Tundu Lissu na CHADEMA mnavuna mlichopanda!

Tundu Lissu na CHADEMA mnavuna mlichopanda!

Endeleeni na uchaguzi wenu wa maigizo.Chadema ilibidi wapambanie kile wanachokiamini, mchezo wa kutegemea huruma za chama cha mapinduzi haufai ni bora kutoshiriki kabisa
Hili halikuwa lengo lakn.
Tukizingatia malengo ya chadema ilikuwa kuzuia uchaguzi. tuliaminisha umma kuwa hapatakuwa na uchaguzi mwezi wa 10.
Sasa tumegeuka tunasema wanashindana na kivuli chao wenyewe, kitu ambacho ni kweli.
Kufanikiwa kwa CCM kufanya uchaguzi kunadhihirisha kuwa wenzentu walikuwa mbele ya muda na walijiandaa vyema, chadema tulikurupuka ndio maana leo hii tumeishia kubadiri kauli zetu.

Ukweli ni kwamba maamuzi ya CDM hayakuwa maamuzi sahihi na wanajuta ingawa hawawezi kuonyesha wazi ila huo ndio ukweli
 
Sijakuelewa kabisa hapo, halafu wewe ni mkongwe hapa! Ngoja uone baada ya miaka miwili nchi itakuwaje, nchi haina check and balance, inaends kama gari bovu, mie napongeza sana Chadema, maana hii inflation itakayokuja itakuwa zaidi ya ruksa zama zile, siujui hebu niambie kuna nini kilichobaki? Servicing the debts, si umeona hadi TRĄ sasa hivi ni kama “captured”? Miradi yote itasimama na services zitasimama. Wananchi ndiyo watapata akili, maana itakua survival of the fittest.

Hili siyo suala la Chadema, letu sote.
 
Chadema wapumbavu sana


Wewe una uwezo wa kujua nani ana akili na nani hana akili? Kama huwezi hata kutambua kuwa wewe ni mwendawazimu, huo uwezo wa kutambua wenye akili, utaupata wapi?
 
Mada zako unazoandika, Unatumia neno Moja la Kingereza 'Blunders', kwalo unajiona umeandika Kwa kutumia akili na Umekaa ukafikiria ukaanza kuandika.


Hivi kua Mwanaccm unatakiwa kwanza uwe mjinga ndio ujiunge CCM au unakua kwanza Mwanaccm Kisha unakua Mjinga???.
 
Mmeitengeneza chauma na kuivuruga chadema, ila cha ajabu bado mnaumia ninyi ninyi. 🤔🤔🤔
 
Sija kuelewa Wala hujaeleweka na Wala huzijui hoja zao, lisu Yuko jela lakini Kila siku anaanzishiwa nyuzi hapa jukwaan. Kutokuwepo CHADEMA nalisu si ndio furaha yenyewe yaani kama vile yanga wangekataa kuleta timu uwanjani unafikiri nani angefurahi
kinachonekana wanaCCM wengi wanahangaishwa na kutokuwepo Kwa CHADEMA uwanjani mechi imepwaya sana

Sisi tulioamua kutiki tukatiki tuachane na CHADEMA. Hivi hao walio amua kuingia uwanjani mbona na wao wameanza kupoteana kunani huko? Mfano ACT na CHAUMA wako wapi? Timu Moja inasikika zingine zipo wapi?

Inawezekekana Kuna watu wanataka kuachana na Siasa za maigizo na kujaza tumbo wakati wengine wananeemeka Kwa kupitia misaada ya kupritend kuwa Kuna Demokrasia na vyama vingi. Upinzani wa kweli unataka watu serious mbao wanaangalia kesho siyo Leo tu. Kazi na utu
 
Kwa yanayoendelea, kwa mtu yetote mwenye akili timamu na uelewa mkubwa, anajua kuwa CHADEMA ya sasa ni imara kuliko iliyokuwepo, ukiiacha ile ya wakati wa Dr. Slaa.

CHADEMA ya sasa ni ya chama chenye msimamo imara katika inayoyapigania, siyo ile CHADEMA ya kuvizia ruzuku.
 
Mazingira anayopitia Lissu ya vizingiti vya kisiasa yangeweza kumfanya mwanasiasa mwingine kukubali hongo ili apate nafuu.

Lakini Lissu amekuwa mfano wa nadra wa mtu anayekataa kupoteza mwelekeo wa kisiasa kwa ajili ya manufaa binafsi.

Ni kweli kwamba Lissu ana sauti kubwa ndani ya CHADEMA, lakini hiyo ni kwa sababu ya msimamo wake usioyumba.

Kama tungekuwa na viongozi wengi wa aina yake, upinzani nchini ungekuwa imara zaidi, na demokrasia ingepata nafasi ya kustawi.

Umeandika ukweli mtupu!
 
Back
Top Bottom