala wa haki. Upinzani pekee ni kelele za "tunaonewa" au "yana mwisho haya." Mbona mgao wa umeme umedumu hadi leo na hakuna dalili za mwisho, na maisha ya Watanzania yanaendelea tu huku wapo bize na UBUYU?

Wito wangu kwa Lissu ni kujifunza kwa wenzie kama Mbowe au hata Zitto au pengine Dkt Slaa, mwanasiasa aliyekuwa na uwezo mkubwa wa kuwasilisha hoja bila jazba wala kutumia lugha isiyopendeza.

Na what if hao "Paper Tigers" happen to be not wrong? Will Tundu Lissu have the audacity to apologise?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dawa ni kufanya maamuzi magumu.

Bila na wao kupata misukosuko, kamwe hawawezi kuja kwenye meza ya mazungumzo wala kuona umuhimu wa kutusikiliza(these people are callous and therefore they are enjoying what they are doing).

In short, this regime is worse and needs special treatment(they deserve similar treatment).
.....
......wellNoted Mkuu
 
Ndugu Lissu,

Tunashukuru kwa neema ya mwenyezi mungu, as it shows your rapid mending process.

Kwenye huu uzi wako, its very unfortunate, umechukua jukumu la kuelezea ukweli kwa maoni yako, na pia kutumia lugha ya kuwatusi na kuwadhalilisha wanachama na viongozi wenzako chamani,
QUOTE
""Malaya wa kisiasa wanaojiuza "

Ndugu huwezi kuzungumzia issue yoyote bila Jazba, kebehi na matusi. You have to know that you are leader with a lot of young followers. What tupe of example do you want to be?

Ndugu jibalishe na badilsha lugha yako, na simaanishi badilisha uwanaharakati wako.

Hao unaowadhalilisha Bavicha Asilia, ni wanaharakati kama wewe, wamekipigania chama na wanastahili heshima.

Umewataja wahama chadema kama malaya wa kisiasa, lakini wanaohama CCM kuja Chadema wao sio malaya bali mashujaa!!!!

What a wishy washy thoughts.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sikuwahi kutoa pole kwa Magufuli na sitotoa. Aliyefiwa na dada yake ni adui yangu kisiasa na kiubinadamu. Naamini kuwa wapinzani wameonewa sana ila kwenye huu utawala wa Magufuli maonevu yamekithiri.
Pole yako ingemfufua marehemu?
Hata ungeitoa, anakujua? Tukutane 2020
 
"Chui wa Kuchora !!! " Ha ha ha

CDM itapata marafiki wengi sasa ila
wengi wao ni Chui wa kuchora; kwa kuandika & kukosoa mafundi balaa ila bomu likipigwa ni uvunguni...wiki hawatoki ndani.
 
Mmmh hizi kauli zinachoma Sana "Malaya wa kisiasa wanaojiuza "

Nimenukuu hilo neno kumbe inapaswa tuwaite as Titled above

Hii Ingekuwa Press Dar ni balaa, Maneno yataumiza sana hasa akisoma yule mkurya mwenye sura mbaya na hovyo
Mkurya amekuwa na sura mbaya baada ya kukihama chama, lakini alipohama ccm na kuja cdm, alikuwa jasiri mzuri.

Jee kina Lowasa,Sumaye, na wale wengine wote walijiunga na cdm kutoka ccm, nao wataitwa hilo jina?

Mbona nyie ndio mnafanya siasa za kinafiki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ajabu kwa kweli mtu aliyepo kwenye matibabu nje ya nchi eti ndio anona anaujua ukweli kuliko waliokuwepo eneo la tukio. Halafu hii mindset ya kuona Chadema haikoseagi hata siku moja ndio inayowamaliza kila siku.
kuna hoja hapo zinahitaji majibu; hatuongelei ugonjwa wa mtu hapa.
1. Kwa nini msimamizi hakuwepo ofisini siku ya urejeshwaji wa form unaotambulika kisheria?
2. Je ni kwa namna ipi form za mgombea wa CCM zikapokelewa wakati naye alikuwa anasubiri kwenye benchi nje ya ofisi?
3. Je Mbowe anahusika kwenye sakata hili la kutopokelewa form ya mgombea wake kwa namna ipi?
4. Je ofisi ya Katibu Mkuu CDM pia inahusika kutopokewa kwa form hii? Kwa namna ipi?
5. Je Sheria ya uchaguzi inasemaje juu ya vifungu vya kuchukua form kujaza na kurejesha? Unachukua kwa nani na unarudisha kwa nani kwa muda upi?

Hizi ndizo hoja unatakiwa kuzijibu ama kuzitolea ufafanuzi then uje sasa na conclusion yako.

Usije na wewe ukawa kwenye kundi la Chui wa Karatasi - Jitoe.
 
Ajabu kwa kweli mtu aliyepo kwenye matibabu nje ya nchi eti ndio anona anaujua ukweli kuliko waliokuwepo eneo la tukio. Halafu hii mindset ya kuona Chadema haikoseagi hata siku moja ndio inayowamaliza kila siku.
Kwahiyo haya aliyoyasema siyo ya kweli na kama siyo tupe ukweli unaoujua? tuletee hapa ukumbini tuamini ukweli wako ukishindwa hayo katafute dume.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom