Tundu Lissu na CHADEMA mnavuna mlichopanda!

Tundu Lissu na CHADEMA mnavuna mlichopanda!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
17,547
Reaction score
28,494
Kwa mwaka mmoja tu uliopita, mtu angekuambia CHADEMA itakuwa kama ilivyo leo ungebisha sana. CHADEMA imefanya some strategic blunders ambazo zimekigharimu chama pakubwa.

Moja nikubadili uongozi wa juu katika mwaka wa uchaguzi, hata kama sababu zilikuwepo.

Pili, u-one man show wa kiongozi Tundu Lissu, umefanywa kuwa rahisi kushughulikiwa na CCM na serikali yake.

Mimi mwana CCM lakini kama Mwalimu alivyosema kama upinzani ukiwa lege lege, hata chama kilicho madarakani kitakuwa legelege. CHADEMA lazima wawe na Think Tanks na Strategists siyo mawazo ya mtu mmoja.

Huko kwenye ubwabwa wa CHAUMMA ni kujipotezea muda tu.
 
Mazingira anayopitia Lissu ya vizingiti vya kisiasa yangeweza kumfanya mwanasiasa mwingine kukubali hongo ili apate nafuu.

Lakini Lissu amekuwa mfano wa nadra wa mtu anayekataa kupoteza mwelekeo wa kisiasa kwa ajili ya manufaa binafsi.

Ni kweli kwamba Lissu ana sauti kubwa ndani ya CHADEMA, lakini hiyo ni kwa sababu ya msimamo wake usioyumba.

Kama tungekuwa na viongozi wengi wa aina yake, upinzani nchini ungekuwa imara zaidi, na demokrasia ingepata nafasi ya kustawi.
 
Wengi wao walishindwa kung'amua mapema kama lile lilikuwa goli aka frame ya biashara.
Na shida yao kubwa ni ujuaji hasa pale wanapogutuliwa.

Walitahadhalishwa juu ya biashara ya EL miaka mingi nyuma kabla ya 2015, wakawa wanakaza shingi.
Wakatahadhalishwa tena juu ya FAM wakawa wanakaza shingo na matusi juu..

Awamu ya nne wakapambana sana na JPM huku wakiwaunga mkono mtandao na kuwabatiza jina wafuasi wa JPM Sukima gang, wengi wakawa upande wa team JK na kumsifia sana JK.

Awamu ya tano paah, mwanzoni wakamsifia sana mama na kumuunga mkono kwenye 4R..
Huku wakiwaponda na kuwazodoa Sukuma gang.
Ghafla wamemgeuka mama wapo upande wa Sukuma gang na kumshambulia JK, RA na mtandao( their former allies).

Kifupi huu ukigeu, geu na kukosa misimamo, ujuaji, muendelezo wa sera na mambo yao ndio kunawafanya waonekane hawako serious na mara nyingi hutumika kama bargain chip halafu wanabwagwa.

Safarini Hodeidah Yemen
 
Kwani unayoyaona unafikiri yametoka hewani tu!
Umetoka nje kabisa ya nilichokuambia ufanye.
Achana nayo Kama iko nje ya uwezo wako.

BTW, naona mnasumbuka sana na CHADEMA, tatizo liko wapi?
Nyie subirini mkatiki huko kwenye igizo.
Achaneni na wanaovuna walichopanda.
 
I think hapa kuna typing error,

Nadhan ulitaka kuwasema cuf ambao Wana kila kitu na wako huru

Chadema wamefungwa kila kitu, hawana ruzuku, hawana office, mwenyekiti yuko jela

Yan they lost everything

So hoja yako nadhan ulikuwa unawalenga cuf na sio chadema
 
Back
Top Bottom