Pamoja na yote yaliyomkuta, Tundu Lissu hakuogopa kurudi nyumbani na tena sio kurudu tu bali kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na aliporudi hakukaa kimya amezungumza ukweli wote wa mambo bila chembe ya uoga.
Hata baada ya hila za kila aina dhidi yake na wagombea wa CHADEMA, Lissu ameendelea kufanya kampeni zenye mvuto kuliko zote katika kila mkoa na wilaya za nchi yetu.
Tundu Lissu amewafungua watanzania macho, amewafanya wajisikie huru tena amewarudishia matumaini na kuwafanya wajiamini tena na kuthubutu kutumia uhuru wao.
Hatimaye Tundu Lissu amemaliza kampeni zake leo pamoja na kuzuiliwa na kuwekewa mizengwe kila mahali Lissu amemaliza mwendo kwa ufanisi mkubwa!
Hima hima mtanzania usifanye kosa kumchagua mtu ambaye hana maono wala huruma kwa watanzania, sote tumchague Tundu Antipas Lissu awe rais wetu 2020-2025.
Mungu mbariki Tundu Lissu, Mungu ibariki Tanzania. Nawatakia uchaguzi mwema!