Kwa NEC hii - tawi la CCM - hata apate kura zote hawawezi kumtangaza kuwa mshindi. Lakini kwangu mimi ninaona alichofanya katika kipindi hiki cha kampeni ni USHINDI wa aina ya pekee. Magufuli ame-terrorize kila segment ya jamii kwa kipindi cha miaka mitano: neno alilotamka hata kama ni kukohoa limekuwa sheria, wanasiasa walifungiwa kufanya siasa, bunge likafungiwa kufanya kazi za kutetea wanananchi na kuwajibisha serikali likabaki kupongeza kila utopolo, tasnia ya habari ikawekwa makufuli, wanataaluma wakageuzwa kuimba nyimbo kama watoto wa chekechea -
hakuna tena tafiti za maana labda zile zitakazotoa majibu ya kupongeza, watu walipigika lakini wakawa hawana pahali pa kupazia sauti zao, nk nk. Pamoja na vikwazo alivyowekewa na vyombo vya dola na vya binafsi (kwa maagizo ya Magufuli) TAL amekuwa jasiri, amekuwa na uthubutu katika kipindi hiki cha kampeni na hivyo kuwa SAUTI ya walionyongenyezwa, walio wengi - the people.
Watu wamejisikia ahueni katika vichwa na mioyo yao, na kuwa na matumaini yaliyotoweka. HONGERA SANA TAL umetimiza wajibu wako na utabakia katika historia ya mashujaa wa nchi hii. Pia HONGERA kwa 'wanyonge wa magufuli' (wananchi wa kawaida) kwa kumdhihirishia mbele ya macho ya dunia kuwa nyie sio wajinga kama ambavyo yeye na timu yake ya akina polepole wametokea kujiaminisha ama kutaka kuuaminisha ulimwengu kuwa anapendwa sana pamoja na ufedhuli wake. Wananchi wa Tz (ukiweka kando wasomi ambao ni wa binafsi na hivyo kuishia kujipendekeza kwa mafedhuli) na nyie ni MASHUJAA. Huu ni ushindi!!!!